"Better to write for yourself and have no public, than to write for the public and have no self."
Cyril Connolly (1903 - 1974)
Sunday, October 17, 2010
Mwalimu Nyerere aenziwa Marekani
Jumamosi ya Oktoba 16, waTanzania, waAfrika na waMarekani wenye asili ya Afrika walijumuika katika kukumbuka kazi na Maisha ya Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere. Katika sherehe hizo, zilielezwa kazi za Mwalimu Nyerere, umuhimu wake kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Maajar, alieleza kazi kuu alizofanya Mwl Nyerere ikiwa ni pamoja na kuunganisha umoja kwa nchi yenye makabila 120, dini mbalimbali, na kuhimiza lugha ya Kiswahili na pia kusaidia kuunganisha Afrika kama anavyosema hapa chini
Baada ya maonesho nilibahatika kuongea na Balozi Mwanaidi Maajar kuhusu ufahamu wake juu ya Mwalimu Njerere na pia ambacho anaamini Mwl angekemea kama angekuwa hai
Lakini pia tulipata nafasi ya kusikiliza WOSIA kutoka kwa Brother Hodari Abdul Ali, mMarekani mwenye asili ya Afrika aliyezungumzia ziara yake ya Tanzania akiwa mwanafunzi, uelewa wake kuhusu Tanzania, Afrika na pia umuhimu na faida ya ushirikiano kati ya waTanzania na waMarekani wenye asili ya Afrika. Bwn Hodari ni Mkurugenzi wa Give Peace a Chance Coalition (G-PAC), mtangazaji wa WPFW Pacifica Radio na mmiliki wa duka la vitabu liitwalo Dar Es Salaam lililopo Maryland nchini Marekani.
Na hizi hapa chini na baadhi ya kumbukumbu zilizonaswa na kamera ya blogu hii Waandaaji na wafanikishi wa kumbukumbu ya maisha na kazi za mwalimu wakiwa na Balozi Maajar Bwn na Bibi Tingling Bwn Hodari. Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyebahatika kwenda Tanzania na kuonana na Mwl Nyerere miaka ya 70. Na sasa ana suka la vitabu liitwalo Dar Es Salaa. Alikuwa akitoa neno Mkuu wa Ukimwi Orphans Dr Lutayuga akitoa hotuba Balozi Maajar na Afisa wa ubalozi Suleiman Saleh wakifurahia maonesho ya mavazi ya wabunifu saba wa nchini Tanzania waliowakilishwa na Khadija Mwanamboka kama yaonekanavyo hapa chini Waonesha mitindo / mavazi wakiwa katika picha ya pamoja
Baada ya maadhimisho nilipata nafasi ya kuhojiana na Khadija Mwanamboka kuhusu kazi ya ubunifu. Alipoanzia, alipo na anapoelekea. Huyu hapa chini Khadija Mwanamboka
.Today we have bigger houses and smaller families; more convenience but less time. .We have more Degrees but less common sense; more knowledge but less judgment. .We have more experts but more problems; more medicine but less wellness. .We spend too recklessly, laugh too little, drive too fast, get too angry too quickly, stay up too late, read too little, watch Tv too much and Pray too seldom. .We multiply our Possessions but reduce our values; we talk too much, love too little and lie too often. .We’ve learned how to make living, but not a life; we’ve added years to life not life to years. .We have taller buildings, but shorter tempers; wider freeways but narrower viewpoint. .We spend more, but have less; we buy more, enjoy less. .We’ve been all the way to the moon and back, but have trouble crossing the street to meet our neighbor. .We’ve conquer outer space, but not inner space. .We split the atoms, but not our prejudice .We write more, learn less; plan more but accomplish less; we’ve learned to rush but not to wait; we have higher income but lower morals. .We build more computers to hold more info, to produce more copies but have less communications. .We’re long on quantity but short on Quality. .These are the time for Fast food and slow digestion; tall men and short characters. .More leisure but less fun; more kinds of food but less nutrition; two income but many divorces, fancier houses but broken homes.
1 comment:
Asante KUBWA saaaaana Mubelwa. Yaani ile THANK YOU BIIIIG kabisa.
Post a Comment