Monday, August 31, 2009

MPAKA TUZIKE NDIO MUAMKE (II)?????

Moto wa Shule ya Sekondari Idodi uliogharimu maisha ya wanafunzi 12. Picha toka kwa Blogu ya Kaka Francis
Ajali Morogoro. Picha kwa hisani ya Blogu ya Kaka Maduhu
Wiki hii inaanza. Inaanza ilhali iliyotangulia haikuwa na mwisho mwema kwa wandugu wengi waTanzania. Tumeendelea kushuhudia VIFO vinavyochukua maisha ya ndugu zetu weengi kwa sababu ambazo tungeweza kuzuilika. Inasikitisha saana kwani haioneshi kuwa kuna JITIHADA ZA KUZUIA VIFO HIVI zaidi ya "hadithi za TUNASHUGHULIKIA"
Tumeandika saana kuhusu kauli za wanasiasa wasiojua namna ya kuzuia ajali zaidi ya kuonekana KUIGIZA KUSIKITIKA pale yanapotokea madhara.
Tarehe 8 Septemba mwaka jana niliuliza swali kuwa MPAKA TUZIKE NDIO TUAMKE? (Bofya hapa) na japo tumebadilishiwa kivuko, lakini bado kuna mengi yanayohitaji kukingwa. Sote tunajua namna ambavyo vivuko vya Kigamboni viliwatenda wasafirishaji kabla hawajaletewa kipya.
Tunaona namna ambavyo ajali zinaua na hakuna aonekanaye kujitahidi KUZUIA AJALI HIZI. Majanga kama haya ya MOTO mashuleni yanaendelea kutokea na la kusikitisha ni kuwa wanawekeza kwenye kuchunguza sababu ya moto na si namna ya kuuzuia. Kisha kama ilivyo ada, zitatolewa salamu za rambirambi na ONYO KALI kisha kila kitu chasahaulika hapohapo. Sijui ni kwanini hatujitahidi kuzuia maafa haya? Yalishatokea ya kutisha na yaliyostahili kuwa funzo tangu enzi za Shauritanga, lakini hakuna hatua madhubuti zilizowekwa (ama nisemwe kubainishwa) kuzuia haya. Kwa yeyote ambaye amewahi kutembelea mabweni ya shule atakubali kuwa HAKUNA VIWANGO VYAYO na sina hakika kama kuna ukaguzi kuangalia kama mabweni yote nchini yanafaa JAPO KUTUMIKA KAMA MAKAZI YA WATU ACHILIA MBALI WATU WANAOTAKIWA KUWA NA MAZINGIRA MAZURI KUWEZA KUFANIKIWA KIELIMU.
Tukitaka kugusa kuhusu ajali za barabarani itakuwa ni kurejesha maumivu kwa wengi. Binafsi nilishasema kuwa TUMECHOSHWA NA SALAMU ZA RAMBRAMBI (Iko hapa kama uliikosa) na bado hatuoni hatua madhubuti za kuzuia ajali hizi. Kama tutaanza kujadili "mabati na utengenezaji" wa mabodi ya mabasi yasafirishayo abiria, sifa na uhalali wa madereva waliopo barabarani wakisafirisha ndugu zetu, usalama wa mabasi hayo, matengenezo yake muhimu, usajili na mengine ya muhimu yanayostahili kuangaliwa kabla hayajaruhusiwa kuwa barabarani, basi tutaishia kujiumiza wenyewe (labda kwa kuwa wenye dhamana hawajali).
Na ndio maana najiuliza kwa mara ya tena kuwa MPAKA TUZIKE NDIO MUAMKEEEEE???
Heaven Help Us All

4 comments:

  1. Ninanukuu "Majanga kama haya ya MOTO mashuleni yanaendelea kutokea na la kusikitisha ni kuwa wanawekeza kwenye kuchunguza sababu ya moto na si namna ya kuuzuia." mwisho wa kunukuu:- Kama serikali ingefanya mkazo wa kuweka umeme mashuleni vifo vyote hivi havingetokea lakini wao wamekuwa vipofu hawaoni tatizo badala yake wanapeleka watoto wao kwenye shule bora zaidi huku wakilipa ada kubwa kwa fedha za serikali. Inasikitisha sana kuona hili SIJUI NI LINI TUTAAMKA?????

    ReplyDelete
  2. Yasinta sio serikali tu bali pia hata sisi tungejaribu kuchangia maendeleo ya shule zetu na kununua umeme wa sola vifo visingetokea.

    katika safari yangu ya mikoani iliyomalizika juma la jana, nilikuwa katika hoteli moja kubwa usiku ghafra nikajisikia kuishiwa na amani nikaona kama moto unawaka au jengo linaporomoka. nikajikaza kisabuni na asubuhi nikajishangaa niko mzima.

    kazi ipo

    ReplyDelete
  3. Tumeshakuwa watu wa kuuguza vidonda tu, badala ya kujikinga tusivipate.
    Mzee wa Changamoto, inabidi uwe mshauri wa waziri mkuu katika masuala ya majanga au vp?

    ReplyDelete