Tuesday, March 15, 2011

Lazima tupande ndio tuvune. Yaani tuwekeze ndio tunufaike.

Photo Credit: Qwota.com
"Everyone wants to go in heaven; but nobody wants to die" Ni mameno ya Winston Hubert McIntosh ama Peter Tosh alipoimba kwenye wimbo wa Equal Rights. Kwa ufupi naona kama linalohimizwa hapa ni suala la kutaka kuweka bayana kuwa kama unahitaji chochote lazima kuwekeza gharama zitakiwazo.
Natazama "mfumo" wa serikali uliopo na najiuliza kama unatoa changamoto kwa watendaji kusaidia walio na uhitaji. Yaani kama Rais na wabunge wote wanachaguliwa kwa wakti mmoja ina maana ikitokea wabunge wakawa wengi kutoka katika chama cha Rais basi hata wasipotekeleza ilani za uchaguzi hakuna wa kuhoji kwa nguvu bungeni. Lakini pia najiuliza kama serikali ni kwa ajili ya wananchi si ina maana wanatakiwa wafanye kila lililo ndani ya uwezo wao kuwezesha wananchi kufanikiwa? Unadhani itawezekana kama kufanya kila liwezekanalo itamaanisha serikali kuhatarisha nguvu zake za kiutawala? Kimsingi tutasema NDIO lakini kiitifaki itakuwa HAPANA.
Lakini bado najiuliza kama tungekuwa na chaguzi tofauti, kwa maana Marais na wakuu wa mikoa wakachaguliwa miaka miwili na nusu kabla ya wabunge na madiwani si ingekuwa safi? Kwamba kwa nusu muhula tunawaangalia na kuwasoma viongozi waliopo madarakani na kama hawatekelezi lolote "tunawamwagia upupu" kwa kujaza wapinzani wao kwenye uchaguzi ujao. Ndhani hii ingeamsha UTEKELEZAJI wa ilani za uchaguzi na pia ingewasaidia wananchi kupata kile wanachohitaji kutoka kwa wawakilishi na viongozi wao.
Najua watasema ni gharama, lakini kama ndizo zitakazowasaidia wananchi kutoka kwenye umaskini na ujinga kwanini zisitumike? Kuna gharama gani zaidi ya kuwa na taifa lenye uhitaji mkubwa leo kama ambavyo ilikuwa miaka 50 iliyopita?
Gharama lazima zitumike kuokoa taifa maana NI LAZIMA TUPANDE NDIO TUVUNE, YAANI TUWEKEZE NDIPO TUNUFAIKE

1 comment:

Unknown said...

Yawezekana nikawa nje ya mada!!. Hata hivyo bado kuna mambo ya kuzingatia katika kuamua kujenga mahusiano rasmi ambayo kwa kweli huwa ni mwanzo wa safari mpya kabisa ya kimaisha yenye malengo na mwisho tafauti na yale tuliyokuwa nayo katika mahusiano ya awali kama wananchi katika nchi moja.

Kimtazamo mimi;
Si kila kiongozi anaweza kugeuzwa kuwa rasmi kiasi hiki. Lazima tukubali kwamba jambo hilo linahusisha watu waliofikia umri wa kuweza kuamua kuhusu maisha ya wananchi kwa ujumla ya baadaye Tafauti na ya awali, kivipi.

Hata hivyo bila kusahau na kukataa ukweli kwamba, jamii inayotuzunguka bado ina nafasi yake kubwa sana kwa wahusika kuweza kufikia uamuzi wa kweli.

Ni kipindi cha kuelewana zaidi tena kiundani, kwani kile tutakachokiamua baadae kinatudai udumifu wa maisha yetu na maendeleo yote. Udumifu, heshima na sifa kwa hali yoyote, unategemea sana jinsi tulivyoyaanza,tulivyoyachukulia mambo na kuchambua na hasa bila kusahau kuwa ni kipindi cha kusali na kuomba mwongozo na msaada wa Mungu.