Saturday, September 20, 2008

"Tumepiga hatua japo tuna kazi nzito ya kufanya"- Balozi Amina S Ali


Mhe Balozi Amina Salum Ali akikisitiza jambo wakati akizungumza usiku wa leo

Wanachama wa Tanzanian University Women's Association (TUWA_USA) wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe Balozi Amina Salum Ali baada ya mazungumzo yake

Mhe Balozi Ali akijadili jambo na baadhi ya wahudhuriaji

Baadhi ya bidhaa zilizonadiwa kusaidia shule ya Msingi Amani

Watanzania popote duniani tumeombwa kukumbuka kuchangia kwa namna tutakavyoweza kuboresha elimu ya msingi ambayo licha ya mafanikio yaliofikiwa mpaka sasa, bado kuna mengi ya kushughulikia.

Wito huo umetolewa na mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Afrika nchini Marekani Mhe Amina Salum Ali alipokuwa akitoa NENO KUU kwenye hafla ya kuchangisha pesa za kusaidia shule ya msingi Amani iliyopo Ilala jijini Dar Es Salaam iliyoandaliwa na Tanzanian University Women's Association tawi la hapa Marekani.

Akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa mpaka sasa katika elimu ya msingi nchini, Mhe Balozi Ali amesema hatua tatu ambazo Tanzania imepitia katika elimu ya msingi tangu ipate uhuru, zimeonesha mafanikio katika masuala kama uwiano wa jinsia mashuleni, kupunguza idadi ya wanaoshindwa kumaliza shule kwa sababu zinazozuilika, kupunguza mwendo kwa watoto kufuata elimu na hata utaratibu wa kujenga shule ya msingi katika kila Kata na kuhakikisha kila mwana mwenye umri wa kwenda shule anakwenda.

Ametaja moja ya mafanikio makuu ya hatua hizo ni asilimia 100 ya watoto wenye umri wa kwenda shule wanafanya hivyo Visiwani Zanzibar huku mafanikio ya bara yakiwa kwenye asilimia 90 kulingana na sehemu unakochukua Takwimu.

Hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya The Wesin Gran iliyopo hapa Wahington DC ilijumuisha watu wa Umri, Jinsia na Nyendo mbalimbali za maisha na ilihusisha pia chakula cha jioni na mnada wa bidhaa mbalimbali toka Tanzania ambao fedha zake pamoja na zile za kiingilio zitakwenda kusaidia Shule ya Msingi Amani ambayo takwimu zaonesha ina wanafunzi 2989, madawati 287, walimu 50 na madarasa 17 ambao ni sawa na uwiano wa wanafunzi 59.78 kwa mwalimu mmoja, wanafunzi 175.82 kwa darasa na wanafunzi 10.41 kwa dawati.

TUWA inashirikiana na kuhusiana na Tanzania Women Graduates Federation (TWGF)ambayo iko chini na mwavuli wa The International Federation Of University Women (IFUW). Kwa habari zaidi bofya www.tuwausa.org

No comments: