Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Bwn Trevor Andrew Manuel
Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya kusini amekubaliana na ushauri wa Chama chake cha African National Congress (ANC) kujiuzulu kwa manufaa ya kile kilichokaririwa kuwa "manufaa ya waAfrika kusini" na kuepusha kura ya kutokuwa na imani naye.
Mbeki ambaye amekuwa akishutumiwa kushinikiza kesi ya rushwa dhidi ya Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo na M/kiti wa ANC Jacob Zuma ambayo ilitupiliwa mbali na Jaji wiki iliyopita na kusafisha njia kwa Zuma kugombea urais katika uchaguzi ujao.
Katibu mkuu wa ANC Gwede Mantashe amesema kuwa Kamati kuu ya chama ilikubaliana kumwambia Mbeki ajiuzulu kabla ya kipindi chake madarakani naye hakuonesha kushtushwa na alikubali kushiriki katika mkakati huo.
Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, Makamu wa Rais ndiye anayetegemea kuchukua nafasi yake, lakini Makamu wa Mbeki Bi Phumzile Mlambo-Ngcuka naye ameonesha nia ya kujiuzulu (http://www.sabcnews.com/politics/the_parties/0,2172,177148,00.html) jambo ambalo linaelekea kufanywa na mawaziri wengine.
Waziri wa Fedha Trevor Manuel ambaye anaheshimika sana kwa ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo, ndiye anayeangaliwa na wengi kuchukua nafasi ya mpito kama Bi Phumzile ataamua kujiuzulu.
Rais Mbeki ataendelea kukaimu madaraka mpaka mtu wa kushika nafasi yake atakapoteuliwa. Kwa habari zaidi http://news.yahoo.com/s/ap/20080920/ap_on_re_af/af_south_africa_mbeki. Hata hivyo uamuzi wa kumfanya Rais ajiuzulu umeleta hisia tofauti nchini Afrika Kusini (http://www.sabcnews.com/politics/the_parties/0,2172,177154,00.html)
No comments:
Post a Comment