Showing posts with label Entertainment. Show all posts
Showing posts with label Entertainment. Show all posts

Sunday, March 19, 2017

Mahojiano na Dj D - Ommy ndani ya Kilimanjaro Studios U.S.A


Machi 16 2017, Mubelwa Bandio na Viola walipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Dj D-Ommy katika studio za Kilimanjaro Studios.
Dj D-Ommy ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani amezungumza mengi kuhusu maisha, kazi na tasnia nzima ya muziki.
Pia akapata fursa kuzindua rasmi kifaa kipya cha kazi kwa studio yetu, Pioneer DDJ SZ2
Karibu usikilize

Tuesday, November 26, 2013

Ngoma Africa Band "wauteka" mji wa Bremen,Ujerumani kwa muziki

Wavuna umati wa washabiki wa kimataifa
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya Ngoma Africa almaarufu FFU ughaibuni,usiku tarehe 23 Novemba 2013 walifanikiwa kwa mara nyingine kuliteka jiji la Bremen nchini Ujerumani. Kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU alikiongoza jukwaani kikosi kazi chake katika jumba la Übersee-Museum akiwa na matumaini kuwa wanaenda kutumbuiza washabiki "high class" (wenye hadhi ya kibwanyenye) lakini mziki ulipoanza mdundo uliwachanganya washabiki na kila mmoja alijimwaga uwanjani !
Ngoma Africa Band walijikuta wapo katika kibarua kama kawaida yao cha kushambulia kwa virungu vya muziki na kufanikiwa kuupanua wigo wake kwa kuwanasa mashabiki wengi wa kimataifa.
Bendi hiyo iliyojiimarisha na kujenga himaya ya kimataifa kwa kutumia muziki wake, imekuwa ikitajwa kama bendi bora ya kiAfrika barani ulaya.
Bendi ya Ngoma Africa inafanananishwa sawa na kikosi maalumu cha kuzuia ghasia FFU, lakini pia ina majina mengi ya utani na kiusanii kama vile Viumbe wa ajabu  "Anunnaki Elien" n.k ambayo imepewa na washabiki au wapenzi wake.
Kiongozi wake pia ana majina kama vile kamanda Ras Makunja wa FFU ,mtawala wa Anunnaki Empire.
Ngoma Africa band wanasikika kupitia www.ngoma-africa.com

Saturday, July 6, 2013

Sunday, June 30, 2013

Makamilisho ya Tamasha la Kiswahili ....Masanja, Shilole wawasili DC

Sherehe za miaka mitatu ya blog ya vijimambo itakayoambatana na Tamasha la Utamadunmi wa Kiswahili zinazidi kukamilika ambapo wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole ambao wanatarajiwa kutoa burudani siku hiyo wameshawasili hapa Washington DC.
Mgeni rasmi katika siku hiyo ambaye ni Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi anataraji kuwasili alhamis ya Julai 4.
Zifuatazo ni baadhi ya taswira za kuwasili kwa wasanii hawa hi leo
 Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa Kiswahili, Bwn. Baraka Daudi alipokwenda kuwapokea walipotinga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
 Dada Asha Riz, mjumbe aliyewawakilisha Tano Ladies kwenye mapokezi hayo akipata picha ya pamoja na wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole mara tu walipowasili uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole wakielekea kuchukua usafiri kuelekea Washington, DC
 Masanja na Shilole katika picha ya pamoja nje ya uwanja wa ndege waKimataifa wa Dulles.

Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog

Thursday, March 29, 2012

KALI Tv......Connecting Africans in the Diaspora

KaliTV's show includes two segments: one that covers entertainment news as well as social and cultural events in diaspora communities, and the other that looks at issues facing Africans in the diaspora through news coverage, interviews, and short programs on special topics of interest.

This week Kali TV focuses on the New African Films Festival at the AFI Theater in Silver Spring, Maryland.

Saturday, November 26, 2011

NI LEO...USIKOSE

TICKETS FOR "THE 2ND ANNUAL MITINDO NITE" AVAILABLE NOW...
$20 ADVANCE | $25 DOOR | $30 V.I.P. (FRONT ROW SEATING - UP CLOSE & PERSONAL) FOR TICKETS CONTACT: 240-413-3801 | 202-660-8228 | 571-445-0008


ADDRESS: 2126 INDUSTRIAL PKWY, SILVER SPRING, MD 20904

Wednesday, November 23, 2011

Burudani toka Afrika Mashariki

Kama inavyoonyesha hapa chini, ni usiku wa burudani ya kiAfrika Mashariki katika ukumbi wa RANDEZVOUS, uliopo
11910 PARKLAWN DR,
ROCKVILLE,MARYLAND 20852

Wasanii Chameleon wa Uganda, AJ Ubao wa Tanzania na Kanja toka Kenya wanatarajiwa kuburudisha.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na DMK GLOBAL kupitia 301-661-6207

Saturday, June 25, 2011

Miss Morogoro 2011

Tarehe 01 / 07 / 2011, katika hoteli ya Morogoro Hotel, warembo 15watapanda jukwaani kuwania taji la Miss Morogoro 2011. Shindanolitaanza saa mbili usiku hadi saa sita likishindikizwa na burudanikabambe toka kwa timu nzima ya Tip Top Connection, pamoja na vibwagizobabukubwa toka kwa msanii Wanne Star.Kiingilio kitakua 10,000 Tsh kwa mtu mmoja.
WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAKUFUNZI WAO, MRATIBU, MKURUGENZI WA FG ARTS PROMOTION, NA WAWAKILISHI WA WADHAMI WAO. AMBAO NI REDDS NA VODACOM TANZANIA.
WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 KWENYE PICHA YA PAMOJA WAKIPATIWA ELIMU YA MAZINGIRA KUFUATIA KAULI MBIU YA SHINDANO HILO MWAKA HUU, AMBAYO NI “BETTER ENVIROMENT TODAY” (BET).
WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 REHEME MARWA (KUSHOTO) NA SHARIFA ISSA (KULIA).
WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 SALMA KUYELA (KUSHOTO) NA ASHA SALEH (KULIA).
WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 TOKA KUSHOTO NI NAJMA ALLY, SALMA S. KUYELA NA BERTHALIUS USIRI.
WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 TOKA KUSHOTO NI AGNESS ROISER, PENDO DANIEL NA HASNAT KHAMIS.
MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 ASHA SALEH AKIWA KAMBINI KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE.
MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 BERTHALIUS USIRI AKIWA KAMBINI KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE.
MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 SHARIFA ISSA AKIWA KAMBINI KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE.
MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 REHEMA MARWA AKIWA KAMBINI KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE.
MSHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 RUBY JOSEPH AKIWA KAMBINI KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE.
WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 KWENYE PICHA YA PAMOJA WAKIPATIWA ELIMU YA MAZINGIRA KUFUATIA KAULI MBIU YA SHINDANO HILO MWAKA HUU, AMBAYO NI “BETTER ENVIROMENT TODAY” (BET).
BAADHI YA WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 WAKIPATA KIFUNGUA KINYWA KAMBINI MWAO KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE MOROGORO.
BAADHI YA WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MOROGORO 2011 WAKIPATA CHAKULA CHA JIONI KAMBINI MWAO KWENYE HOTELI YA MASUKA VILLAGE MOROGORO.

Picha na habari kwa mujibu wa SOUL MAKINI: Wakala wa Miss Tanzania ngazi ya mikoa na Mratibu wa mashindano ya urembo mkoa wa Morogoro (Miss Morogoro 2011).

Sunday, February 20, 2011

Jelani Film Premiere. Sunday March 13, 2011 at 7:00pm [ET]. BETHESDA, MD


Exclusive Film Premiere
Jelani
Written by Omar Chase Kaseko & Sasha Ryan
Directed by Omar Chase Kaseko
Produced by Kali Imagez & Ashes Film Production

Jelani tells the story of an inter-cultural relationship between
an African immigrant from Tanzania and an African-American woman
living in the United States. The film illustrates significant differences and tensions between
these two communities, addressing complex factors to include gender, class, and education.

The movies at Montgomery mall
7101 Democracy Blvd
Bethesda, MD

The link to buy tickets online :
http://jelanipremiere.eventbrite.com/

Monday, November 10, 2008

Hongera Miriam Odemba

Miss Earth 2008 Karla Henry
Miss Earth Tz Miriam Odemba

Mshiriki na mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kumsaka Miss Earth 2008 Miriam Odemba amefanya kile ambacho wengi walimtabiria. Kuwa miongoni mwa washindi wa shindano hilo.
Odemba ambaye ameshika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro hicho kilichofika tamati jioni ya leo huko jijini Angeles, Pampanga nchini Phillipines, ameweza kuitangaza vema Tanzania kwa kushinda pia tuzo ndogo ya Miss Aficionado ambapo alikuwa mshiriki pekee toka Afrika aliyeshinda moja kati ya tuzo hizo 27 zilizowekwa kwenye kundi la Special and Minor Awards.
Kwa Odemba hii ni CHANGAMOTO nyingine baada ya kuwa amepitia maisha ya aina nyingi yenye vikwazo vingi na hatimaye akaweza kuvipita na kurejea katika kile anachokimudu zaidi. Urembo na Mitindo.
Twampongeza kwa kurejea katika kile amuducho na kumsihi kutumia taji hilo kama balozi mwema wa Taifa kutangaza hali ya kimazingira ambayo imekuwa mbiu kuu ya mashindano hayo yanayosemekana kuwa moja kati ya mashindano makubwa zaidi ya ulimbwende kwa idadi ya ushiriki wa nchi na washiriki wake hujihusisha zaidi na masuala ya kimazingira.
Mshindi wa shindano la mwaka huu ni Miss Phillipines Karla Paula Henry ambaye kabla ya kutwaa taji hilo, alishashinda Tuzo za Miss Earth Designers Award na Miss Photogenic.
Hongera Saaana Odemba

Friday, September 26, 2008

Tufunguke Akili? Come On Latoya

Mshiriki Latoya Lyakurwa (kati) akiwa na ma-afisa wa MultiChoice
Picha kwa hisani ya http://www.issamichuzi.blogspot.com/

Katika mahijiano yake na waandishi wa habari ambayo yamechapishwa katika vyombo mbalimbali na pia video yake inapatikana katika tovuti ya Daily News http://dailynews.habarileo.co.tz/streaming/, mshiriki toka Tanzania katika shindano la tatu la Big Brother Afrika Latoya Lyakurwa amewataka wananchi na waTanzania kufunguka akili zao na kutambua kuwa hii ni "new era" ambapo hatuishi kwenye miti na wala hatuvai majani hivyo inatupasa kukubali kile tunachokiona kwenye Televisheni. Akijibu swali la mwandishi aliyemuuliza anaonaje ama juu ya wale wanaosema kuwa Big Brother haiendani na mila na tamaduni za wa-Tanzania na waAfrika? alisema "... mimi nasema watu wafunguke akili. Utandawazi, yani ni kwamba (kicheko) nilikuwa nataka tu niwaambie kwamba yaani wafunguke mawazo yao yaani kwamba sasa hivi hii ni new era, yaani tuko katika maisha mapya hatuishi tena kwenye miti, hatuvai majani, kwa hiyo hata kuangalia vitu kama hivyo kwenye Tv inabidi tu-accept, kwa hiyo it's a new era, kwa hiyo tufungue akili zetu na tujue kwamba huu ni utandawazi"

Vinavyonisumbua hapa ni vitu hivi vichache ambavyo ni
1: Latoya hakujibu swali la kama anakubaliana nao ama la katika suala la kuendana na mfumo wa maisha yetu,
2: Nadhani watu wamefunguka akili saana na ndio maana wakaoanisha kile walichokiona ama wanachokiona kinaendelea kwenye mchezo huo na maisha halisi ya jamii yetu.
3: Utandawazi na "New Era" vina mengi yenye upana wake lakini si kweli kuwa kila kionekanacho kwenye Tv kikubaliwe kwa kuwa tu ni "new era" ndani ya utandawazi
4: Kwa yeye kuona sasa kuwa hatuishi kwenye miti na kula majani hivyo tunastahili ku-accept kila tuonacho kwenye Tv nadhani ni kipimo cha fikra.
Latoya angeweza kuelezea kwa namna nyingine kwa kueleza mabadiliko ya maisha na michakato ya kutafuta pesa, lakini si kusema kuwa wanaofikiria hivyo hawajafunguka akili na kukubaliana na new era na utandawazi. Ule ni mchezo ambao alikuwa na kila haki ya kushiriki kwa kuwa ulikuwa ni utashi, lakini naamini maadili mengi yanavunjwa na huo ni ukweli ambao kwa waujuao wanaweza kuoanisha hilo na swali ambalo kwa namna alivyolijibu kunaleta maswali mawili. Ama Latoya hajui mila na desturi zinazozungumziwa ama hatambui vema suala la utandawazi na new era aliyoizungumza.
Bado naamini kuwa kuna maadili mengi yanayovunjwa katika mila, desturi na imani za wengi na tunalotakiwa kukubali ni kuwa kuangalia ni utashi kama ushiriki, lakini kueleza ukweli hakumaanishi kuwa hujafunguka kiakili ama kuambatana na "new era".

Ni Changamoto tuuuuuu