Miaka inasonga na twakumbana na mengi. Twakumbana na masaibu makubwa na madogo na tunapokaa chini na kutafakari, tunatambua kuwa ndio TUNAKUZWA kwa kupambana nayo. Kuna mengi uliyokutana nayo na kuna mengi uliyoyashinda na ndio maana kwa ushindi huo unaweza kukaa chini na kutuelimisha meengi pasina hofu kwani twajua kuwa ULIKUWA KATIKA HALI HIYO NA UMEISHINDA.
Umekuwa chachu ya UTAMBUZI kwa wengi na mmoja kati ya wengi ni Mimi.
Basi katika siku hii muhimu ya kukumbuka kuzaliwa kwako, NAPENDA KUKUTAKIA KILA LILILO JEMA na kumbuka kuwa yote yatokeayo yana sababu.
Tupo PamoJAH na tutaendelea kuielimisha jamii yetu.
Nikuunganishe na Inno aliyekuwa akiuliza mengi kuhsu Maisha nami naamini wajiuliza mengi hasa kulingana na masaibu ya juzijuzi. Kwani maisha ni zawadi, majaribu ama adhabu kwa baadhi ya watu?
What is Life?? HERI YA SIKU YA KUZALIWA KAKA KALUSE
Hongera kwa sikukuu ya kuzaliwa Kaluse na pole kwa masahibu yaliyokupata. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akulinde!
ReplyDeletehongera basi
ReplyDeleteKaka Nashukuru sana kwa hili, naona hata maneno yameniishia,
ReplyDeleteKwa kweli namshukuru mungu kwa kuniwezesha kuiona siku hii ya leo ambayo ndio siku yangu ya kuzaliwa.... sijisikii kufanya lolote na ninataka siku ya leo niwe na utulivu kidogo ili kutafakari yajayo.....ni furaha iliyoje kuwa nipo na nitaendelea kuwepo na makala za utambuzi zitaendela kurindima kama kawaida.....kaka tupo pamoja Blessings.......