Sunday, September 7, 2008

Winston "Burning Spear" Rodney.

.Umri kwake si kikwazo
.Nidhamu ya hali ya juu na muziki uliopangiliwa.
.Ujumbe kwa watu wa rika, rangi na maisha yote


Burning Spear akifanya vitu vyake stejini



Akiikonga hadhira kwa kongas




Akilishambulia jukwaa ktk "Original Roots Reggae" style


" Talk to me my People"

Mamia ya washabiki wa Roots Reggae wakionekana kukubali kazi njema ya Winston "Burning Spear" Rodney

Kwenye front row, tulikuwepo kina sie kumfaidi "Grandpa" . He's Great

Kama umri ni kikwazo kwa wengi katika muziki, basi hilo si tatizo kwa Mwanamuziki maarufu wa Reggae ulimwenguni Winston Rodney a.k.a Burning Spear. Mkongwe huyo ambaye ni mshindi wa tuzo mbalimbali ikiwemo Grammy ya Best Reggae Album kwenye toleo lake la mwaka 200 la Calling Rastafari usiku wa kuamkia leo alifanya show moja kali katika ukumbi wa Recher Theatre uliopo maeneo ya Towson hapa Maryland. Akionesha NIDHAMU ya juu katika muda na muziki pia, Burning aliweza kuwadhihirishia mamia ya ma-askari wa Reggae waliomiminika ukumbini (wengi wao wakiwa wazungu) kuwa miaka 39 katika muziki wa Reggae imemkomaza vilivyo na aliweza kuonesha uwezo mkubwa saana katika kulitawala jukwaa. Burning Spear (jina alilotoa kwa Rais wa kwanza wa Kenya Hayati Jomo Kenyatta) aliimba nyimbo zake kama Days of Slavery, Columbus, Marcus Garvey, O Rastaman, na nyingine nyingi zikiwemo mpya zipatikanazo ktk albamu yake mpya ya Jah Is Real iliyotoka tarehe 17 mwezi uliopita.
Upande wa ala (ambao anaheshimika zaidi) aliweza kuonesha utaalamu wa hali ya juu na "coordination" ya ajabu baina ya wapiga ala wake na kwa hakika bendi yake ilicheza Instuments ambayo sijawahi kuona "live" katika onesho lolote maishani mwangu.
Huyo ndo Burning Spear, miaka 63 (39 kati yake kwenye muziki) mpigania Amani, Haki na Utu akiviunganisha na ujumbe wa Siasa na Imani yake katika U-Rasta na umoja wa watu weusi.
Waweza kumpata kwa kubofya http://www.burningspear.net/
Blessings

1 comment:

Anonymous said...

JAH Bless I n I brethren!