International Women's Day

International Women's Day

IMETOSHA

IMETOSHA

KUMRADHI

Kutokana na kubanwa na masomo, mabandiko hayatakuwa kila siku kama awali.
NAWAPENDAThursday, August 18, 2011

Mkutano Mkuu, Jumuiya ya waTanzania, Sept 17

TANGAZO MAALUMU

Ndugu Wanajumuiya,
Kama tulivyo wafahamisha hapo awali kuwa kazi mliyo tutuma imekamilishwa. Tuna washukuruni wote mlio leta na kutuma mapendekezo yenu kutokea mwanzo mpaka mwisho wa ukamilishaji wa Katiba mpya. Maoni yenu yote yalipokelewa na kufanyiwa kazi ndani ya Katiba, tunashukuru sana kwa mchango na muda wenu mliojitolea kwa nia ya kujenga Jumuiya yetu ya Watanzania.
Hivyo basi, imetufikisha katika hatua kubwa na ya mwisho ya kuindeleza mbele Jumuiya yetu. Nakama tunavyo jua kuwa kwasasa hivi hatuna Jumuiya ila tuna Jina la Jumuiya na kwa sasa hivi Jumuiya haina Fedha za kujiendesha/ kuendesha shughuli zake. Kutokana na hali hiyo na muda wenyewe ulivyo pita, Wanakamati ya kuunda katiba tumependekeza kama ifuatavyo
- Tutakuwa na Mkutano mkuu mmoja ambao utashughulikia maswala makuu mawili:

1. Shughuli ya kwanza itakuwa ya kupitia na kupitisha Katiba.

2. Shughuli ya pili itakuwa ya uchaguzi mkuu, tutachagua viongozi wa Jumuiya.

Hivyo basi tunaambatanisha na fomu ya uchaguzi.
Kwa wale wote watakao penda kujitolea kugombea uongozi mbalimbali, tafadhali soma vizuri maelezo ya fomu hiyo na maelezo hayo yafuatwe kama yanavyosemwa. Hii itatusaidia kurahisisha kupata uongozi bora.
Kila mgombeaji atakuwa na wiki mbili za kujaza/kushughulikia na kutuma fomu hizo. Wiki inaanzia tarehe 08/18/2011 – 09/01/2011. Na fomu hizo zitumwe na zikiwa na anuani zilikotoka na juu ya bahasha ziseme
JUMUIYA YA WATANZANIA
4023 APPLE JACK CT
PASADENA, MD 21122
Mwisho, Mkutano Mkuu utafanyika tarehe 09/17/2011 saa 4 asubuhi ( 10:00am). Anuani ya ukumbi wa mkutano mtafahamishwa hapo baadaye.

No comments: