Wednesday, September 23, 2009

Bado natamani kuwa mwalimu. Ila shule iwe UN na wanafunzi ma-Raisi

Leo kikao cha 64 cha umoja wa mataifa kinaendelea katika kile wanachoita "The general debate". Kikao hiki kilianza rasmi Jumanne ya Sep 15. Bado nawaza mengi kuhusu UMOJA WA MATAIFA. Hivi umeweza kutenda yale yaliyokuwa madhumuni ya kuanzishwa kwake? Imezuia VITA KUU YA TATU YA DUNIA ama imezuia vita moja tuu ya tatu ya dunia? Maana naona nyingi ambazo kwa wingi wake ni kama tayari Vita ya dunia.
Najiuliza hivi ni kweli kuwa yanayojadiliwa humu huwa yanatekelezwa? Na kama hayatekelezwi ni nani wa kulaumiwa????
Na ndio maana narejea niliyoandika Nov 18, 2008 kuwa "Natamani kuwa mwalimu. Shule iwe UN na wanafunzi ma-Raisi"

Ingenichukua muda kusahihisha Homeworks, lakini wote wangefanya VEMA dunia ingekuwa sehemu bora ya kuishi kuliko ilivyo sasa.


Napenda old style ya ualimu ambapo walimu walikuwa wanajua uwezo wa takribani kila mwanafunzi. Walikuwa wanahakikisha kuwa kila mtu anafanya "homework" yake na walikuwa wanasahihisha siku inayofuata. Walimu walikuwa na uwezo wa kutambua kama umefanya mwenyewe homework yako ama umefanyiwa. Halafu kingine nilichokuwa napenda ni ile style ya kubandika matokeo darasani. Yaani kujua nani kawa wa kwanza na nani wa mwisho. Hapo ilikuwa ni lazima usome sana maana ni kuangalia nani ana VEMA nyingi na nani anaongoza darasa. Lakini kwa mtazamo wangu ilikuwa na faida maana yaliyotendeka ilikuwa ni CHANGAMOTO KWETU kuongeza juhudi katika masomo.
Style hii ningeipata nikaweza kuitumia UN naamini ingesaidia saana. Yaani kuhakikisha kila maraisi wanapoondoka wanapewa "homework" ya kufanya nchini mwao na wakirejea kwa "darasa" (kikao) kijacho kwanza tunaangalia nani kafanya nini na kafanikiwa mangapi kisha tunasonga mbele. Yaani kujua nani anajua na kutatua matatizo ya nchini mwake na kuwasaidia wananchi wake na pia tungejua nani hana ajualo kuhusu shida na mahitaji ya wale awaongozao. Ingetuwezesha kujua nani yuko mstari wa mbele kubadilishana mawazo (pale nitakapowapa group discussion ya kukokotoa maswali) na kutumia "ideas" za wenzake kufanya homework zake kuwasaidia wananchi wake. NINA UHAKIKA kwa mfumo huu lazima ULIMWENGU ungekuwa hatua kadhaa mbele kuelekea kwenye mafanikio ya kutatua shida za wenye uhitaji.
Kwani wanapokutana huwa hawapewi majukumu ya kutekeleza? Ama wakipewa wanaweza kuyatekeleza bila kuwaeleza wananchi? Lakini kama ni majukumu kwa wananchi si tungeona mabadiliko huko tuliko? Namaanisha hata kama hatuambiwi si tungejua kuwa "ujenzi wa hizi zahanati ni manufaa ya raisi kwenda kwenye mkutano wa mwaka huu?"
Najiuliza kama kuna mwananchi anayeweza kujibu akiulizwa amenufaika nini kwa raisi wake kwenda kwenye vikao vingi vya Umoja wa Mataifa?
Sisemi hatujanufaika, ila kama manufaa hatuyaoni bayana na hatuambiwi pia, sijui tufikirieje matumizi ya kodi zetu!

Anyway, japo kuna ukweli ndani yake, lakini nafikiri hii ni njozi. Never Mind!!!

6 comments:

  1. huwa sielei sana hizi politics bwana. ni ulimwengu tuuishio mbele ya wanaumoja wa mataifa. unamiliki siraha na kujaribu kuleta amani wakati wenyewe ungekuwa na amani usingekuwa na siraha. sasa utaletaje amani wakati umeshikilia siraha?

    ReplyDelete
  2. i was looking for people like you i got you. call me 240 264 7902

    ReplyDelete
  3. Masikini ya Mungu,
    yanayojiri huko UN tutayapata kwenye magazeti, radio,blogs na kwenye telivisheni.Sina hakika kama mwakilishi wetu atatoa tathmini na manufaa ya kikao hicho kwetu sisi wadau aliotuwakilisha.

    Tutasikia tena kupitia vyombo vya habari kuwa mkuu amerejea na siku inayofuata atakwenda tena Uganda.
    Da! Twaambulia ratiba tu, madhumuni tutajiju.
    Kama atapewa homework,sa sijui ataifanya kimya kimya, kwanza tutajuaje kapewa homework?
    Kazi ipo.

    ReplyDelete
  4. Asanteni saaana WAUNGWANA.
    Nakumbuka katika post ya awali akaka Kitururu alisema kinachomsikitisha ni kuwa NDANI YA UMOJA WA MATAIFA KUNA MATAIFA YASIYO NA UMOJA.
    Na hii inashangaza saana kuona kuna jina na siasa zaidi ya maana na ulengwa.
    Nimewanyaka Kaka zangu Kamala na Kissima.
    TZFORCHANGE. Karibu saana Mkuu changamotoni. Hakuna shaka kuwa nitakusaka na naamini tutaweza ongea mengi mema ya "kuikomboa jamii" yetu.
    Ni MABADILIKO TANZANIA tunayohitaji.
    Blessings

    ReplyDelete
  5. Hata utembeze viboko namna gani, hakitaeleweka kitu. Pengine hili litakuwa ndilo darasa ambalo litakuwa na wanafunzi watukutu, wakaidi, wabinafsi na wasiojali kuliko darasa jingine lolote hapa duniani kuanzia academy ya Plato enzi zile mpaka wakati huu.

    UN imeshakuwa "irrelevant" kama "League of Nations" wakati ule iliposhindwa kumnyamazisha Adolf Hitler wakati akijiandaa kuanzisha vita vya pili vya dunia.

    Tuko mwanzo mwanzo wa muhula na kazi zimepamba moto kwelikweli. Napita hapa kila ninapoweza ingawa pengine ni kwa mwendo wa kasi kiasi kwamba siachi nyayo zangu. Mambo yameanza kutulia na nyayo zangu utaziona tena mara kwa mara!

    ReplyDelete
  6. Mbona itakuwa vizuri...leo nimemuona Gaddafi...talking nonsense maana I can't even quote anyway kaka sorry but please correct this "Kikao hiki kilianza rasmi Kumanne ya Sep 15."...samahani ila ndio hivyo...the word is a bit distracting...lol

    ReplyDelete