Kutokana na CHANGAMOTO zilizo nje ya uwezo wangu, nimeshindwa kuweka kipengele cha Them, I & Them kwa siku ya leo. Ila, nina CHANGAMOTO YETU SOTE KUHUSU ULEZI NA MALEZI

Kuna wakati maisha yetu hayaendi kama tupendavyo. Yaani uwezo wa kutimiza ndoto zetu unazidiwa na ukweli wa ugumu wa maisha. Na kwa kuwa hatutimizi malengo yetu, haimaanishi kuwa hatuwezi kuishi maisha mema. Tunaweza kwa KUTAMBUA wapi palipo na uwezekano wa kusaidiwa kutimiza ndoto ama malengo yetu kwan ufasaha na mafanikio zaidi ya tunavyoweza. Ni hapa ambapo tunatakiwa kuwa wasaidizi wa wenzetu. Wa ndugu na jamaa zetu na kuwaonesha njia sahihi ili wafanikiwapo wawe na uwezo wa kutusaidia sisi na jamii kwa ujumla.
Juzi nilikuwa nasoma ukurasa wa rafiki yangu kwenye facebook. Nikakutana na picha njeeema saana ya Mamaye kisha nikaeleza ukweli kuhusu jukumu la kinamama. Aliponijibu nikajikuta nakaribia kutiririsha chozi. Alinieleza kuhusu UPENDO, UJASIRI NA IMANI aliyonayo mama yake. Sikushangaa sana kwani na yeye yuko hivyo. Kisha nikarejea kwa wazazi wengi niwajuao (namtanguliza Mamangu mpenzi) na kugundua kuwa wengi wanafanya mengi ambayo sasa hivi yanaigusa jamii kubwa kuliko ambavyo ingekuwa kama wangeamua kujilimbikizia wao. Najaribu kufikiri kama Mama zetu wangepata muda wa kuelimishana kwa namna tufanyavyo (hata kama wangekuwa na ma-pc kila chumba cha nyumba na muda wa kufanya hivyo). Lakini hii ni sehemu ndoooogo saaaana ya faida ambayo Mama zetu (na wazazi + walezi kwa ujumla) wameiwekeza kwetu na sasa ulimwengu mzima unanufaika.
Niliwahi kuandika kuwa HUWEZI KUWASHUKURU WOTE WALIOKUSAIDIA, BALI WAOMBEE. Waombee kwa moyo wa kuwekeza katika kile unachokitumia sasa kutuelimisha na kutupa changamoto za maisha.
Na hii sasa ni CHANGAMOTO YETU SOTE kubadili mawazo ya u-mimi na kuwekeza katika kile tuwezacho, lakini pia kile tunachoweza kuwawezesha wenzetu na tufanye hivyo.
Narejesha habari hii toka kwake Dr Ben Carson aliyoizungumza katika kipindi cha Morning Edition cha NPR ambapo kila Jumatatu huwa wanaleta watu tofauti kueleza wanachoamini. Yeye alisema anaamini kuwa THERE IS NO JOB MORE IMPORTANT THAN PARENTING. (Bofya hapa kusoma na kusikiliza wengine wasemavyo)
Labda tujiulize kuwa ni matendo mangapi yanayoimong'onya jamii kwa kuwa watu hawakulelewa vema?? Hawakuoneshwa njia sahihi ya kupia, hawakufunzwa kujitambua na kutambua na kuheshimu tofauti na mafanano yetu, hawakuelezwa kuwa sisi ni zaidi ya muonekano, ni zaidi ya pesa, ni zaidi ya mali, ni zaidi ya sifa za mtaani na hata zaidi ya vile ambavyo wasiotujua wanatufanya tujione????
Ni mangapi yanayotokea sasa na kuonekana dhahiri kuwa ni matokeo ya ULEZI M'BOVU???
Naungana na Dr Carson kuwa HAKUNA KAZI ILIYO MUHIMU ZAIDI YA KULEA NA NAWASHUKURU WAZAZI NA WALEZI WANGU WOOOTE WALIONILEA NA WANAOENDELEA KUNILEA (kwa namna moja ama nyingine)
Bonyeza "play" umsikilize na / msome Dr Carson hapa chini
N.P.R (National Public Radio)
3 comments:
KAKA ULIJUAJE UKWELI MTUPU ULIOTUELEZA.
NDUGU YANGU NIMEREJEA TENA.
Nashukuru kaka, somo zuri sana.
Niongeze kidogo hapa.
Hatuwezi kurudisha fadhila kwa wazazi/walezi,tuwatumikie wangali bado duniani,kwani itakuwa painful sana pale ambapo utataka kuanza kuwatumikia lakini kwa bahati mbaya wakawa hawapo tena.
Kaka Kissima! ni kweli ila kwa wale ambao walezi wao bado wazima wachukue nafasi. Nafasi ndio hii na ni sasa. Asante kwa somo zuri Mzee wa Changamoto kama kawa yako kila wakati ni changamoto tu. Safi sana kuchangamsha watu.
Post a Comment