Wednesday, July 1, 2009

Tunataka kuwaamini polisi, lakini HAWAAMINIKI.

Kuna matukio mengi yanayotendwa na askari polisi nchini ambayo yanasikitisha saana. Hatujui ulipo mstari kati ya usalama wa raia na siasa. Kumekuwa na mambo mengi ambayo yanapunguza heshima na imani ya wananchi kwa jeshi hili. Kibaya zaidi ni kuwa Polisi HAWAAMINIKI katika yale watendayo. Si tunakumbuka yaliyotokea wakati wa mauaji yaliyoanzisha kesi ya kina Mhe Zombe? Tuliambiwa nini na tukaja kugundua nini? Unadhani watu wanafikiriaje kuhusu jeshi lao? TUMESHUHUDIA wasio na hatia wakihukumiwa, wakiuawa na hata kusingiziwa mambo mbalimbali. Unafika wakati WANANCHI WANAKOSA IMANI, UPENDO NA HESHIMA kwa jeshi hili na kuamua kujichukulia hatua mkononi. Hili si jambo jema hata kidogo lakini badala ya kujitahidi kuwatisha na kuwafunga wasio na hatia, JESHI LA POLISI LIBADILI, LIBORESHE NA KUHESHIMU UTENDAJI WAKE WA KAZI NA KUTENDA HAKI KWA WANANCHI
Mfano mzuri ni namna walivyoshughulikia tatizo hili la Wana-CCM kufanya mkutano kanisani na kumpiga kiongozi wa kanisa (bofya kusoma) ama kule Tunduma ambapo Polisi wamekamata zaidi ya watu 88 (Bofya hapa) ambao walianzisha vurugu kupinga kuuawa kwa mwananchi akitoka kutazama mpira. Kosa la wananchi ni kujichukulia sheria mkononi, lakini lazima pia kuangalia CHANZO CHA TATIZO. Tumeshashuhudia matukio kama haya ya kionevu kama ambavyo Changamoto Yetu ilivyoandika tarehe 1 Novemba mwaka jana (Bofya hapa kuisoma)
Ni lazima kuvunja uharibifu unaowafanya wasio na hatia kubambikizwa kesi na kisha twende kuwaweka huru. Wapo wengi ambao hawana makosa lakini wako jela wanateswa na RUSHWA iliyoshamiri katika jeshi la polisi.
Ndio maana Luciano akawaambia wenye tabia na mtazamo kama wenu kuwa BREAK DOWN THOSE BRICK WALLS, AND SET THE INNOCENT FREE

1 comment:

  1. Sijui lini yatakwisha mambo kama haya Bongo si polisi, jeshi, wala waziri wote nyia moja katika rushwa.

    ReplyDelete