Sunday, September 29, 2013

Mhe. Mwigulu Nchemba aunguruma DMV

Habari na picha kwa hisani ya VIJIMAMBO BLOG
Mhe. Mwigulu Nchemba akijianda kuingia kwenye ukumbi wa Mirage  uliopo Hyattsville akiambatana na Msaidizi wa Rais Mhe. Rajab Luhwavi huku wakisindikizwa na wenyeji wao Mwenyekiti wa CCM DMV Bwn. George Sebo( kushoto), Katibu wa CCM New York Bwn. Shabani Mseba(kulia). Katikati mwenye shati la kijani ni Mwenyekiti wa zamani wa CCM DMV Bi Loveness Mamuya.
Mhe. Mwigulu Nchemba akiongea na Watanzania DMV kwenye ukumbi wa Mirage uliopo Hyattsville, Maryland pamoja na mambo aliyoongea ni kuwaomba Watanzania ughaibuni kupima wanayoongea wapinzani huku akisikitishwa na kauli za upinzani wanaodai barabara si maendeleo huku akitoa mfano wa barabara za Marekani ni kielelezo cha maendeleo ukilinganisha na barabara Tanzania.
 Juu na chini ni viongozi wa dini wakiomba dua kabla ya mkutano
 Kikundi cha kwaya cha CCM DMV kikitumbuiza kwa nyimbo

 
Watanzania na wafuasi wa CCM wakifuatilia mkutano
Juu na chini ni Watanzania wakisimama wakati Mhe. Mwigulu nchemba akifuatana na msaidizi wa Rais walipokua wakiingia ukumbini.

 Viongozi wa dini na Jumuiya ya Tanzania DMV katika picha ya pamoja
 Viongozi wa CCM Chicago.
Viongozi wa CCM kutoka majimbo mengine wakihudhuria mkutano wa CCM DMV. kutoka kushoto ni Nassoro Basalama, Godffrey Lepana( NC) Judith Mhuto( IL) Shabani Mseba(NY) na Rechel Wasira(IL)
Kushoto ni ni Rose Kungwi katibu mwenezi CCM Chicago, IL
 Mhe Mwigulu Nchemba akisalimiana na wanachama wa CCM DMV na Watanzania waliohudhuria mkutano wa CCM DMV.
Msaidizi wa Rais Kikwete, Mhe. Rajab Luhwani akisalimiana na Watanzania DMV wakati alipokua kaiingia mkutano wa CCM DMV.

No comments: