Sunday, October 11, 2009

Rogers Mtagwa...

Aonesha uhodari, nusura amuumbue Lopez...agomewa pambano la marudiano Lopez (shoto) akipambana na Mtagwa (kulia) Picha na Chris Farina/Top Rank
"Mtagwa hurt Lopez with a series of shots late in the 10th round and never stopped swinging.
He sent Lopez staggering into the ropes at the end of the 11th round. Lopez only avoided a knockdown because he grabbed the ropes to keep himself upright and Cotton didn't see it as the bell rang.
Then the real drama started when the bell rang to start the 12th round.
Lopez came out of his corner on unsteady legs and you just knew it would be a race against the clock.
Could Lopez last three minutes?
He did, but just barely.
Mtagwa was all over him. Lopez was desperate to survive. He had no defense and could barely hold on and throw the occasional punch to stay in the fight as the crowd was standing and going wild."

Huu ni uchambuzi wa mkongwe wa uandishi wa ndondi katika mtandao wa ESPN Dan Rafael alipokuwa akieleza mpambano kati ya Rogers Mtagwa vs Jual Manuel Lopez. Katika pambano hilo Manuel alitetea ubingwa wake kwa kuonesha ujasiri wa kumaliza pambano aliloonekana kuumizwa katika raundi 3 za mwisho. Rogers ambaye alikuwa akipewa nafasi ndogo ya kushinda amekuwa bondia wa kwanza kumfikisha Lopez raundi ya 11 na ilionekana wazi kuwa alimzidi nguvu katika raundi ya 10-12. Hata hivyo, licha ya kuonesha uwezo mkubwa wa kumpiga na kunyakua mkanda huo, Promota Bob Arum amekataa ombi la Mtagwa la pambano la marudiano na kusisitiza kuwa anasonga mbele na maandalizi ya pambano la Jan 23 dhidi mmoja kati ya Celestino Caballero (ambaye anaonekana kutaka pesa zaidi ya zile ambazo promota Arum anapanga kumlipa) ama mabingwa wengine katika uzito wa featherweight Steven Luevano au Elio Rojas. Uamuzi huu wa kibiashara zaidi umeonekana kuleta mnong'ono kidogo kwa mashabiki wanaotoa maoni wakisema hata kama Mtagwa hatapata re-match, Lopez si bondia bora kama asemwavyo kwani hajapambana na nyota halisi wa mchezo huo na usiku wa jana ulikuwa dhihirisho.
MTAZAMO WA CHANGAMOTO YETU::Si jambo la kushangaza saana kwa promota kufanya hivyo kwani anaonekana kufuatilia maslahi zaidi na amegundua kuwa Lopez anauza zaidi ya Mtagwa (kutokana na upinzani wa jadi uliopo baina ya washabiki wa ndondi wa Puerto Rico na Mexico) na licha ya sifa zinazozidi ubora wa Lopez, bado wanajua kuwa mashabiki wa Puerto Rico na Mexico wanaingiza pato kubwa hivyo kumuweka Lopez katika nafasi ya kunyang'anywa mkanda na Mtagwa ni kupoteza pesa nyingi anategemea kama atampambanisha Lopez na bondia mwingine wa Marekani ya kusini katika pambano la kugombea mkanda. Na hili ndilo linaloonekana kuharibu ulimwengu wa ndondi kwa sasa ambapo ubora wa mabondia sio unaotawala mapambano, bali matakwa ya mabondia na mapromota. Tunaona sasa Heavyweight ilivyolala kwa kuwa hakutakuwa na pambano la kuunganisha mikanda (UNIFICATION BOUT) ambalo miaka ya nyuma lilitumika kumsaka bingwa bora zaidi wa uzito huzika, kwani wenye kuishikiliza mikanda ya uzito wa juu (ndugu Vitali na Vladimir Klitscho) walishaapa kutopigana baina yao. Tuliona namna ambavyo Mayweather aliwakimbia Cotto, Margaritto na hata Paul Williams licha ya kuwa ndio waliokuwa katika ubora na orodha ya kupambana naye. Na sasa tumeona namna ambavyo Mtagwa ameonesha kuwa bondia pekee aliye tishio kwa Lopez lakini promota Bob Arum anazuia uwezekano wa bondia wake kupoteza mkanda.
KAZI NZURI MTAGWA NA TWATUMAI MENGI MAZURI YAKO MBELE YAKO PUNDE.

3 comments:

John Mwaipopo said...

nadhani mwanakwetu kafanya vema. vema sana tu. nimeelewa kuwa mtagwa alikuwa anapambana na 'mshindi'. ndo ndo ndo si chururu siku moja atakuja kututoa kimasomaso. alikuwa anapambana ulingoni wakati mchezo umeisha kabla hata ya kuanza kwa pambano lenyewe. fitina tu.

viva afrika said...

hatutachoka kusema umetuwakilisha vema mtagwa bado tuko nyuma yako, hatutakuacha kamwe.

Yasinta Ngonyani said...

Tupo pamoja na tutafika tu!!!