Saturday, October 10, 2009

Nimeipenda hii... Kisha nikajiuliza ni lini ntaona waTz Pamoja?

Sipendi kuiona "waTanzania Pamoja" kwa kuwa waKenya wametoa, bali kwa kuwa ni kitu cha maana na manufaa kufanya. Si kwa manufaa ya wanamuziki tu (ambao wanapata mengi si kwa kufanya kazi ya pamoja bali kwa kuonesha ushirikiano) lakini kwa jamii nzima ambayo itathamini zaidi UMOJA NA USHIRIKIANO WA WASANII. Nimependa zaidi intro ya mtoto aliposema "People should LOVE EACH OTHER because we were created in GOD's OWN IMAGE and we should RESPECT EACH OTHER all times.....EVERYONE IS IMPORTANT. TUPENDANE ILI TUISHI"

Lakini pia niwasikilizishe hii ya Waganda kuhusu Africa na kisha tuone kama hii yaweza kuwa CHANGAMOTO kwa waTanzania kufanya hili

TUPENDANE

JUMAMOSI NJEMA

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

TUPENDANE, NI KWELI SISI SOTE NI WANANDUGU. JUMAMOSI NJEMA NAWE PIA NA FAMILIA YAKO UIPENDAYO. UPENDO DAIMA.

Albert Kissima said...

Sisi sote watoto wa baba mmoja(MUNGU), Wengine wanamwita Molaaa, Wengine wanamwita Alah, wengine wanamwita Jehova, wengine wanamwita Jah, ni yuleyule tu,destination yetu ni moja,so kila mtu kwa utaratibu uleule na kwa maana ileile ajitahidi ili cku moja tukutane pamoja na tushangilie kwa pamoja.Hili litawezekana kama binadamu hatutabaguana,litawezekana kama tutaishi kwa amani na upendo.


Jmosi njema kaka pamoja na wanablog wote.

chib said...

Kwa kila lililo jema si dhambi kuliiga