Thursday, August 18, 2011

DWIGHT HOWARD awezesha ujenzi wa bweni Tanzania

"Do you see the smiles on their faces after you have done what you do best?
Do you see satisfaction on their faces after you have blessed them with your gift?
You don't think it's much but to them it means the world
They wake up in the morning and wish you were there, you don't have to lie to gain their trust
You have never won a Nobel prize they have never seen you on the TV
Your little contribution makes their lives a little bit better every day"
Lucky Dube
Ni jana tu nilipokuwa ninapitapita mtandaoni nilipokutana na habari kuhusu ziara ya mchezaji nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani DWIGHT HOWARD alivyotembelea Tanzania na kuwezesha kupatikana ama kujengwa kwa Bweni katika shule ya sekondari Kipok.
Dwight, ambaye kupitia tovuti ya foundation yake ya D12 amesema alikuwa katika maandalizi ya kuelekea Tanzania, Haiti, India na China ametoa msaada wa shilingi milioni 90 kusaidia ujenzi wa jengo hilo.Mbali na kutoa mchango huo, Dwight, alishiriki kwenye kujenga sehemu ya msingi wa bweni hilo na kuzindua rasmi ujenzi huo kama aonekanavyo pichani.Ukweli mwingine ni kuwa Dwight Howard ni mtu mwenye pesa, na pengine Shilingi milioni 90 si kitu kwake, lakini MATOKEO ya hicho ambacho wengine wanaweza kuona ni kidogo ndiyo ninayopenda kuyazungumzia hapa. Kuona umuhimu wa kuwekeza katika elimu kwa mabinti hawa si kitu kidogo na ni hilo linalonifanya nimpe heshima na shukrani zaidi.
Ni maisha ya mabinti wengi yatakayobadilika na kuboreshwa kwa ushirikiano wake. Ni upendo wa aina yake alioonyesha kwa kushirikiana na wapendwa wa eneo hilo kuwezesha ujenzi huu.
Hili ni jambo ambalo halistahili kupita bila kupongezwa (kama ambavyo ningependa yeyote anayeshuhudia jambo kama hili kuleta hapa tupongeze).
Ni kwa sababu hii, napenda kumuunganisha Dwight Howard katika orodha ya watu walioingia kwenye MWANANCHI MIMI. Kipengele kinachohusu wale walioenda zaidi ya kazi ama fani zao, kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida.You're a hero D.
Photo Credits: D12 FOUNDATION FACEBOOK PAGE


Do you see the smiles on their faces

After you have done what you do best
Do you see satisfaction on their faces
After you have blessed them with your gift
You don't think it's much
But to them it means the world
They wake up in the morning and wish you were there
Don't have to lie to gain their trust
You have never won a Nobel prize
They have never seen you on the TV
Your little contribution makes their lives a little bit better every day

[Chorus:]
You're a hero, you're a hero

Big it up, big it up for the fireman
Big it up, big it up for the street cleaners
Big it up for the man and the woman who take care of abandoned children
Big it up, big it up for the grandmothers
Who are left to take care of the children
Big it up, big it up Wo!


MWANANCHI MIMI ni kipengele kinachoonesha, kuthaminisha na kuendeleza juhudi mbalimbali zinazofanywa na wananchi wenzetu / sisi wananchi katika kuisaidia jamii yetu. Hapa ni mahala ambapo hata wewe msomaji unaweza kuungana nasi kuonesha unathamini kazi ya mtu fulani kwa jamii yetu. Wapo wengi saana lakini hawapati thamani ya kazi zao kama ambavyo ingestahili na pengine ni kwa kuwa hawako katika "channel" ya kuvutia vyombo vyetu vya habari. Kwa habari zaidi nani ya label hii BOFYA HAPA

1 comment:

Ebou's said...

DWIGHT HOWARD Nimtu mmoja safi sana katulia na hana makeke ya kimaisha Marekani inamuangalia sana juu ya ubora wake na wakati umefika wa kujitengezea jina na kuonekana katika watu bora katika dunia ya DO SOMETHING, kuna watu ambao wanampa muongozo wakuchangia nchi masikini katika changamoto za maisha hasa katika Elimu.

Ukisikia raha ya dunia ndio hiyo, kujipendekeza kwa watu na watu wakakupenda.