Showing posts with label Reggae Time. Show all posts
Showing posts with label Reggae Time. Show all posts

Saturday, April 17, 2021

DONDOO NA REGGAE ya Kwanza Radio. Kazi za Lucky Dube

Jambo ambalo bado nawaza kuhusu Lucky Dube ni uwezo wake wa kuwaza kitu ambacho kipo, na ambacho kingeweza kutendeka kwa namna fulani lakini hakikutendeka hivyo japo kinaleta maana halisi ya fikra ya kutendeka kwake. 
Yaani alikuwa na uwezo mkubwa saana wa KUSADIKI habari ama tukio ama maisha halisi kwa namna ambavyo yanaweza KUSADIKIKA. 
Alieleza, kuuliza ama kufafanua utata ama fumbo ama mwenendo fulani wa maisha kwa namna ya kipekee. 
Tunaweza kuangalia baadhi ya nyimbo kuwaza kwa pamoja kuwa ALIWAZA NINI?? 

Tutakujia punde kupitia tovuti yetu www.kwanzaproduction.com 
Kwa sasa unaweza kusikiliza radio kupitia 
Radio Garden 
OnlineRadio Box 

Reggae Time ya Kwanza Radio.. Rastafarianism

Amani, Upendo na Heshima kwako msikilizaji wa Kwanza Radio. Karibu katika kipindi hiki cha Reggae Time, kinachokujia kutoka hapa Kilimanjaro Studios. Na leo, tunagusia mambo kadhaa ambayo ni vema kuyajua kuhusu maRasta. Watu wengi wanaposikia neno RASTAFARI, wanaelekeza fikra zao kwa watu wenye rasta ama dreadlocks, kwa uvutaji wa bangi, kwenye muziki wa Reggae na kadhalika. Lakini, kwa hakika uRasta ni falsafa makini ambayo huchukua mwelekeo mkubwa wa kiImani. Japokuwa wapo wengi ambao hufuata ama kujiita maRasta ili kupata mwanya wa kufanya baadhi ya mambo maovu, ukweli unabaki palepale kuwa wapo wafuasi wazuri wa imani ya uRasta, ambao jamii isiyowajua vema, inawachukulia visivyo. Mubelwa Bandio anakusihi uwe naye pamoja mpaka mwisho. Wewe msikilizaji unaweza kushiriki kwa kutuma ujumbe ama maoni yako kwenye mitandao yetu ya kijamii. Tufuatilie kwenye Facebook, Instagram, Twitter na Soundcloud. Tafuta Kwanza Production.

Reggae Time ya Kwanza Radio. Historia ya muziki wa Reggae

Muziki wa reggae ni mahadhi ambayo ni matokeo ya kutambulika na kuendelezwa kwa aina ama mitindo mingine ya muziki. Licha ya kwamba reggae inatambulika zaidi kutoka katika miziki ya Carribean yenye asili ya Afrika na miziki ya R&B toka Marekani, lakini reggae tunayoisikia sasa ni muendelezo wa midundo ya Rocksteady na Ska kuanzia miaka ya 1960 huko Jamaica. Katika miaka ya 1950, enzi ambazo wakazi wa visiwa vya Carribean walikuwa wapenzi wakubwa wa miondoko ya Calypso na wakati ambao waMarekani walikuwa akipenda zaidi miziki ya wasanii kama Harry Belafonte, wananchi wengi wa Jamaica walikuwa wakisikiliza zaidi miziki ya Rhythm and Blues (R&B) za kiMarekani. Miziki hiyo ilikuwa ikisikika zaidi kutoka miji ya Memphis, New Orleans na Miami na kuwa maarufu sana nchini Jamaica. Wanamuziki wa Jamaica wakachanganya miondoko hiyo ya R&B na miondoko ya Calypso ya Jamaika na kutengeneza muziki mpya wa SKA.

Saturday, September 24, 2016

Kipindi cha Reggae Time, Pride Fm... Sept 24 2016

Kipindi cha REGGAE TIME kutoka Pride Fm Mtwara Tanzania hutayarishwa na kutangazwa na Mubelwa Bandio
Husikika kila Jumamosi kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki
Radio hii yasikika duniani kote kupitia tovuti www.878pridefm.com na kwa walio Marekani na Canada wanaweza kuisikiliza kwa kupiga namba 832 280 0658

Saturday, December 12, 2015

Reggae Time ya PRIDE FM Dec 12 2015.......Uhuru Afrika

Desemba 9, ilikuwa ni siku ya uhuru wa Tanganyika.
Desemba 12, ni uhuru wa Kenya
Katika kipindi hiki, tumeangaza machache juu ya UHURU wa nchi za Afrika na UHURU WA AFRIKA kwa ujumla.
Je! Tuko huru? Tunauenzi uhuru wetu? Na pengine nini kifuate baada ya kutoka kwa wakoloni?
KARIBU tujadili haya kupitia muziki wa Reggae.
Kipindi cha REGGAE TIME kutoka Pride Fm Mtwara Tanzania hutayarishwa na kutangazwa na Mubelwa Bandio.
Husikika kila Jumamosi kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki
Radio hii yasikika duniani kote kupitia tovuti www.878pridefm.com na kwa walio Marekani na Canada wanaweza kuisikiliza kwa kupiga namba 832 280 0658

Saturday, October 3, 2015

Reggae Time ya Pride Fm Oct 3 2015......Siku za maisha yetu

Photo Credits: www.rickey.org

Kipindi cha REGGAE TIME kutoka Pride Fm Mtwara Tanzania hutayarishwa na kutangazwa na Mubelwa Bandio
Husikika kila Jumamosi kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki
Radio hii yasikika duniani kote kupitia tovuti www.878pridefm.com na kwa walio Marekani na Canada wanaweza kuisikiliza kwa kupiga namba 832 280 0658</

Saturday, June 13, 2015

Reggae Time ya Pride FM....Jumamosi June 13, 2015

Mubelwa Bandio na Babu Sikare
Leo ni International Albinism Awareness Day.
Na inaadhimishwa kwa mara ya kwanza tangu UN iitangaze (Nov 18 2014)
Katika sehemu ya kwanza ya kipindi, nimezungumza na Babu Sikare, mwanaharakati mTanzania aishiye hapa USA aliyeshiriki mchakato wa miaka kadhaa kupigania siku hii.

Kipindi cha REGGAE TIME kutoka Pride Fm Mtwara Tanzania hutayarishwa na kutangazwa na Mubelwa Bandio
Husikika kila Jumamosi kuanzia saa tisa kamili alasiri kwa saa za Afrika Mashariki
Radio hii yasikika duniani kote kupitia tovuti www.878pridefm.com na kwa walio Marekani na Canada wanaweza kuisikiliza kwa kupiga namba 832 280 0658
Kama una TuneIn app tafuta Pride Fm ama http://tun.in/seTTx