Thursday, September 4, 2008

Hizi Jumuiya za nini na za nani?

Tumekuwa tukishuhudia kuzinduliwa kwa Jumuiya za waTanzania waishio nchi mbalimbali na kwa hakika wamwkuwa wakiweka malengo na Katiba zenye kuonesha kuwajali na kuwasaidia saana wenzetu huko walipo. Lakini Jumuiya nyingi (na hapa nasema si zote) hutokomea baada ya hapo na kurejea wakati wakiomba michango kusaidia shughuli za Maziko na Mazishi ya wenzetu na wakati wa matamasha na michezo.
Hivi ni kweli kuwa mambo tuyaonayo yakiwekwa kwenye blogs ndio pekee wafanyayo, ama kuna mema mengi waendeleayo nayo bila kuweka hapa? Na kama wanatangaza sera zao hapa na kufanya mengine kupitia mitandao hii, ni kwa nini hayo mengine mema wasiyaweke pia tuwashukuru? Ama ni kwamba Jumuiya hazifanyi kazi zao katika kuwasaidia waTanzania walio ndani ya maeneo yao? Na kama hazifanyi kwani ni Jumuiya za nani na za nini? Ni changamoto tuuuu

No comments: