Katika moja ya posti zake za J2 ya Septemba 7, Kaka Michuzi Jr alionesha kile alichoita uchunguzi usio rasmi ambao ulionesha namna vifaa muhimu vinavyosaidia kutoa taarifa itokeapo hitilafu ama janga la moto katika jengo kubwa na muhimu la Kitega Uchumi vikiwa vimeharibika (http://michuzijr.blogspot.com/2008/09/uchunguzi-usio-rasmi.html#comments) na kutofanya kazi ilhali bado tuna taswira ya kile ambacho kimeshalikumba jengo hilo refu miaka michache iliyopita. Kutofanya kazi kwa vifaa hivyo vinavyosaidia kutaarifu walio ndani ya jengo kutoka kukiwa na moto na hivyo kusaidia kuokoa maisha ya watu na mali, kunaashiria kutotiliwa maanani kwa suala la kusaidia kuokoa maisha kabla janga halijawa kubwa. Nakumbuka ktk likizo yangu pia nilishuhudia "boti ya uokozi" iliyoegeshwa Kigamboni ambayo kwa namna yoyote ile haiwezi kutosha kuokoa endapo pantoni zetu zilizozeeka na zinazoharibika "kila siku" zitaleta tafrani.
Hivi ni kweli kwamba wahusika hawaoni haya ama mpaka maafa yatokee ndio tuamke?
MENGINE YANAEPUKIKA.
Ni Changamoto tuuuuuuuuu
Hivi ni kweli kwamba wahusika hawaoni haya ama mpaka maafa yatokee ndio tuamke?
MENGINE YANAEPUKIKA.
Ni Changamoto tuuuuuuuuu
No comments:
Post a Comment