Sunday, September 7, 2008

Kumbe Tanzania tuko juu, Kwanini bado maskini?


Baadhi ya vikwangua anga jijini Dar vinavyochochewa na kuchochea uwekezaji na huduma za kibenki


Tanzania imetajwa kama nchi ya 78 katika nchi bora za kufanya biashara ulimwenguni kwa mwaka 2008. Kwa mujibu wa matandao wa Forbes unaojihusisha na habari za Mapato na Biashara, takwimu zilizotolewa miezi miwili iliyopita zaionesha Tanzania kuwa imepanda nafasi 26 toka ile iliyokuwa nayo mwaka jana ya 104 na sasa iko nafasi moja juu ya China iliyoshuka nafasi mbili toka mwaka jana.
Imeonesha kuwa ukuaji wa viwanda, madini hasa Dhahabu, mabadiliko ya mfumo wa kibenki na uwekezaji, michango ya wahisani pamoja na sera madhubuti za uchumi ni kati ya vigezo vilivyoiweka Tanzania katika nafasi hiyo. Lakini pia miundombinu chakavu imekuwa kikwazo katika uwekezaji na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
Natumai siku moja mwenye werevu na mamlaka atajitokeza kueleza kwa nafasi hii na vitu hivi tulivyonavyo na vingine ambavyo havijatajwa, kwanini tukingali maskini.
waweza ku-bofya http://www.forbes.com/business/lists/2008/6/biz_bizcountries08_Tanzania_CHI105.html kwa habari zaidi

No comments: