Monday, July 13, 2009

Za Kale Vs Maisha ya sasa...... WAKATI NILIKUWA MDOGO

Mzee wa Changamoto "wakati huo nikiwa mdogo"
Wapo wanaoamini kuwa MAJUTO NI MJUKUU. Wakimaanisha kuwa kuna kujuta katika kuishi ambako mara nyingi hukufanya ujutie nafasi ambazo umepoteza wakati wa kuelekea hapo ulipo. Kuna ukweli wa kukumbuka tulipoanguka ili kuweza kuepuka kuanguka tena. Lakini naamini ukishajifunza huna haja ya kujuta.
Lakini KUKUMBUKA ni muhimu saana. Na kumbukumbu ni moja ya mambo ambayo kwa pamoja tyunashirikishana na wakati mwingine kutuonesha mabadiliko ya hapa na pale, kulinganisha umakini wa harakati zetu kimaisha na hata mabadiliko yanayoonekana na yasiyoepukika.
Mfano ni kukumbuka maisha yalivyokuwa wakati wa utoto na sasa. Kuna mambo ambayo hatuwezi kuyaepuka kuyakumbuka (na mengine huwa ni burudani). Hebu kumbuka tu-picha twa utotoni, ama "marafiki" wa utoto, michezo na mengine mengi. Unadhani maisha yako yalivyokjuwa enzi unacheza chndimu? Enzi za mipira ya kufuma toka makaratasi ya nylon? Enzi za kutengeneza ma-toy yetu wenyewe? Mmhhhhhhh! Nakumbuka enzi hizo.
Leo hii tuungane na wana Marquiz du Zaire wakitukumbusha enzi, katika kibao chao WAKATI NILIKUWA MDOGO.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa**

2 comments:

  1. kuna wakati ulijinyea na kujikojolea harafu eti unamwonesha mama! sasa hizi unaweza hata kumuaga kuwa unaingia chooni kufyatu jitu linukalo au unasema nakuja mama samahani kidogo!!!!!

    ReplyDelete
  2. Asante kwa kumbukumbu za utotoni. Nakumbuka jinsi tulivyokuwa tunabeba vigunzi vya mahindi kuwa ndio watoto. Kutengeneza watoto na udongo wa mfinyazi. Mmmh we acha tu: Katoto ako kamependeza ...lol

    ReplyDelete