Thursday, September 18, 2008

Mwanaume mzee zaidi duniani alonga.

"Natamani mingine mitano ama zaidi..."

Tomoji akipongezwa na Meya Nakoto Nagamine wa mji wa Miyakonojo aliposherehekea miaka 113 ya kuzaliwa kwake

Mwanaume anayeaminika kuwa mzee zaidi ulimwenguni Tomojii Tanabe, amesherehekea siku yake ya kutimiza miaka 113 na kusema anatamani kuishi miaka mingine kama mitano ama zaidi.
Tomoji ambaye ni mkazi wa mji wa Miyakonojo katika kisiwa cha Kyushu kusini mwa Japan, anaonekana mwenye afya njema akiendelea na maisha yake ya kawaida na kula mlo wa kawaida bila kutumia pombe wala kuvuta.
Ni miongoni mwa watu 36,000 waishio nchini Japan wakiwa na zaidi ya miaka 100 (rekodi ya nchi yenye watu wengi wenye umri mkubwa) wanaoaminika kuishi miaka mingi kutokana na lishe yao bora yenye wingi wa Samaki na Mchele.
Mtu mzee zaidi anaaminika kuwa Edna Parker mwenye miaka 115 (Apr 20 1893) anayeishi Indiana nchini Marekani
Kadirio la maisha kwa wananchi wa Japan ni miaka 86 kwa wanawake na 79 kwa wanaume, takwimu zinazoiweka nchi hiyo katika nafasi tatu bora huku Tanzania tukiwa nafasi ya 193 kwa kadirio la miaka 49.41 kwa wanaume na miaka 52.04 kwa wanaume. Hata hivyo matarjio ya kadirio la maisha kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa yanaonesha kufikia mwaka 2010, Tanzania itakuwa nafasi ya 170. Unaweza kubofya http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_countries_by_life_expectancy kwa takwimu zaidi juu ya makadirio ya maisha kwa nchi mbalimbali.

No comments: