Friday, July 5, 2013

Mchungaji Emmanuel Mgaya (MASANJA MKANDAMIZAJI) kuhubiri Washington DC Jumapili hii

Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara maalum, atahudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya kesho (Jumapili 07/07/2013)
Bwn. Mgaya ambaye pia hufahamika kama Mchungaji Mtarajiwa  na ambaye amekuwa akifanya huduma ya uhubiri nchini Tanzania, atahubiri katika ibada ya jumapili katika kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES katika ibada ya kawaida ya kila jumapili ambayo hufanyika kuanzia saa saba kamili mchana mpaka saa tisa kamili alasiri (1:00pm - 3:00pm)
Anwani ni
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740

Hii itakuwa ni huduma ya kwanza nchini Marekani kwa Mtumishi huyu ambaye ni Mchungaji msaidizi katika kanisa la EAGT Mito ya Baraka lililopo Kariakoo jimbo la Temeke jijini Dar Es Salaam likiongozwa na Askofu Bruno Mwakibolwa na ameshafanya huduma katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Mtumishi Emmanuel Mgaya akihubiri Neno la Mungu katika viwanja vya kanisa la Tanzania Assemblies of God, Mbagala Dar Es Salaam
Photo Credits: Ramsoict.com
Masanja akiwa kwenye moja ya mikutano ya Injili wilayani Nzega mkoani Tabora, katika Mkutano wa Injili ulioongozwa na Mtumishi wa Mungu Daniel Kulola
Photo Credits: Strictly Gospel
Bwn. Emmanuel Mgaya, ambaye pia anafahamika zaidi kama Masanja Mkandamizaji kupitia kazi za uchekeshaji wa kwenye luninga, yuko nchini Marekani kwa ziara maalum ya Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili linalofanyika leo Jumamosi (June 6, 2013)

No comments: