Monday, July 6, 2009

Za Kale vs Maisha ya sasa......KIU YA JIBU

Kuna nyakati ambazo kuzikumbuka ni burudani tosha. Nakumbuka enzi za kumpenda mtu ukamtumia ujumbe kupitia mtu mwingine, ama ukajitahidi kumuonesha wampenda kwa kukimbia kutamka na hivyo kusaka kila kitakachokuwezesha kufikisha ujumbe wako. Na baada ya hatua hiyo kupita, inakuja nyingine ambapo (kulingana na mazoea), msichana asingekujibu juu ya uamuzi moja kwa moja. Ina maana kijana angestahili kusubiri kwa muda huku akiwa na kiu ya kujua jibu litakalokuja toka kwa "mpendwa".
Ni wakati ambao kwa wale walioupitia wanakumbuka ilivyokuwa. Ni nyakati ambazo hakukuwa na kutumiana text messages, wala emails, na hata vi-barua havikuwa kwa wingi na simu ndio ilikuwa anasa. Kwa hiyo ilikuwa ni kusubiri "kalenda" ifike ili kupata jibu.
Jumatatu hii, tukumbushane nyakati hizo kwa kuwasilikiza DDC MLIMANI PARK katika kibao chao KIU YA JIBU.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa**

3 comments:

  1. Kweli kabisa nakumbuka jinsi watu walivyokuwa wanaandikiana vibarua shuleni na kumtuma mtu mwingine akampe yule aliyemwandikia. Kazi kwelikweli. Asante kwa ukumbusho.

    ReplyDelete
  2. Kwa Wasukuma ilikuwa taabu zaidi...we acha tu!

    ReplyDelete