Monday, August 17, 2009

Za Kale vs Maisha ya sasa......MOLA (ISIAKA KIBENE)

Toleo la kwanza la kipengele hiki lilihusisha wimbo wa DUNIA IMANI IMEKWISHA (Bofya hapa) ambamo tulieleza namna ambavyo ulimwengu umepoteza imani ambapo watu wanaonekana kutaka kujidhihirisha uwezo wao wa kimwili hata kama inamaanisha kuwadhalilisha ama kuwatesa wengine. Katika toleo la kumi la kipengele hiki, tukabandika wimbo BINADAMU HAWANA WEMA (Bofya hapa) ambalo nalo halikuwa mbali na maelezo kuhusu kujipoteza kwetu katika harakati za kujitafuta. Maishani siku hizi tumeshuhudia namna ambavyo binadamu wanaweza kuwa na ukatili usiosemeka na kutenda ambayo hayawezi kuaminika kutendeka kwa binadamu mwingine. Sikiliza kisa cha kusikitisha kilichorushwa katika kipindi cha LEO TENA kwa kuBOFYA HAPA na itaweza kusaidia kuelewa kwanini NINAENDELEA KUIOMBEA JAMII IREJEE KUWA ILIVYOKUWA AWALI kwenye kujali utu na kuuthamini.
Yaonekana KUONGOZWA NA UTASHI WA MWILI ni tatizo kubwa kwani kutokana na tofauti za mahitaji ya miili yetu tunajikuta TUNAENDELEA KUJIPOTEZA KATIKA HARAKATI ZA KUJITAFUTA (Isome)
Ndio maana JUMATATU ya leo naungana na wana Msondo ngoma katika kumuomba MOLA kuirejesha dunia iwe kama ile ya zamani.
Ndani mwake utamsikia Maalim Gurumo akiimba "imani na upendo duniani vimetoweka, ufukara na umaskini vimetawala"
Wasikilize wana Msondo.

Tx Moshi William, Othman Momba, Joseph Maina na Seleman Mwanyiro ni baadhi ya walioshiriki ktk wimbo huu ambao wameshatangulia mbele ya haki. MPUMZIKE KWA AMANI NA KAZI YENU YAENDELEA KUELIMISHA

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa**

1 comment:

  1. Ni kweli kabisa sasa binadamu wa sasa wamekuwa wakatili sana. Sasa sijui watu wa zamani walitumia mbinu gani ambayo sasa inashindwa kutumika? Asante sana kwa zilipendwa nimekumbuka nilipokuwa kachiki. Lol

    ReplyDelete