Monday, October 12, 2009

Happy Birthdate Brother Chib & Sister Subi

Da Subi wa Nukta77
Kaka Chib wa Hadubini
Labda niunganishe hapa kuwa kuna mengi ya pamoja miongoni mwenu. Sio tu ninyi ni BINADAMU, bali pia mna asili ya TANZANIA na kila mmoja wenu kwa mahitaji ya maisha anasaka maisha bora nje ya nchi. Nyote mna UCHUNGU NA NCHI yetu na kila mmoja wenu anajitahidi kutumia kila chema aonacho aliko KUIELIMISHA JAMII YETU. Nyote mwajikita kutujuvya hili na lile na hasa CHAMBUZI ZA KIAFYA na NYOTE MMEZALIWA TAREHE 12 OKTOBA (puuzia miaka na masaa japo najua vyote. Lol)
Labda hizo ni character ambazo kila mmoja anazijua na hamna namna ya kuzificha wala kuzieleza (japo sijui kwanini nimezisema) maana hizo ni kwa wote. WACHA NIWE SELFISH SASA NIANIKE MANUFAA YENU KWANGU
Napenda kusema kuwa ninyi (kama ilivyo kwa bloga wengi hasa wa habari na chambuzi) NAWAPENDA SAANA. Napenda ushirikiano wenu, napenda moyo wenu wa kupata nafasi ya kuandika hili na lile na pia kutufunza kupitia maoni. Nyote mnafurahisha mnapoamua kutupa taswira na habari za kuondoa msongo wa mawazo na hilo nalifurahia kwani bado MNAHESHIMU WASOMAJI NA WASHIRIKI WENZENU.
Kaka Chib nimejifunza mengi toka tumeanza kuwasiliana. Nashukuru kwa namna ambavyo unajibu unapoweza na kuonesha kuelekea zaidi ya unapoweza unapodhani ni kwa manufaa yetu.
Dada Subi ninakuandika mwisho kwani hata msomaji akichokea hapa atakumbuka mengi niliyosema kwako. Wewe ndio fundi mitambo wa Changamoto Yetu na nimekusakizia kwa wengi walioniuliza kuhusu mengi nisiyoyajua kuhusu blog. Well, kwenye facebook na emails umeendelea kunifunza hili na lile.
Najivunia kuwa nanyi, na najivunia uwepo wa kila mmoja hapa. Na pengine wapo wanaorejea kusoma kabaraza kangu kwa kuwa wasomaji wa hapa (ambao ni ninyi "watoto" na bloga wenzangu watoao maoni) mnajikita kwenye uelimishaji na utafutaji wa suluhisho mbalimbali
NAWAPENDA KWA KUWA NAPENDA KUPENDA PENDO LINALOPENDEKA NA NAPENDA KUSEMA KUWA NAPENDA KUPENDEKA MNAKUPENDWEKA NAMI
Leo sijaweza kusema kila ninaloweza kusema lakiji haimaanishi kuwa sina la kusema. Natamani ningeweza kusema yote niliyonayo leo, lakini kwa wale wajuao, basi wanajua kuwa niko kwenye "mchakamchaka" mkuu. Lakini kwenu ninyi na kwa wasomaji wote wa kibaraza hiki, NAWAPENDA NA NAWAOMBEA
Huu wimbo ni maalum kwenu
HAPPY BIRTHDATE Brother CHIB & Sister SUBIRA

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongereni sana kwa siku hii muhimu .

Subi Nukta said...

Shukrani kwa salam za sikukuu ya kuzaliwa na kwa kutupatia nafasi katika blogu yako! Asante sana!

chib said...

Na heshima iliyoje kuweza kutukumbuka kwa namna ya pekee. Huwezi jua umeongeza kiasi gani pumzi yangu hapa duniani kwa ujumbe huu katika blogu yako. Na binafsi nimepokea ujumbe mwingi wa pongezi kutokana na heri na baraka ulizotoa hapa kwenye blogu yako.
Natoa shukrani zangu nyingi tena na tena.
Naendelea kuona manufaa ya kublogu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hongera kuktoka huku migombani pia