Saturday, April 17, 2021

Reggae Time ya Kwanza Radio.. Rastafarianism

Amani, Upendo na Heshima kwako msikilizaji wa Kwanza Radio. Karibu katika kipindi hiki cha Reggae Time, kinachokujia kutoka hapa Kilimanjaro Studios. Na leo, tunagusia mambo kadhaa ambayo ni vema kuyajua kuhusu maRasta. Watu wengi wanaposikia neno RASTAFARI, wanaelekeza fikra zao kwa watu wenye rasta ama dreadlocks, kwa uvutaji wa bangi, kwenye muziki wa Reggae na kadhalika. Lakini, kwa hakika uRasta ni falsafa makini ambayo huchukua mwelekeo mkubwa wa kiImani. Japokuwa wapo wengi ambao hufuata ama kujiita maRasta ili kupata mwanya wa kufanya baadhi ya mambo maovu, ukweli unabaki palepale kuwa wapo wafuasi wazuri wa imani ya uRasta, ambao jamii isiyowajua vema, inawachukulia visivyo. Mubelwa Bandio anakusihi uwe naye pamoja mpaka mwisho. Wewe msikilizaji unaweza kushiriki kwa kutuma ujumbe ama maoni yako kwenye mitandao yetu ya kijamii. Tufuatilie kwenye Facebook, Instagram, Twitter na Soundcloud. Tafuta Kwanza Production.

No comments: