Thursday, September 4, 2008

Mapenzi yake yatimizwa

Mwili wa Angel Pantoja Medina ukiwa umeegeshwa ukutani pembeni ya jeneza lake wakati wa kutoa heshima za mwisho nyumbani kwa mamake huko San Juan. Puerto Rico Mama na Kaka wa marehemu wakielekea uliko mwili wa Angel wakiwa pamoja na waombolezaji wengine


Katika hali ya kushangaza, kijana Angel Pantoja Medina wa San Juan, nchini Puerto Rico aliweka usia kuwa akifariki mwili wake usimamishwe pembeni ya jeneza lake wakati wa kutoa heshima za mwisho kabla ya maziko. Na ndivyo ilivyokuwa Jumatatu ya August 18 (kama muonavyo pichani) ambapo kijana huyo aliyesemekana kuuawa tarehe 15 August alisimamishwa pembeni ya ukuta wa nyumba ya mamake akiwa ameegemezwa ukutani akiwa amevalishwa vema ili watu waweze kutoa heshima za mwisho.

Hivi USIA una nguvu kiasi hiki?

Picha na habari kwa toka Associated Press (AP)

1 comment:

Triple S said...

Ni jambo la aina yake kwa usia kuwa na nguvu namna hii na sijui wamefanyaje maana nimebaki hoi.