Tuesday, September 2, 2008

Changamoto yetu Wanasiasa "watoto"


John Tyler Hammons ni kati ya ma-Meya wenye umri mdogo kabisa hapa nchini Marekani na ni kati ya ma-meya wenye umri mdogo wanaohudhuria mkutano unaoendelea kumuidhinisha mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican huko Minnesota. Akiwa na umri wa miaka 19, Meya Hammons alishinda uchaguzi wa kiti hicho katika mji wa Muskogee, Oklahoma kwa asilimia 70 ya kura dhidi ya meya aliyewahi kushikilia kiti hicho kwa mihula mitatu na anajumuishwa katika kundi la viongozi hao wachanga lijumuishalo Mayor . Hii yaweza kuwa changamoto kubwa kwa wanasiasa wachanga nyumbani na alama ya mabadiliko kwa wakongwe wasiopenda kung'atuka. Ni CHANGAMOTO YETU sote kujua mabadiliko tuhitajiyo, watu watakaotuletea na kisha kuwachagua pasina kung'ang'ania kina fulani ambao wamekuwepo miaka nenda rudi bila mabadiliko.
Kwa habari zaidi juu ya John Tyler Hammons click http://en.wikipedia.org/wiki/John_Tyler_Hammons na kwa orodha ya ma-meya wenye umri mdogo kupata kushika nafasi hizo nchini marekani bofya http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_the_youngest_mayors_in_the_United_States

No comments: