Showing posts with label Ana kwa Ana. Show all posts
Showing posts with label Ana kwa Ana. Show all posts

Friday, February 28, 2014

Ana kwa Ana ya Jamii Production na Dr Wilbrod Slaa



Jamii Production imepata fursa ya kipekee kuhojiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Wilbrod Slaa Hii ni sehemu fupi ya mahojiano haya yaliyodumu kwa dakika 90
Lakini pia msikilize alivyozungumzia kesi ya mwekezaji aliyedhulumiwa mali zake katika jimbo la Karatu ambalo yeye (Dr Slaa) alikuwa mbunge kwa miaka 15

Wednesday, December 11, 2013

Ana kwa Ana na Mhe. January Makamba

Karibu katika mahojianokati ya Jamii Production na Mhe January Makamba.
Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ameeleza mengi na kujibu maswali ya wasikilizaji wetu waliyouliza kupitia ukurasa wetu wa Facebook
KARIBU

Monday, November 4, 2013

Mahojiano ya Jamii Production na Dj Luke Joe wa Washington DMV


Dj Luke akiwa studio na Mubelwa Bandio wa Jamii Production
Karibu katika mahojiano na Dj mkongwe kutoka Tanzania na mmiliki wa blog ya Vijimambo Lucas Mkami a.k.a Dj Luke Joe
Dj Luke ambaye makazi yake kwa sasa ni Maryland nchini Marekani ameeleza mengi kuhusu kazi zake hizi.
Katika mahojiano haya, ameeleza historia yake katika kuchezesha muziki, aliyemvutia kuingia katika kazi ya uDj, mafanikio ya Dj, changamoto zake, ku-blogu na mengine mengi.
Karibu Uuungane nasi

Monday, October 14, 2013

Mahojiano ya Jamii Production na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Dr Charles Kimei


Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kulia) akizungumza na Jamii Production  ndani ya ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico uliopo Jijini Washington DC
Jumatano ya Oktoba 9, 2013, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRBD Dr Charles Kimei akiambatana na Mkurugenzi wa Masoko wa (CRDB) Tully Mwambapa, Bw. Mkurugenzi wa Hazina (CRDB) Alex Ngusaru na Msaidizi wa Dk.Kimei , Kenneth Kasigila walikuwa jijini Washington DC (pamoja na mambo mengine) kueleza mipango ambayo CRDB inayo katika kuboresha huduma za akaunti ya Tanzanite pamoja na kutambulisha huduma mpya ya JIJENGE.
Jamii Production ilipata fursa ya kuhojiana na Dr Kimei ambaye amefafanua mengi kuhusu huduma hizo.
KARIBU UUNGANE NASI

Na hapa chini ni mahojiano hayo katika SAUTI (AUDIO)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei na akipata picha na mpiga picha mkuu wa Jamii Production Abou Shatry baada ya mahojiano.

Wednesday, October 9, 2013

Ana kwa Ana ya Jamii Production na Hezekia Mwalugaja

Jamii Production tulipata fursa ya kuhojiana na mlezi-kiongozi wa Hananasif Ophanage Center (HOCET)  Hezekia Mwalugaja katika studio zetu hapa Washington DC
Ameeleza mengi kuhusu kituo anachoongoza.
Jinsi kilivyoanza, mahala kilipo, tofauti yake na vituo vingine vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu,
Pia ameeleza kuhusu jambo / mambo yayayomsikitisha kuhusu vituo vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu Tanzania
Kaeleza kuhusu shule waliyoanzisha maalum kwa watoto hao, mafanikio waliyoanyo (ambayo ni ya kujivunia hakika) na mengine mengi yatakayokufanya usijutie muda wako kufuatilia mahojiano haya.

KARIBU UUNGANE NASI

Sunday, September 29, 2013

Ana kwa Ana na Dr Willbrod Slaa

Karibu katika sehemu mbili za mahojiano na Katibu Mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzanzia, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Willbrod Slaa yaliyofanyika Septemba 22, 2013 hapa Washington DC
Kati ya aliyozungumza ni pamoja na
1: Hali ya kisiasa nchini Tanzania hivi sasa
2: Nini walichomaanisha waliposema "nchi haitatawalika"?
3: Ni kweli kuwa CHADEMA inaamini kuwa Tanzania hakuna amani?
4: Kuna namna ambavyo tunaweza kutenganisha "siasa na maamuzi ya serikali"?
5: Anaonaje tofauti ya UTENDAJI WA BUNGE baina ya kipindi alichokuwepo yeye na hili la sasa?
6: Vurugu zinazotokea bungeni.....Kwanini?
7: Harakati za kuungana na wapinzani wengine kupinga mchakato wa katiba..."hamjifuniki wakati kumekucha?"
8: Maswali ya wasikilizaji na wasomaji wetu
9: Kwanini CHADEMA inahusishwa na vurugu katika mikutano yake?
10: Kwanini hawajatoa mkanda wa mauaji ya Arusha waliosema wanao?
11: Kwanini hawawajibishi baadhi ya wabunge ama wanachama wanaoonekana kuasi chama?
12: Maendeleo Tanzania. Yanapangwa kulenga maendeleo mjini?
yanagawa umaskini kuwa wa mjini na vivjijini?
Na mengine mengi

KARIBU UUNGANE NASI

Tuesday, August 27, 2013

Mjadala wa rasimu ya Katiba mpya DMV

Karibu katika sehemu mbili za mjadala uliohusisha BAADHI viongozi na wanaharakati wa siasa waishio Washington DC
Katika sehemu ya kwanza, wachangiaji walikuwa viongozi wa CHADEMA tawi la Washington DC ambao wameeleza mtazamo wao na wa chama chao kuhusu rasimu hiyo.
Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Tawi Bwn. Kaley Pandukizi, Katibu wake ambaye pia ni Afisa Habari Bwn Liberatus Mwang'ombe na Mweka Hazina wa Tawi Bwn. Ludigo Mhagama
Na katika sehemu ya pili, Mwenyekiti na Katibu wa CHADEMA DMV waliungana na mwanaharakati wa chama cha CUF ambaye pia ni mmoja wa waasisi na Katibu wa Zanzibar Diaspora USA Bwn. Shamis Abdul kujadili mambo mbalimbali katika katika
Karibu uungane nasi

Edibily Lunyamila akilonga na Vijimambo

Edibily Lunyamila alipokuwa akishuhudia mazoezi ya timu ya Yanga katika makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar Es Salaam. 
Photo Credits: Bin Zubeiry
Mcheza soka nyota wa zamani wa kimataifa Edibily Lunyamila, amefanya mahojiano na Dj Luke wa blog ya Vijimambo na kueleza mambo mbalimbali ikiwemo shughuli zake baada ya kustaafu soka na hata anavyolinganisha soka la "enzi" wake na sasa.
Pia kagusia changamoto ambazo wachezaji wastaafu wanakumbana nazo na maoni yake katika kukuza soccer la Tanzania
MSIKILIZE

Kijiwe cha ughaibuni

Karibu katika kipindi kingine cha KIJIWE CHA UGHAIBUNI kinachoandaliwa na Blog ya Vijimambo.
Katika kipindi hiki, wadau hujadili mambo mbalimbali yanayoikumba jamii yetu na kujaribu kuweka mtazamo wao kuhusu namna ya kukabiliana na matatizo wayajadiliyo
Leo hii, wameanza na suala la KATIBA MPYA YA TANZANIA
KARIBU UUNGANE NAO

Thursday, August 22, 2013

''Bongo Views'' ya GENN Redio toka kwa waTanzania wanaoishi Kansas City

Global Entertainment and News Network (GENN) iliyopo Kansas City nchini Marekani, inatambulisha kwenu kipindi  kipya cha BONGO VIEWS kitakachokuwa kikiwajia moja kwa moja kila Jumamosi  kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya kati (12 jioni kwa Marekani ya Mashariki)
Photo
Muendesha wa kipindi cha Bongo Views Joshua Kijo Simon Madelkeka akiendelea kujadili pamoja na washiriki wake kuhusu suala la uraia wa nchi mblili na mambo mengine ndani ya Studio ya Global Entertainment and News Network (GENN)
Photo: BONGO VIEWS: ANDY MKINGA and BAVON
Wachangiaji kipindi  kushoto Mjombo Andrew Mkinga,  akiwa na Anko Bavon Mwakasungula, wakijadili Mjadala kuhusu uraia wa nchi mblili na mambo mengi kuhusu mstakabaliwa nchi yetu, wakiwa ndani ya Studia ya Global Entertainment and News Network (GENN)

Kipindi cha Bongo Views  kitawajia tena LIVE wiki hii, siku ya Jumamosi Aug 24, 2013  kuanzia Saa 11 jioni kwa Saa za Marekani ya kati.  (Saa kumi na mbili jioni kwa Saa za EST US.)
Kwa wale mtakaopenda kushiriki,  msikose kutembelea. HAPA Global Entertainment and News Network (GENN).

Mjadala utakua kuhusu tatizo la madawa ya kulevya nchini.
Ili kuchangia kwa njia ya simu, piga simu namba  (913) 662-1190

Wednesday, August 14, 2013

Kijiwe cha Ughaibuni


Karibu katika kipindi kingine cha KIJIWE CHA UGHAIBUNI kinachoandaliwa na Blog ya Vijimambo.
Katika kipindi hiki, wadau hujadili mambo mbalimbali yanayoikumba jamii yetu na kujaribu kuweka mtazamo wao kuhusu namna ya kukabiliana na matatizo wayajadiliyo
KARIBU UUNGANE NAO

Tuesday, August 13, 2013

SwahiliVilla blog katika tamasha la FestAfrica 2013 MD USA


Miongoni mwa waliolonga na SwahiliVilla Blog (SVB) ni mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya FestAfrica, mTanzania Nenelwa, kutoka Baltimore Maryland. Ungana na Abou Shatry katika mahojiano haya

Monday, August 12, 2013

Ana kwa Ana ya SwahiliTv na Mfanyabiashara Davis Mosha

Wadau wenzetu wa habari SwahiliTv, walipata nafasi ya kuongea na mmoja wa wafanyabiashara maarufu toka nchini Tanzania Bwn. Davis Mosha alipokuwa katika ziara nchini Marekani.
Ungana na mtangazaji Alex Kassuwi wa Swahili Tv katika mahojiano haya

Friday, August 9, 2013

Tamasha kubwa la muziki wa Injili kufanyika Washington DC kesho

Waimbaji wanaofanya vema kwenye muziki wa Injili Afrika Mashariki, Upendo Kilahiro na Christina Shusho, watatumbuiza katika Tamasha kubwa la Injili litakalofanyika Jumamosi hii jijini Washington DC
Kama walivyoongea kwenye VIDEO HII, waimbaji hao wamekamilisha maandalizi ya tamasha hilo ambalo pia litashirikisha waimbaji wenyeji wa hapa Marekani.
Tamasha hilo kubwa lililo sehemu ya Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries litafanyika siku ya Jumamosi kuanzia saa kumi kamili mpaka saa tatu usiku (6:00pm - 9:00pm) na kiingilio kwenye tamasha hilo kitakuwa ni dola kumi ($10) kwa watu wazima, bure kwa watoto.
Anwani ambapo litapofanyika tamasha hilo ni
The Way of the Cross Gospel Ministries 
(at University United Methodist Church) 
3621 Campus Drive 
College Park, MD 20740 
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na
Mch. Ferdnand Shideko +1 240 476 6718 ama
Ms Flora Mnkande +1 240 217 6335
Waimbaji hawa wote watatumbuiza nyimbo zao za zamani na mpya na wanawaalika watu wote kujumuika nao na waimbaji wenyeji kuweza kupata BARAKA kwa njia hii ya uimbaji

Tuesday, August 6, 2013

Kijiwe cha Ughaibuni


Karibu katika kipindi kingine cha Kijiwe cha Ughaibuni kinacholetwa kwenu na Blog ya Vijimambo.

Sunday, July 28, 2013

Ana kwa Ana ya Sunday Shomari na Mhe. Edward Lowassa

Karibu katika sehemu mbili za mahojiano baina ya Mtangazaji Sunday Shomari na Waziri Mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na M'bunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa yaliyofanyika siku ya Jumatano Julai 17, 2013 jijini Washington DC.
KARIBU

Tuesday, July 23, 2013

Ana kwa Ana na wadau wakuu wa GENN Radio (Kansas U.S.A)

Photo Credits: Swahili Villa blog
Karibu katika Mahojiano haya baina ya Jamii Production na wadau wakuu wa Global Entertainment and News Network (GENN) iliyopo Kansas City nchini Marekani. Katika mahojiano haya, utasikia Mkurugenzi wa kituo Bwn. Robert Otto na watangazaji AJ na Dada D wakizungumzia harakati zao kwenye kituo hiki kipya cha Radio.
 

Friday, July 19, 2013

Ana kwa Ana ya Swahili Tv na Mhe. Edward Lowassa

Wanahabari wenzetu wa Swahili Tv, walipata fursa ya kuhojiana na Waziri Mkuu wa Zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa.
Pamoja na Mambo mengine, Mhe. Lowassa anawaasa wanaDiaspora kuungana mkono katika shughuli zao, kupendana na kutakiana mema
Pia anaongelea swala la elimu, mchakato wa katiba na mustakabali mzima wa siasa za Tanzania

Tuesday, June 11, 2013

VIDEO: Mahojiano na Mhe. Balozi Amina Salum Ali

Karibu katika sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano kati ya Jamii Production na Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali.
Katika sehemu hii, Mhe Amina ameeleza mengi ikiwemo...
1: Historia ya maisha yake.
2: Aliingia vipi kwenye kazi ya diplomasia?
3: Ni nini wajibu wake? Anawajibika kwa nchi ya Marekani ama na mashirika ya kimataifa kama IMF na World Bank?
4: Ni wapi ulipo mpaka kati ya majukumu ya mabalozi wa nchi wanachama wa AU na yeye anayewakilisha Umoja?
5: AU ina mikakati gani katika kufunda ama kuwalea viongozi wa afrika?
6: Kuna MAFANIKIO GANI ya Umoja wa Afrika hasa ukizingatia kuwa tangua kuanzishwa kwake tumeshuhudia nchi zikizidi kugawanyika badala ya kuungana kama Ethiopia na Eritrea na hata Sudan na Sudan ya Kusini?
7: Ni nini kinachokwamisha Umoja wa Afrika katika migogoro kama ya Kongo?
8: Nchi zetu ziko huru, zinajitawala, lakini ni kwa MANUFAA YA NANI?
9: Ni kweli kuwa Umoja wa Afrika unaendelea kuwepo si kwa mafanikio yake, bali kwa kukosekana kwa UMOJA M'BADALA?
10: Ni kweli kuwa kuna mamluki wanaokwamisha harakati za Umoja wa Afrika toka nje ya bara letu?
11: Tofauti ya mifumo ya utawala na nguvu za kijeshi na uchumi zinaathiri vipi UMOJA WA AFRIKA?
KARIBU UUNGANE NASI
Katika sehemu hii ya pili, Mhe. Balozi Amina amezungumza mengi ikiwa ni pamoja na....
1: Nafasi ya wanawake katika maamuzi na maendeleo ya Afrika. Je! Idadi kubwa ya wanawake tulionao katika nyadhifa barani Afrika ni ishara ya maendeleo ama ni "nafasi za upendeleo"?
2: Anaitafsiri vipi DEMOKRASIA YA AFRIKA na anaamini kipimo cha Demokrasia barani Afrika kingekuwa nini?
3: Ni nini anachoamini kuwa kingefanyika barani Afrika ili kuleta demokrasia ya kweli?
4: Anaamini Umoja wa Afrika umefanikiwa kwa kiasi gani katika madhumuni ya kuanzishwa kwake?
5: Je! Anaamini kuwa RUSHWA itaisha barani Afrika?
6: Yeye kama Mwanasiasa, Mwanadiplomasia na mTanzania, anazionaje siasa za Tanzania kuelekea 2015?
7: Anaishauri nini serikali katika kukabilaiana na ukuaji wa TEKNOLOJIA YA HABARI?
8: Kutokana na hali ilivyo Tanzania hivi sasa, anaionaje nafasi ya mwanamke katika kuongoza Tanzania?
9: Nini wito wake kwa wale wote wanaofuatilia mahojiano haya?
KARIBU UUNGANE NASI

Kijiwe cha Ughaibuni....Vijimambo

Karibu katika kipindi kingine cha Kijiwe cha Ughaibuni kinacholetwa kwenu na Blog ya Vijimambo.

Kijiwe 25