Friday, August 19, 2011

Msechu ahimiza umuhimu wa kujua lugha ya kiingereza


MMOJA kati ya washindi wa shindano la Tusker la Tusker All Stars 2011 Mtanzania Peter Msechu amewaasa wanafunzi nchini kutilia mkazo wa lugha ya Kiingereza kwani inasaidia katika kupata mafanikio.
Msechu amesema hayo leo jumatano wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Nia Njema iliyopo mjini Bagamoyo ambayo aliwahi kusoma kidato cha kwanza hadi cha nne.
Alisema kufahamu lugha hiyo ni kitu muhimu kwani kumemsaidia kwa kiasi kikubwa kutwaa taji hilo ambalo litamuwezesha kufanya kazi na wasanii mbalimbali wakubwa duniani.
“Napenda niwaambie lugha ya kiingereza ni mkuhimu katika kusaka mafanikio ya kitu…mimi nilipokuwa nasoma hapa niliona kama mwalimu wangu ananionea baada ya kuniadhibu kutokana na kutoifahamu vema, lakini sasa nimeona hawakuwa wakikosea,”Alisema.
Aliongeza kuwa, tangu alipoanza mchakato wa kushiriki shindano hilo kwa mara ya kwanza alikutana na changamoto ya lugha hali iliyomfanya aombe msaada wa kufunzwa zaidi na walimu wake hali iliyomsaidia kuchanja mbuga.
“Asikwambie mtu kiingereza ndiyo kila kitu kwani bila hivyo ningeona aibu kujifunza na kuishia njiani…nawasihi wadogo zangu kuitilia mkazo lugha hii,”Aliongeza.
Aidha, Msechu aliwashuku walimu wa shule hiyo kwani ndiyo chachu ya mafanikio yake kutokana na shule hiyo kutilia mkazo lugha hiyo kama lugha kuu ya mawasiliano shuleni hapo.
Naye mkuu wa shule hiyo, Anthony Nyenshile alimpongeza msanii huyo kwa kukiendeleza kipaji chake sambamba na kujibidiisha hali ambayo imemfikisha hapo alipo.
“Kwa kweli kijana huyu alikuwa mchapakazi na anayependa sana sanaa…tunakupongeza kwa hatua uliyofikia hivyo tunakutakia kila lka heri katika harakati zako za kimuziki,”Alisema.
Msechu, pamoja na wenzake wawili Alfa wa Burundi na Davis wa Uganda walitwaa ushindi wa shindano hilo lililofikia tamati mwishoni mwa wiki iliyopita huko Nairobi, Kenya.
Kwa ushindi huo wasanii hao watapata fursa ya kupanda jukwaani na wasanii mbalimbali wakubwa toka nchini Marekani ambao wanatarajiwa kwenda nchini Kenya.
Msechu akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Nia Njema akiwahamasisha umuhimu wa kuifahamu lugha ya kiingereza.
Msechu akiwa ofisini kwa mazungumzo na mkuu wa sekondari ya Nia Njema, Anthony Nyenshile.
Msechu akiwa na baadhi ya marafiki zake aliosoma nao shuleni hapo ambao walimsindikiza katika ziara hiyo.
Msechu akiwa na baadhi ya walimu wa NIA Njema High School

Shukrani kwa Dina Ismail wa Mamapipiro Blog

1 comment:

emu-three said...

Wow,msechu msechu...ooh, nimemkumbuka, ok, safi sana tupo pamoja!