"Better to write for yourself and have no public, than to write for the public and have no self."
Cyril Connolly (1903 - 1974)
Tuesday, April 7, 2009
When will i be home again???
"Sometimes I wonder when will I be home again?" Haya ni maneno ya Luciano ambaye katika wimbo wake aliouita hivyohivyo (when will I be home) ameimba mengi kuanzia walivyopoteza asili ya kwao kwa wazazi wao kupelekwa utumwani, kisha anazungumzia asakavyo asili yake na anajiuliza kama asili yake yaweza kuwa TANZANIA na kisha akazungumzia vitu vya kujivunia avionavyo na kuvipenda barani Afrika kama kuchomoza kwa jua kulivyona machweo yake, michezo ya watoto mitaani, kuoga mtoni (kwa wale walio karibu na mito) mpaka utayari wake wa kufika huko AFRIKA na kuendeleza kuimba kuwa "sometime i wonder when will i be home again?"Maswali ni mengi na wengi wanaweza kujiuliza mengi, lakini nami nitoe changamoto hapa kuwa ni kipi ukumbukacho zaidi unapofikiria safari ya nyumbani? Hapa namaanisha kule iliko asili yetu. Na leo nilipokuwa naendeleza kazi nilikuwa nasikiliza huo wimbo mara kadhaa. Ni kwa kuwa nilikumbuka sana nyumbani, kisha nikarejea kwenye kompyuta yangu na kuanza kujikumbusha taswira za nyumbani. Nakubali kuwa tumebarikiwa. Mbali na ndugu na jamaa, UHALISIA NA USAILIA WA NYUMBANI ni kitu kingine ninachokikumbuka saaaana. Naishia kujiuliza tena WHEN WILL I BE HOME AGAIN?????
HAPA KWENYE MLO NDIO KABISAAAA. Sijui lini tena???
Msikilize Luciano katika wimbo huu When will i be home
nakuona sijui uko viunga vya kashura sijui wapi hapa. kwa hakika umenikubusha sana home lakini niko njiani kueleke bukoba next wee.
nikumbukapo home huwa nakumbukamarafiki zangu wa shule za msingi, disco toto, nk. nakumbuka wazee wa vijijini na busara zao za ukubwani, nakumbuka ukwasi wa baadhi yao, kuoga mtoni na kulewa na washikaji.
nakumbuka msosi wa mviringo kama huo. mkubwa kiasi kwamba huwezi amani kuwa mtaumaliza lakini unaisha tu labda hamjaukalia.
bahati mbaya wiki ijayo narudi home nikiwa siwazi kula tena ndnizi nyama wala samaki, nikiwa siwezi kunywa tena kakonyagi wala lubisi. njiuliza itakuwaje nymbani na watu wa kwetu watanipokeaje na uamzi wangu mpya.
Nakumbuka vizuri sana mara yangu ya kwanza kukalia hizo nyasi. Nilikuwa form two pale Kahororo Sec. Wikiendi tulikuwa tunakwenda kule ziwani na kuna mawe kama hayo. Asante kwa kuniletea kumbukumbu za ujanani. Nyumbani daima ni nyumbani ati!
Kaka huo msosi umenikumbusha mbaaaaali kweli yaani ni chijijini kabisa kasoro hapo ni iyo sinia tu, si kule msosi wamiminwa moja kwa moja kwenye mbabi hizo au majini ya migomga na ako kanyasi ndo usiseme tena. ahhha we acha tu.
Kaka Kamala umesharudi? chakula kimenikumbusha mbali kweli, nilipokua Ishozi Kijiji cha Katano.....Tweyambe Sec. Niliandaliwa chakula cha namna hii nilipokaribishwa na jamaa zangu Asante kwa picha, Nimepakumbuka jamani!
.Today we have bigger houses and smaller families; more convenience but less time. .We have more Degrees but less common sense; more knowledge but less judgment. .We have more experts but more problems; more medicine but less wellness. .We spend too recklessly, laugh too little, drive too fast, get too angry too quickly, stay up too late, read too little, watch Tv too much and Pray too seldom. .We multiply our Possessions but reduce our values; we talk too much, love too little and lie too often. .We’ve learned how to make living, but not a life; we’ve added years to life not life to years. .We have taller buildings, but shorter tempers; wider freeways but narrower viewpoint. .We spend more, but have less; we buy more, enjoy less. .We’ve been all the way to the moon and back, but have trouble crossing the street to meet our neighbor. .We’ve conquer outer space, but not inner space. .We split the atoms, but not our prejudice .We write more, learn less; plan more but accomplish less; we’ve learned to rush but not to wait; we have higher income but lower morals. .We build more computers to hold more info, to produce more copies but have less communications. .We’re long on quantity but short on Quality. .These are the time for Fast food and slow digestion; tall men and short characters. .More leisure but less fun; more kinds of food but less nutrition; two income but many divorces, fancier houses but broken homes.
11 comments:
Wow! hapo umeniacha hoi kabisa. ni kumbukumbu nzuri sana na huo msosi mmh nimetam,ani kwelikweli mpaka mate yamevuja
Moyoni unatamani,
Kuwepo kwenu nyumbani,
Pengine hujui lini,
Wajiuliza!
Ndugu zako wa nyumbani,
Bado wanakutamani,
Wakwone japo machoni,
Wajiuliza!
Hujasahau nyumbani,
Uliko ughaibuni,
Basi utarudi lini?
Twajiuliza!
Da Yasinta unatamani msosi wa home? Si juzi juzi ulikula hadi ukachoka ukakwea pipa huyoooo ukasepa.!
Kaka mkubwa mambo vp?
nakuona sijui uko viunga vya kashura sijui wapi hapa. kwa hakika umenikubusha sana home lakini niko njiani kueleke bukoba next wee.
nikumbukapo home huwa nakumbukamarafiki zangu wa shule za msingi, disco toto, nk. nakumbuka wazee wa vijijini na busara zao za ukubwani, nakumbuka ukwasi wa baadhi yao, kuoga mtoni na kulewa na washikaji.
nakumbuka msosi wa mviringo kama huo. mkubwa kiasi kwamba huwezi amani kuwa mtaumaliza lakini unaisha tu labda hamjaukalia.
bahati mbaya wiki ijayo narudi home nikiwa siwazi kula tena ndnizi nyama wala samaki, nikiwa siwezi kunywa tena kakonyagi wala lubisi. njiuliza itakuwaje nymbani na watu wa kwetu watanipokeaje na uamzi wangu mpya.
ikibidi nitasingizia ugonjwa daktari kaknikataza
napenda home
Tukumbuke kuwa nyumbani kwa wengine nyumbani kwao ni china.
Na maswala ya nyumbani ni bora yana undugu na sisi ni bora kuliko wao!
Kumbuka nyumbani BOMBA ingawa kwa wengine nyumbani ni majukumu kuliko furaha!:-(
Na majukumu yanafurahisha kama unaweza.
Nakumbuka vizuri sana mara yangu ya kwanza kukalia hizo nyasi. Nilikuwa form two pale Kahororo Sec. Wikiendi tulikuwa tunakwenda kule ziwani na kuna mawe kama hayo. Asante kwa kuniletea kumbukumbu za ujanani. Nyumbani daima ni nyumbani ati!
Ama kweli nyumbani ni nyumbani...
Wow!Ebitoke!asante sana kwa kunikumbusha nyumbani.

Post a Comment