Showing posts with label Tanzania yangu. Show all posts
Showing posts with label Tanzania yangu. Show all posts

Monday, October 14, 2013

UJINGA ndani ya busara za UWEPO wa Mwenge

Hiviiiiiiiii.....................
Mmeona picha za MAPOKEZI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ALIYEKWENDA KUZIMA MWENGE kule IRINGA?
Hapa ndipo palipo na UTAMU wa SIASA. Ambao hauna tofauti na TEKNOLOJIA
"MFANANO" wavyo watokana na ukweli kuwa vinatufanya tujihisi tuko karibu ilhali vinatutenganisha zaidi.
Sasa......
Siasa zinasema ziko pale KUTUJENGA
KUENDELEZA UMOJA WETU...
Na katika tukio MUHIMU AMBALO NDIO ISHARA PEKEE YA UMOJA WETU....WATU WANAVAA SARE ZA KUWATENGANISHA KIITIKADI.
NI AIBU
 
 Kwa Tanzania...
MWENGE NDIO KITU PEKEE CHA KITAIFA KINACHOZUNGUKA KOTE KILA MWAKA.
Na natamani kama MWENGE ungekuwa ukitumika kama SANDUKU LA MAONI ambalo (kwa kuzunguka nchi nzima) tungehakikishiwa maoni ya nchi nzima.
Sina tatizo na NIA YA MWENGE, japo NINA TATIZO NA UTEKELEZAJI WA NIA HIYO.
Hii ilitakiwa iwe siku ambayo TUNGEONA NA KUJIVUNIA UMOJA.
Lakini ona mambo tunayojivunia...
NI AIBU KWETU KAMA TAIFA.
Siamini kama hii ni ishara ya kukua kwa demokrasia...ni ishara ya kumomonyoka kwa UMOJA ambako (kwa bahati mbaya) wapo wanaoonekana kufurahia
SHAME ON US!!!!!!! 
I mean, SHAME ON WAO wanaoendekeza mgawanyo wa hivi....
Well...na wale wote wanaojivunia mgawanyiko huo)
Picha kwa hisani ya kurasa za facebook za Maggid Mjengwa na Liberatus Mwang'ombe


Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA
Tuonane "Next Ijayo"

Kwako "Babu". Natamani ungekuwepo ukayaona na kuyasikia ya sasa


Shikamoo Babu.
Natumai kwa sala zetu za wewe kuLALA MAHALI PEMA PEPONI utakuwa huko ukipumzika baada ya mengi uliyotenda.
Sasa nimeamka nikasikiliza wengi "wanavyokuenzi", nikaona mimi nisikwambie haya leo, unasikia mengi na pengine mengi yanakufanya ukereke kwa UNAFIKI unaoendelea. Nimeona nikuandikie ili BAADAE SANA ukishapunguza hasira za hawa wakuenzio kwa kuishi usivyopenda zikiisha, usome ujumbe huu.
Babu....
Nangalia uchumi wa dunia unakoelekea na namna mataifa yanavyochukua umiliki wa uendeshaji wa shughuli muhimu za kiuchumi kisha naishia kujiuliza kama hii si sehemu ama aina mpya ya ujamaa?
Ninasoma MAKALA HII ninapata ka-picha kadoogo kwa mbali kuwa kama Mheshimiwa Baba wa Taifa Mwl Nyerere ungekuwepo, basi ungeweza kurejea kusema mawili matatu ambayo ulishawahi kusema miaka kadhaa iliyopita na ambayo yamekuwa katika hotuba zako na nukuhu zilizopo sehemu mbalimbali.
Nawaza......
Ungekuweo leo hii ungesemaje? Hakuna mwenye jibu sahii lakini kwa kuwa ulishaonya kwenye hotuba zako, ninaloweza kuhisi ni kuwa ungekumbusha kile ulichosema ambacho wengi hawakudhani kuwa kingetimia na ungekuwa wakati wa kudhihirika tena kwa maono yako.
Miaka 14 tangu ututoke, bado unakumbukwa na binafsi natamani ungekuwepo ukanona viongozi wengi wa barani Afrika ambao wanayumbishwa misimamo yao na hata kupindisha ilani zao zilizowapa nafasi ya kuwatumikia wananchi, na kuwa kama hawatambui maslahi ya wananchi wao mpaka WAPANGIWE na mataifa makubwa ambayo baadhi ya viongozi wao hawajui lolote kuhusu nchi hizo.
Natamani ungekuwepo ukaona viongozi wetu wa sasa ambao hawawezi kusimamisha mapigano (hata ya RUSHWA) mpaka watishiwe na mataifa fulani, ama wawekewe vikwazo na fulani.
Si unakumbuka ulivyozungumza kuhusu RUSHWA?
Wengine hawakukusikia, wengine walipuuza, wengine wanafanya kile ambacho sisi huku tunaita "kupotezea"
Ngoja niwakumbushe hiki kisha tuendelee.

Natamani ungekuwepo ukaona viongozi wasiothamini uhai wa wananchi wao kwa kuendeleza vita baina ya wanachi wa nchini mwao mpaka waamriwe kuacha na mataifa ya nje.
Yaani wa kuhimiza kuhusu UCHAPAJI KAZI wamemomonyoka saana. Siku hizi ni MWENDO WA AHADI utadhani wana pesa ya kuibadili nchi.
Hawategemei RASILIMALI WATU. Na wanasahau hata mfano uliowahi kuwapa kipindi kile wa JFK
Najua watanichukia kusikia nawakumbusha, ila........nawakumbusha

Ungekuwepo basi ungeona viongozi wanaotumia mwanya wa elimu na mfumo m'bovu wa utawala kujilimbikizia mali kwa jasho la wahitaji (sio maskini) wengi Barani mwetu.
By the way, hayo ni ya Afrika kwa ujumla, ya nyumbani Tanzania yanasikitisha zaidi. Utayasoma kwingine ukipata nafasi.
Ngoja....
Babu, ni kama vile kila mtu nasaka kufika pale ambapo wewe ulisema ni MZIGO.
Lakini siku hizi wanavyopakimbilia. Naamini uchaguzi wa 2015, tutakuwa na karatasi ya kura yenye maneni P.T.O.
Sijui wanapajua kweli ama wanadhani kwa kuwa watakuwa WATAWALA WAKUU basi watafanya watakalo?
Wakumbushe Babu..Wakumbushe

Kibaya zaidi, ka-mchakato ka kuelekea huko kwenye urais kameanza kunuka uDINI na hata uKABILA.
Yaani...natamani ungekuwepo ukawaambia. Japo nina mashaka kama wangesikiliza. Kwani si ulishawaambia?
Najua kuna wanaobisha, ngoja niwawekee ulilosema

Ni viongozi wachache tunaoweza kujivunia na ambao msimamo wao unaendelea kuonekana kuwa wazi na usioyumbishwa na "viranja" wa dunia. Wengi wanamjua Mandela kama kiongozi hodari, shupavu na jasiri katika Afrika na wengi wanakubaliana na hilo, lakini pia kama alivyosema Mchambuzi na Mwandishi hodari Freddy Macha, kabla ya Mandela alikuwepo Nyerere na ujasiri, uwezo na upeo wako bado unaheshimika miongoni mwa wengi.
Tunakanganywa na hawa uliowaacha ambao HATA SIKU MOJA HAWAJAKIRI WALA KUWAJIBIKA KWA MAKOSA YAO.
Wakikosa wa kumsingizia nchini, watamsinginzia aliye nje. Na sikwambii kitu kipya....si unakumbuka ulipozungumzia kuhusu KODI?
Wewe unakumbuka Babu, wacha niwakumbushe hawa wanaochagua la kusahau (hasa linapowahusu)

KAMA UNAYAONA HAYA NA MENGINE MENGI BASI ENDELEA KUTUOMBEA NA KAMA HUYAONI BASI TWAKWAMBIA YALIYOPO LAKINI KAMA HUTUSIKII, NDIO MAANA TUNAENDELEA KUTAMANI TU KAMA UNGEKUWEPO.
Anyway Babu......
Ulitekeleza sehemu yako na huko uliko PUMZIKA KWA AMANI.

Sunday, September 15, 2013

Tanzania yangu. Ivunayo isipopanda (II)


Alhamis wiki hii nilisoma habari kwenye gazeti la Mwananchi kuhusu Bondia Rashid Matumla ambaye amesema kuwa anapigana ili asife njaa
Katika habari hiyo, Matumla amenukuliwa akisema kuwa “Kila kitu changu hivi sasa kinaniendea kombo, nilifanya biashara ya mahindi huko Tanga imekufa vivyohivyo na ile ya mbao, napigana ulingoni nikiwa mgonjwa ili nipate fedha kwani sina fedha kabisa,” Leo nikasoma kuhusu kupokelewa kwa shwangwe kwa bondia Francis Cheka huko Morogoro. Nikawaza mapokezi ambayo Matumla aliwahi kupata na hadhi ya kutumia "VIP" pale kiwanja cha ndege aliyopewa kutokana na mafanikio yake.
Lakini mwisho wake ndio huu aliousema
Najua nilipata kuandika mengi kuhusu haya.
Kuhusu wasanii na watangazaji walioliletea taifa UZALENDO mkubwa. Waigizaji wa michezo ya radioni ambao walitufanya "tugande" kwenye redio zetu kusikiliza michezo ya kuigiza iliyokuwa na mafunzo ilhali wanapata kipato kidogo sana.
Lakini unapofika wakati wa "kula mbivu", inaonekana kuwa MBIVU HIZO ZINAKUWA ZIMEOZA.
Tumeshuhudia wasanii wakichangishwa pesa kwa matibabu.
Wengine ambao wametumikia taifa kwa zaidi ya nusu karne (kama Mzee Muhidin Maalim anaishia kupata msaada binafsi wa wasanii na wadau wengine kabla Serikali HAIJAKUMBUKA KUTOA "CHETI"
Lakini nimeona nirejee BANDIKO hili la Aug 18, 2009 nililobandika chini ya "kichwa" Tanzania yangu. Ivunayo isipopanda
JIKUMBUSHE

Labda TANZANIA YANGU ni jina limaanishalo SERIKALI. Ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikijitokeza kupongeza na kuonekana pale penye mafanikio na "kuwa likizo" kwenye matatizo. Ni kweli. Binafsi nilishangaa kuona watu wanashangaa kumuona Naibu Waziri wa michezo kaenda kumpokea Hasheem Thabeet uwanja wa ndege. Wapo waliohoji umuhimu wa Thabeet na wapo waliohoji majukumu ya Naibu Waziri. Kwa ujumla kila mtu alikuwa na lake la kueleza japo kwangu si kila mtu alikuwa na maana katika kutetea hoja yake. Lazima tukubali kuwa Hasheem amekuwa mtanzania wa kwanza kupata nafasi ya kucheza katika ligi ya Taifa ya mpira wa kikapu hapa Marekani NBA na ni lazima apate "attention" toka nyumbani na hasa katika safari yake ya kwanza kurejea tangu ajiunge na Memphis Grizzlies. Na si ajabu kwa SERIKALI kujibaraguza pembeni yake na kuonesha (kama) inajali ilhali tunajua mchango wao katika kufanikisha safari za wengi wenye nia ya kuwa kama Hasheem. Si jambo la kushangaza hata kidogo kwa sisi tunaofuatilia habari za michezo kwa muda mrefu. Hamkumbuki namna ambavyo WAZIRI MKUU alisherehekea ushindi wa Rashid "snake Boy" Matumla wakati ule akiwa kwenye kilele cha uchezaji wake? Matumla akapewa na "pass" ya VIP uwanja wa ndege na sasa sina hakika kama kuna kiongozi anayekumbuka aliko. Sina tatizo na mapokezi na sina tatizo na namna ambavyo viongozi wa serikali wanajitoa kuwapongeza wachezaji na watu mbalimbali wenye kuonesha kufika kilele cha mafanikio yao. KINACHONICHEFUA ni namna ambavyo SERIKALI inakurupuka na kuandaa mapokezi na dhifa na sherehe na hotuba za kuwapongeza wenzetu wanaofanya vema ilhali inapuuza mazingira yanayowawezesha kufika walipo.
Hatukusikia SERIKALI ikijihusisha na maandalizi ya Rashid Matumla ila tukamuona Waziri Mkuu Sumaye akimnyanyua mkono kwa mbwembwe zoote na bendera kuubwa. Hatukusikia serikali ikimsaidia Thabeet (alipokuwa akisaka njia ya kumfikisha alipo) kufikia ndoto zake lakini leo hii, lakini sasa hivi mpaka Rais anamuandalia chakula kumpongeza.
Sijui kwa wasomaji wangu, lakini nimechoshwa na siasa katika maisha ya watu (hasa ambapo hazistahili). SERIKALI ilistahili kushikwa aibu kwa mafanikio BINAFSI yaonekanayo miongoni mwa watu wake na ilistahili kujua ni wapi pa kuanzia kuwekeza. Inaoshindwa kuwahudumia wananchi wake kwenye shida, isijitokeze kwenye raha.
WATU WAMELIA SAANA KUHUSU WIZI UNAOENDELEA AIRPORT LAKINI HAJATUMWA MWAKILISHI NA SASA ANAKUJA NYOTA TUNAMUONA. Kwanini tusikae chini na kupanga program nzuri itakayowawezesha wale wengi wenye ndoto kama za hawa tuwapongezao kuzifikia? Haihitaji akili za ziada kujua hili. Najiuliza meengi kuhusu TANZANIA YANGU. Ni kwanini haiwekezi katika kupata itakayo? Labda niwakumbushe swali alilouliza Freddie McGregor alipowauliza viongozi kuwa "why dont you set the program, so the youth can work and survive. So that they can better themselves and show some progress in their life, teach the youth the positive things and make them realize, no shooting, no looting, bring back the LOVING and where did we go wrong? Msikilize hapa chini
 
Picha: Kutoka kwa Michuzi & Darhotwire

Monday, August 12, 2013

Tanzania yangu.....Yenye wasanii walio makini "kupanda chini"

Photo Credits: Reverbnation.com
Nikiwa mwanachuo katika Kituo cha Mafunzo ya Ufundi na Huduma (VTSC) chini ya VETA mjini Dodoma, tulikuwa na somo la UJASIRIAMALI.
Na licha ya kwamba miongoni mwetu hatukuonekana kuvutiwa ama kulipenda na / hata kutilia maanani yaliyofunzwa katika kipindi hicho, kuna jambo ambalo tangu lilipotambulishwa kichwani mwangu na Mwalimu wangu Mr. Lawrence Mashindano, limeendelea kuwa MSINGI wa maamuzi mengi nitendayo.
Na ni jambo ambalo sio tu limeonekana kufaa kwenye UJASIRIAMALI, bali katika mfumo mzima wa maisha. Kuanzia mahusiano mpaka maongezi.
Ni kama vile lolote linalohusisha KUFANYA MAAMUZI limehusisha jambo hili.
Nalo ni HATUA TANO katika ujasiriamali (mimi ntaita hatua tano za maamuzi) ambazo ni O.I.G.I.R
Observe the environment
Identify opportunities
Gather necessary resources
Implement activities
Rip rewards.
Kwangu, hatua hizi tano nimezitumia hata katika kuamua lile la kusema na kuandika pia.
Sasa..........
Nirejee kwenye POST yangu ya leo.
Nimekuwa nikifuatilia mahojiano ya wasanii mbalimbali wa Tanzania na nimeishia kuwaza kama nao wanachukulia kazi yao kama UJASIRIAMALI na kama ndivyo, nawaza kama wanaijua hata hadhira yao.
Yaani kuna wakati (katika hali ya kushangaza kabisa) unasikia msanii ambaye anajua fika kuwa HANA HADHIRA YA KIMATAIFA, anawasiliana na hadhira yake kwa lugha ambayo wengi wa wamsikilizao hawaielewi kwa ufasaha ama hawaitumii kila wakati.
Lakini pia, achilia mbali kuelewa na kuitumia lugha hiyo kwa hadhira yake, bado kuna jambo jingine la msanii mwenyewe kutoimudu lugha hiyo.
Limekuwa kama WIMBI la mahojiano kuhusisha majibu mengi ya kiingereza hata pale msanii anapoulizwa kwa kiSwahili, na hili limenifanya niwaze iwapo MTAZAMO wa wasanii hawa ni kuwa "kwa kujibu kwa kiingereza wanakuwa wamedhihirisha ubora ama ukomavu fulani maishani"?
Kibaya zaidi ni pale wanaposhindwa kueleweka kwa wanaojua kiingereza, wakashindwa kueleweka hata kwa wale wateja halisi wao (ambao si wote wanaielewa lugha hiyo)
Karika ukurasa wangu wa Facebook nilipata kuuliza kuwa ni msanii gani ambaye anapohijiwa kwa kiswahili hujibu kwa kiSwahili bila kuchanganya na kiingereza?
Wengi (wa walioona na kujibu) wakamtaja Diamond.
Sina hakika na uhusiano wa hili na UMAARUFU WAKE, lakini kuna ukweli kuwa ASILIMIA KUBWA YA WASANII WETU WENGI HAWAJULIKANI AMA KUTAMBULIKA KWA KILE WANACHOSEMA (kwa kuwa hawana mafunzo ya kuzungumza), BALI KWA HABARI ZA UDAKU NA KASHFA MBALIMBALI
KUMBUKA....NIMESEMA WENGI. SI WOTE
Wapo wachache ambao wanaendeleza utamaduni wa kuwasiliana vema na hadhira yao, kwa lugha ielewekayo kwao na kufikisha ujumbe wao kwa wadau wao.
Na kwa kufanya hivyo, wanajikuta waki"connect" vema na hadhira yao

Kumbuka.....Mzee Nelson Mandela alipata kusema kuwa "If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart."
Kwa tafsiri isiyo rasmi anasema, ukiongea na mtu kwa lugha anayoielewa, yale usemayo yatamkaa kichwani. Ukiongea naye kwa lugha yake, yale usemayo yataelekea moyoni mwake
Ina maana....wasanii wetu waongee na wadau wao kwa LUGHA YA KWAO, ili yale wayanenayo, yawakae mioyoni na sio vichwani.
Wale wanaojitahidi kuwasiliana na wananchi kwa namna inayowa"boa", hawana tofauti na yule anayejitahidi "kukwea chini"


Ni mtazamo wangu tu kwa namna nionavyo tatizo.
Labda namna nionavyo tatizo ndilo tatizo 

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA
Tuonane "Next Ijayo"

Wednesday, July 31, 2013

Tanzania yangu....Isiyoendelea kwa kukosa viongozi "wanaoendekeza ujinga"

ONYO: REJEA KUSOMA KICHWA CHA BANDIKO HILI NA UHAKIKISHE UMEELEWA KABLA HUJAENDELEA NA BANDIKO HILI
Dunia ya sasa inaonekana kwenda kwa kasi
Yaani.....
Kasi (pengine) kuliko uwezo wa baadhi ya watu na mazingira KUAMBATANA na kasi hiyo.
Ni katika hilo, tunakuta baadhi ya mazingira (nchi yangu ikiwemo) ikishindwa kupitia hatua zote zinazostahili kupitiwa kuweza KUSONGA MBELE na mabadiliko hayo.
Matokeo yake ni kuwa watu wanaruka baadhi ya hatua na wanashindwa kuwa na ukamilifu wa pale walipo.
Hivi sasa, kile kinachoonekana kama UJANJA nchini mwangu ndicho kinachonisikitisha
Na ni hicho kinachonifanya niamini kuwa BILA TAFSIRI HALISI YA UZALENDO, basi hiki kionekanacho kama UJANJA kitatupeleka pabaya.
Na ndio maana niliandika kwenye ukurasa wangu wa Facebook kuwa
"Kwa kuwa nchi yetu imejaa WAJANJA.
Na......
Kwa kuwa kuongoza nchi ya wajanja KIJANJA hakutuletei maendeleo,
Mimi nadhani .....
Tujaribu UJINGA"

Nililomaanisha ni kuwa, kutokana na KUKIMBIZA MAENDELEO KULIKO MWENDO WAKE NA KUPUUZA HATUA ZA KUYAFUATA, nchi yetu imejikuta ikitafsiri MAENDELEO na UJANJA kama vitu ambavyo ni matokeo ya njia za mkato kujibufaisha.
Leo hii, mtu anayekwepa kodi anaonekana MJANJA.
Leo hii, mtu anayepokea rushwa na kunufaika bila kukamatwa anaonekana MJANJA
Leo hii, mtu anayetajirika haraka hata kwa kuvunja miiko ya kazi anaonekana MJANJA
Leo hii, mtu anayepokea mishahara ya wafu wizarani anaonekana MJANJA
Na mengine mabaya ambayo ni NJIA ZA MKATO NA ZISIZO HALALI ambazo zinamnufaisha zinahesabiwa kuwa UJANJA
Na kwa hakika
Anayelipa kodi anavyotakiwa, anaonekana MJINGA
Anayefuata sheria katika atendayo anaonekana MJINGA
Anayehimiza HAKI kwa wote anaonekana MJINGA
Anayekataa rushwa hivi sasa anaonekana MJINGA
Anayeonekana kuwajali wananchi anaonekana MJINGA
Yaani, mfumo mzima unaomfanya mtu kutwaa madaraka, umeandamwa na watu ambao fikra zao ziko kwenye KISASI cha kujilimbikizia kama ambavyo walilimbikiza waliotangulia na kumnyima yeye FURSA SAWA aliyohitaji ama kustahili kuwa nayo.
TUNAKUWA KWENYE MAUMIVU
Maumivu ambayo sasa hayatokani na NJAA, bali ni maumivu yanayosababishwa na KUVIMBIWA kutokana na yule mwenye njaa kula kupitiliza na kusababisha maumivu ya UPANDE WA PILI wa kile kilichoonekana kuwa SULUHISHO.
Tatizo linalotukabili si la WATU, bali ni namna tunavyowapata watu hao na kuwadhaminisha madaraka.
Niliandika
"Sasa hivi hata nchi yangu Tanzania iongozwe na Masia na Mtume, iwapo MFUMO UTAKAOTUMIKA NI HUU ULIOPO, bado upande pekee wa maendeleo tutakaoelekea ni wa MAENDELEO HASI.
Tatizo la Tanzania si watu walio madarakani, bali ni MFUMO unaowaweka pale, unaowaongoza katika kuongoza na unaowawajibisha."

Januari 7, 2009 niliandika POST HII yenye kichwa DIKTETA NI NANI NA KWANINI TWAMHITAJI
Na humo, nikaandika
"Najua akitokea mtu akalazimisha baadhi ya mambo ya maana kutendeka nyumbani basi ataitwa dikteta (na kwa bahati mbaya nasi tutashabikia hata kama si tafsiri yetu).
Najiuliza akitokea "kiongozi" akalazimisha kusimamishwa kwa mikataba yote ya madini ili ipitiwe upya hataonekana dikteta?
Je atakayelazimisha viongozi wakuu waliosababisha mabilioni ya hasara serikalini wachunguzwe licha ya katiba waliyoshindwa kuitii kutosema hivyo hataonekana dikteta?
Je atakayelazimisha wabunge kujenga ofisi na kutumia muda mwingi majimboni mwao kama walivyoahidi wakati wa kampeni hataonekana dikteta?
Atakayelazimisha utendaji wa mikoa kulingana na rasilimali zake kuwanufaisha wananchi wake na kisha nchi nzima huyo hataonekana dikteta?
Najua kuwa atakayewafikisha viongozi wakuu mahabusu ataitwa dikteta kwa kuwa amekwenda kinyume cha katiba, lakini sijui kwa nini katiba imlinde yule ambaye ameivunja kujilimbikizia mali na kuitia serikali hasara kubwa?
Kama huyu atakayetenda haya niliyosema hapo juu, atakayevunja mikataba ya ujenzi wa miundombinu yenye utata, atakayehakikisha ahadi za wananchi zinatekelezwa na waahidi hasa wabunge, atakayeshurutisha matumizi mazuri ya rasilimali za wananchi kwa manufaa ya sehemu husika, atakayeshinikiza malipo kwa wafanyakazi ambayo mpaka sasa haijajulikana kwanini hawajalipwa ilhali waheshimiwa wanapata pesa zao bila malimbikizo, atakayehakikisha kuwa mkulima wa anapata senti zake zote alizoikopesha serikali na ambazo anatumia pesa nyingi kufuatilia kuliko atakazolipwa, atakayesimamisha ziara za nje na ndani za viongozi (zisizo za lazima) na atakayeamua Tanzania iwe ya manufaa kwa wa Tanzania kwa kutumia kila kilichopo Tanzania ataitwa DIKTETA, basi namuombea awepo."


NI KWA KUWA HUYU ATAKUWA DIKTETA KWA KUTEKELEZA MEMA AMBAYO WASIO WEMA WATAUONA KAMA UJINGA 

Narejea...
Kwa kuwa VIONGOZI WETU WANATOKA KWENYE JAMII, NA NI JAMII INAYOTAFSIRI MEMA KUWA "UJINGA", BASI NI MPAKA TUTAKAPOPATA VIONGOZI WANAOENDEKEZA "UJINGA", NCHI YETU HAITAENDELEA.

Mungu Ibariki Tanzania.

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA
Tuonane "Next Ijayo"

Monday, July 1, 2013

Tanzania yangu....Na mkono "usioaminika" ndani ya KOPO LA HAZINA


Tanzania yangu ni kati ya nchi ambazo tunaweza kusema kuwa zinajenga mahusiano makubwa na hai na nchi ya Marekani.
Tukumbuke kuwa marais watatu waliopita wa Marekani wameitembelea Tanzania wakiwa madarakani.
 Na hivi sasa, kuna ujio wa Rais Barack Obama nchini Tanzania ikiwa ni kama "majibu" ya ziara ya Rais Xi Jinping wa China aliyeitembelea Tanzania kama nchi ya kwanza katika nchi tatu alizotembelea ikiwa ni siku 10 tu tangu aingie madarakani. Na akiwa nchini Tanzania, Rais Jinping alisaini mikataba 16 inayohusu Biashara, Utamaduni na diplomasia.
Kwa mujibu wa CNN, kuna wafanyabiashara wa kiChina zaidi ya 8,000  nchini Tanzania ambao wanajishughulisha na biashara mbalimbali kuanzia magenge (kiosk) mpaka makampuni makubwa ya kandarasi.
Na sasa, Rais Obama amekwenda Tanzania kwenda kuhamasisha mahusiano ya kibiashara baina ya nchi hizi mbili.
Lakini kubwa zaidi, Rais Obama amekwenda Afrika akiwa na lengo kubwa la kuhimiza mkakati wa kuongeza nishati kwa bara hili ambalo licha ya harakati za kusaka maendeleo, ni theluthi moja tu ya wakazi wake wenye nishati ya umeme.
Katika mpango huo, Obama aliyeambatana na wafanyabiashara wa Marekani anahimiza uwekezaji (na sio msaada) ambao utawanufaisha wafanyabiashara hao na waAfrika kwa ujumla.
Lakini kama alivyosema Jonathan Berman alipohojiwa na NPR, wafanyabiashara wengi wa Marekani wanasita kuwekeza barani Afrika kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo MIUNDOMBINU, UTAWALA WA KISHERIA, NA MAZINGIRA YA BIASHARA HAYAJARASMISHWA
Na hilo ndilo hasa ninalotaka kuzungumzia hii leo.
TANZANIA YANGU ina nafasi kubwa ya kufanikiwa katika biashara iwapo ITAAMUA KUWAJIBIKA NA KUTUMIA VEMA USHINDANI WA UWEKEZAJI UNAOFANYWA NA NCHI HIZI MBILI kubwa.
 Ushindani huu wa uwekezaji nchini mwetu unaweza kuwa BARAKA iwapo tutakuwa na wazalendo katika nafasi za kusimamia uwekezaji huu, lakini pia utakuwa LAANA iwapo wale wenye mamlaka wataamua kujinufaisha.
Kichwa cha "bandiko" hili kinasomeka "Tanzania yangu....Na mkono "usioaminika" ndani ya KOPO LA HAZINA" si kwa kuwa ninapenda kuwa mtazamo hasi kuhusu hili, bali kwa kuwa TUNA HISTORIA YA KUTOTUMIA VEMA HAZINA TULIZONAZO.
Tuna historia ya kutowajibisha wale waliotuletea HASARA
Tuna historia ya kutoona mianya ya mafanikio na maendeleo iliyo mbele yetu
Leo hii, TANZANIA INATAJWA KAMA NCHI YENYE HAZINA KUBWA YA NISHATI na hilo pekee linaweza kuwa MKOMBOZI WA MWANANCHI
Lakini hili si la uongozi tu.
WANANCHI NI LAZIMA WAKUBALI KUTHUBUTU, WAKUBALI KUFUATA SHERIA NA KUJARIBU KILICHO CHA TOFAUTI.
Licha ya matatizo ya uongozi, bado wananchi tumekuwa WAZEMBE na wenye kupenda NJIA ZA MKATO katika harakati za kuelekea mafanikio ya nchi yetu.
Hii ni nafasi kubwa kwetu waTanzania kusonga mbele.
UKWELI NI KUWA, kopo hili la HAZINA (uwekezaji) liko mbele yetu, na ni sisi tusioaminiana katika "mkono unaotumbukizwa humo" kujua kilichomo.
Tuliyaona Angola.
Tunayaona Kongo.
Hatutaki kuyaona Tanzania.
HAZINA IWE BARAKA NA SI LAANA.
Katika kumalizia "bandiko hili", narejea ONYO alilotoa Rais Obama katika HOTUBA KUU KUHUSU ZIARA YAKE BARANI AFRIKA katika Chuo Kikuu cha Cape Town kuhusu WAJIBU WA SERIKALI KUFANYA KILA IFANYALO KWA MANUFAA YA WANANCHI akisema "History tells us that true progress is only possible where governments exist to serve their people, and not the other way around."
Na naamini historia ya nchi yetu itadhihirisha ukweli huu kutokana na yale yanayoendelea katika sekta ya uwekezaji.

Mungu Ibariki Tanzania.

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA

Tuonane "Next Ijayo"

Wednesday, May 22, 2013

Tanzania Yangu.....Inayotunza "ubongo wa digitali" ndani ya "fuvu la analogia"

Photo Credits: Cafepress.com
Dunia ya sasa imefikia wakati ambao ni vigumu saana kudhibiti usambaaji wa habari popote na kwa yeyote.
Sasa hivi, ni kama DUNIA IKO VIGANJANI MWA WANANCHI hata walio mbali na "makao makuu" ya taarifa mbalimbali.
Walio vijijini wanajua kinachoendelea upande wa pili wa dunia bila kufika huko. Ni kwa kuwa simu za "nununu" zinauweka ulimwengu mikononi mwao muda wowote.
Kwa maana nyingine, NI NGUMU KUPUMBAZA walio kwako kwa kuwa wanapata zaidi ya kitokacho kwako.
Nirejee kwa viongozi wetu....
Utawasikia viongozi wakisema "msifananishe hilo la Marekani na hapa Tanzania kwa kuwa wao (Marekani) wamekuwa huru kwa miaka 200 wakati sisi tumekuwa huru kwa miaka 50 tu"
Lakini...wanapopata pesa za kununua MASHANGINGI, hawanunui ambayo Marekani walitumia wakati wa miaka 50 ya uhuru wao
Wanalazimisha watu kuishi maisha ambayo hayaendani na wakati  (katika yale yanayohusu uwajibikaji wao) na kupuuza hilohilo katika yale yahusuyo wananchi.
Kumekuwa na ile DHANA YA KUTAWALA WANANCHI KWA UKOSEFU WA TAARIFA SAHIHI KWAO (wananchi) na hilo linaanza kuwa kikwazo kwa watawala hao kwa kuwa wananchi wanapata habari toka vyanzo mbalimbali duniani (japo wakati mwingine hili linakuwa na madhara makubwa)
Yaani tuna viongozi wanaoamini kuwa wanaweza kuwazuia wananchi wanaoishi na kuwa katika mfumo wa kiDIGITALI kuenenda sawa na "dunia iliyo viganjani mwao" kwa mbinu zao za kiANALOGIA ambazo zinahusisha NGUVU KULIKO TAARIFA ZINAZOKOSEKANA NA KUHITAJIWA NA WANANCHI.
Kumekuwa na tatizo la TAARIFA kwa wananchi kutoka serikalini mwetu na blogu hii imekuwa ikililalamikia sana.
Kinachoonekana ni kuwa WANANCHI WANALAMIMIKIA MAMBO AMBAYO WENYE UFAHAMU NAYO WANAWAONA KAMA VITUKO na hii ni kwa kuwa wananchi wengi hawapati taarifa kamili ya kile kinachoendelea ilhali wenye taarifa kamili wameKAA NAZO.
Sasa tunaona maafa ya wananchi kuchukua hatua wanapohisi wanapuuzwa, ilhali maamuzi yanakuwa yameshafanywa na walitakiwa kujulishwa.
WANAJIONA WANAPUUZWA.
Labda niwakumbushe WATAWALA wetu kuwa katika ulimwengu wa sasa, huwezi kuwafunga wananchi kujua kinachoendelea duniani kwa kuwa DUNIA YA SASA NA UKUBWA WAKE IKO VIGANJANI MWA WATU
Watawala wetu wamewekeza katika "kujenga UKUTA wakiamini itaweza kuzuia HARUFU".
Wanashindwa kuripoti uhalisia wa mambo yanayotokea wakiamini watu hawatapata taarifa kamili na watu wanapogundua kinachoendelea wanahisi KUPUUZWA na / ama kudharauliwa.
Ukweli ni kuwa, ulimwengu wa sasa si wa kutawala watu kwa mabavu na kupuuza nguvu ya mawasiliano ya kiDIGITALI yaliyo kila mahali kwa kutumia njia / mbinu za kiANALOGIA.
Ni LAZIMA WATAWALA WAKUBALI kuwa wanaongoza watu ambao tayari wamesonga mbele kifikra. Na hivyo ni busara nao kusonga nao vivyo hivyo.
Kwa tafsiri yangu, FUVU ndilo linalokinga ubongo.
Na sasa wanaotukinga waTanzania ni VIONGOZI ambao hawataki kuendana na mazingira ya sasa ya dunia.
Yaani....
Yawezekana hata sasa wapo viongozi wanaoshangaa kuona kuna VIONGOZI "WAZEE" wenye akaunti kwenye social media bila kutambua kuwa kwa kufanya hivyo WANAJIFUNZA kile ambacho wananchi wanakijua kwa usahihi ama kinyume chake na kwa kutambua TATIZO, inakuwa rahisi kulikabili.

Tunajua kuwa maandamano na vurugu zilizosababisha mapinduzi makubwa katika nchi kama MISRI na LIBYA hayakuandaliwa kwa mikutano ya hadhara, bali mitandao ya kijamii, hivyo kujua nini wanaelewa na wanaamini ni njia gani ya kutatua matatizo yao, kunaweza kukufanya ukajipanga vema KUWAELEWESHA WASICHOELEWA NA KUWASAIDIA KUTAFUTA NJIA M'BADALA NA YA THAMANI KATIKA KUSAKA HAKI YAO
Ina maana.....

UBONGO (wananchi) umeshafikia kiwango cha DIGITALI cha kupata karibu kila wanalotaka kwenye mtandao, na kusaidiwa kuamua watakavyo kwa kujisomea kupitia mitandao, lakini maFUVU yetu (viongozi) bado yanaamini katika MIKUTANO YA HADHARA ambayo kwa bahati mbaya haina mvuto, haikusanyi watu wengi na haifanyiki kwa wakati muafaka wala kuwafikia kwa haraka kama habari za mitandaoni.
NAAMINI (viongozi) WANGEANZA KWA KUSAMBAZA HABARI SAHIHI KWA NAMNA NA MWENDO ULEULE AMBAO HABARI ZISIZO SAHIHI ZINASAMBAA ILI KUHAKIKISHA KUWA WANA-MATCH MWENDOKASI WA UTOAJI WA TAARIFA AMBAO "UBONGO" (wananchi) WANAO

UKWELI NI KUWA....
Viongozi wetu wanastahili kuji-update katika fikra na kauli zao ili kujua namna ya kuenenda na kasi ya mabadiliko ya teknolojia yanayowawezesha wananchi kujua kinachoendelea duniani kote pale yanapotokea. 
Lakini hii ndio Tanzania yangu....Inayotunza "ubongo wa digitali" ndani ya "fuvu la analogia"



Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA
Tuonane "Next Ijayo"

Tuesday, May 14, 2013

 Chonde Chonde Mhe. Makalla...Kabla hujawaketisha Ruge na Jay Dee

Photo Credits: Vijimambo Blog
 Moja kati ya habari ambazo zimesambaa wiki iliyopita, ni HII ya Naibu Waziri wa Habari Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makalaambaye amenukuliwa "kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee"
  Hili ni JAMBO JEMA na la kupongezwa kwa kuwa hakuna ambaye anapenda kuona MZOZO HUU ambao kwa hakika wengi wanauona USIO WA MAANA KWA JAMII YETU ukiendelea kutawala vyombo vya habari na kuweka kando masuala muhimu ambayo yangeweza kuanzisha mijadala chanya kwenye jamii yetu.
Lakini...
Pamoja na PONGEZI zangu katika kuondoa hili, napenda kuleta OMBI / TAHADHARI kwa Naibu Waziri kuhakikisha kuwa ANATATUA CHANZO CHA TATIZO HILI PAMOJA NA YALE YAFANANAYO NA HILI badala ya kujikita kwa RUGE na LADY JAY DEE.
Ninalomaanisha ni kuwa aangalie kinachosababisha watu wamuunge mkono Lady Jay Dee na wengine wamuunge mkono Ruge japo wote wanapingana na ni katika KAZI MOJA (muziki)
CHONDE CHONDE Mhe Makalla, kabla hujakutana na WAPENDWA HAWA (wachukianao), naomba ufanye uchunguzi kujua kile ambacho kiko nyuma ya kinachosikika na kusomeka kwenye mitandao.
Kwa yeyote mwenye akili timamu, atatambua kuwa KINACHOLALAMIKIWA NI ZAIDI YA KINACHOSEMWA.
Kumekua na matatizo katika fani nzima ya muziki nchini Tanzania. Na sehemu ya matatizo haya inatokana na serikali yetu.
Oktoba 12, 2008 niliandika hapa kuhusu Wasanii kama "chombo cha starehe" cha serikali na kati ya niliyoeleza ni kuwa
"Pengine kubwa na lenye kuonesha "kuthamini burudani" ya wasanii wa nyumbani ni pale wanapoalikwa kwenda kuwatumbuiza waheshimiwa wabunge ambao kwa miaka nenda rudi wameshindwa kuweka sheria ambazo zingelinda haki na mapato yao.
Najua Waheshimiwa wabunge na wenye mamlaka wana-enjoy saana sanaa ioneshwayo na wasanii wetu, lakini kama wanaishia kuwalipa pesa ya onesho (kama hayo ya bungeni) ama kuwapigia makofi na pesa ya onesho la airport, ama kama ni suala la mkataba wa kupiga kampeni na ama propaganda za wasanii, basi napenda watambue kuwa "kwa mujibu wa tafsiri niliyopewa na mwalimu wangu ninayemuamini, nao wanawatumia wasanii kama chombo cha starehe".
Hivi si wakati wa kuweka sheria kali kwa wale wanaosambaza kazi za wasanii? Si wakati wa kupitia vyema hakimiliki na unyonyaji ufanywao kwa wasanii na watu wachache kujinufaisha kwa jasho la wasanii? Ni kweli kuwa viongozi serikalini hawayaoni haya ama hayana "sound" ya kisiasa? Nachukia kila ninapoona "politrix" inaingilia uhalisia wa maisha na kuweka pembeni suluhisho linaloweza kumnyanyua msanii, familia na taifa kwa ujumla.
Lakini pia lawama hizi ama haya yote yatokeayo yana mkono wa wasanii wenyewe. Kutokuwa na umoja miongoni mwao, kuendekeza njaa na majungu baina ya baadhi yao na kutokuwa na elimu na utawala wa KAZI YA SANAA kunawafanya wagawanywe na kutumika bila wao kujijua. Kutokuwa na hesabu kamili na halisi za namna ya kugharimisha muda na kazi zao kulingana na hali ya maisha ya sasa ukizingatia kuwa ndio kazi yao wategemeayo kwa maisha ya sasa na uwekezaji wa maisha yajayo...."

 Na ukweli wa hili la UMOJA na KUENDEKEZA NJAA linadhihirika zaidi sasa ambapo katika MGAWANYIKO uliopo sasa, hakuna wanaojitokeza wazi kuunga ama kupinga kinachosemwa na yeyote kati ya Ruge na JayDee.
UKWELI NI KUWA.....

Kati ya hawa washutumianao (hasa katika hili la kazi za muziki), mmoja kati yao alistahili kuwa "MKWELI KWA KILA MSANII" ambaye (kulingana na msimamo na mahusiano yake kikazi) anauona UKWELI toka upande wake wa maisha.
Lakini mpaka sasa tumesikia WACHACHE sana wakizungumzia hili, kama vile lizungumzwalo haliathiri kazi na / ama fani yao.
Ina maana TATIZO LAWEZA KUWA KWANINI HAWAJASEMA NA WAKISEMA NI NINI KITAWAKUTA?
CHONDE CHONDE Mhe MAKALLA.....KABLA HUJAWAKETISHA RUGE NA JAY DEE, tafuta sababu za ukimya uliopo sasa juu ya hili linaloathiri maisha ya wasanii wengi.
Kama ni kweli kuwa asemalo Lady Jay Dee ni "uzushi", basi tuangalie namna ambavyo wasanii wanaweza kutambua wajibu wao katika jamii na kisha kuwajibishwa kwa kusema kisicho sahihi.
Kama ni kweli kuwa asemalo Ruge ni "uzushi", basi tuangalie namna ambavyo vyombo binafsi vya habari ambavyo pia ni wadau wakuu wa ajira za wasanii vinaweza kuwajibishwa pale vinapotenda yasiyo haki kwenye kazi za wasanii.

Na huu ni MTAZAMO wangu kwa namna ninavyoona tatizo.
Labda....namna nionavyo tatizo ndio tatizo

Monday, May 6, 2013

Kuhusu mlipuko wa Arusha....NAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA

Najivunia saana nchi yangu TANZANIA.
Najivunia na kupongeza HATUA ALIZOCHUKUA MHE. RAIS JAKAYA KIKWETE katika mlipuko wa Arusha.
Nawapa pole sana walioathirika na NAOMBA AMANI, UMOJA NA MSHIKAMANO vitawale katika kipindi hiki kigumu.

KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA KATIKA KANISA KATOLIKI LA YOSEFU MFANYAKAZI PAROKIA TEULE YA OLASITI, ARUSHA MJINI, TAREHE 5 MEI, 2013.


Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa Kanuni ya 49 (1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, naomba kuwasilisha Taarifa yaawali kuhusu tukio la mlipuko uliotokea katika Kanisa Katoliki la MtakatifuJoseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013 saa4:30 asubuhi.

Mheshimiwa Spika,
mnamo tarehe 5 Mei, 2013 saa 4:30 asubuhikulitokea mlipuko katika kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Parokia ya Olasiti, jijini Arusha. Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada yakuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia. Mgeni Rasmi katika uzinduzialikuwa ni Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, AskofuFransisco Mantecillo Padilla. Aidha, alikuwapo mwenyeji wake AskofuJosephati Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Katika uzinduzi huoinakadiriwa kuwa kulikuwa na zaidi ya watu 2000. Wakati Mgeni Rasmiakiwa ametoka nje ya Kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara yauzinduzi mtu alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi kuelekea eneo kulipokuwa na mkusanyiko wa watu ambapo baada ya kutua kulitokeakishindo na mlipuko mkubwa. Mlipuko huo ulisababisha taharuki miongonimwa waumini na kusababisha watu kukimbia ovyo.

Mheshimiwa Spika,
katika tukio hilo watu wawili wamefariki duniaambapo REGINA LONGINO KURUSEI, Mwarusha, umri wa miaka 45, mkaziwa Olasiti alifariki dunia siku ya tukio wakati akipatiwa matibabu katikaHospitali ya Mount Meru na majeruhi mwingine JAMES GABRIEL umri wamiaka 16 amefariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 6 Mei, 2013. Aidha, watu 59 wamejeruhiwa na watatu kati yao ni mahututi. Majeruhi 38walikimbizwa hospitali ya Mount Meru kupatiwa matibabu. Majeruhi 16walikimbizwa hospitali ya St. Elizabeth kwa Father Babu, majeruhi mmojaalipelekwa hospitali ya Selian na majeruhi mwingine alipelekwa katikahospitali ya Dkt. Wanjara, Mianzini. Natumia fursa hii kutoa pole kwawafiwa, uongozi wa kanisa Katoliki, wakazi wa Arusha na Watanzania wotekwa tukio hili la kinyama. Aidha, nawaombea majeruhi wote wa tukio hilowapone haraka.

Mheshimiwa Spika,
Viongozi wa dini na Serikali waliohudhuria ibada hiyohawakupata madhara yeyote kufuatia mlipuko huo. Baada ya Jeshi la PolisiMkoa wa Arusha kupokea taarifa ya tukio hilo waliimarisha ulinzi kwakuongeza idadi ya askari katika eneo hilo. Aidha, Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha MheshimiwaMagesa Mulongo walifika eneo la tukio na kufanya tathimini ya hali ilivyona kuelekeza hatua za kuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika,
kutokana na uzito wa tukio hilo, kitaifa na kimataifa,Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Naibu Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Pereira A. Silima, na InspektaJenerali wa Polisi, Said A. Mwema walikwenda Arusha na walitembeleaeneo la tukio, waliwatembelea majeruhi na kuelekeza hatua za ziada zakuchukuliwa.

Mheshimiwa Spika,
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mlipuko huoni bomu. Uchunguzi wa kubaini aina ya bomu lililotumika unaendeleakufanywa na Jeshi la Polisi na Wataalamu wa Jeshi la Wananchi waTanzania. Hadi sasa watuhumiwa sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi. Miongoni mwao ni Victor Calisti Ambrose mwenye umri wa miaka 20, dereva wa bodaboda, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha ambayeanatuhumiwa kwa kurusha bomu hilo. Watuhumiwa wengine watanowaliokamatwa ni raia wanne wa kigeni na Mtanzania mmoja ambaowanashikiliwa kwa mahojiano.

Mheshimiwa Spika,
siku za karibuni kumekuwepo jitihada kubwa sana zawatu wachache wasiyoitakia mema nchi yetu kutaka kupandikiza chuki zakidini miongoni mwa watanzania na kuleta mapigano na mauaji miongonimwa watanzania, sina shaka kuwa shambulio la Arusha ni sehemu yamikakati hiyo miovu. Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa Serikalihaitavumilia hata kidogo mbegu za chuki za kidini miongoni mwawatanzania na tutachukua hatua kali bila huruma kuzigandamiza njama hizimbaya dhidi ya taifa letu. Tutachukua hatua kali kwa mtu yeyote bila kujalihadhi na nafasi yake katika jamii. Amani yetu kwanza na taifa letu kwanza.

Mheshimiwa Spika,
Pamoja na kukamatwa kwa watuhumiwa hao, Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifawametoa maelekezo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo tayariInspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Wakuu wa Vyombo vinginevya Ulinzi na Usalama wameunda Kikosi Kazi maalumu ili kuchunguza tukiohilo.

Mheshimiwa Spika,
kokote duniani, tukio la kushtukiza, linalosikitisha nakuhuzunisha kama hili linapotokea, wananchi wote huungana na kuwawamoja kama taifa na kulaani wahusika na kuwafariji waathirika wa tukiohilo. Nchini Marekani, Mgombea mmoja wa Urais wakati wa uchaguzi mkuuwa Mwaka 2012 aliishutumu Serikali kutokana na tukio la kulipuliwa kwaUbalozi wa Marekani nchini Libya. Ni wazi kuwa mgombea huyu alichukuatatizo lile kama ajenda ya kisiasa. Hata hivyo, alishutumiwa vikali naWamarekani wenzake kwa kuelezwa kuwa ni mtu mwenye kukosa kabisamisingi ya uaminifu na uzalendo kwa taifa lake (Fundamental dishonest).

Serikali inasikitishwa sana wanasiasa wa aina hii ambao wanajitokezanchini na kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa gharama za maisha yaWatanzania. Wanasiasa na viongozi wote wajiepushe na kaulizinazochochea ubaguzi wa kidini, mifarakano ya kijamii na chuki miongonimwa Watanzania. Serikali isilaumiwe kwa hatua kali za kisheriaitakazochukua dhidi ya viongozi wa aina hii ambao maslahi yao ni muhimukuliko maisha ya Watanzania, maslahi yao ni muhimu kuliko utulivu waWatanzania na maslahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania.

Mheshimiwa Spika,
kwa niaba ya Serikali naungana na Watanzaniawenzangu kulaani wahusika wote wa tukio hilo walioshiriki kwa njia yoyote.

Aidha, Serikali kwa nguvu zake zote itahakikisha kuwa watuhumiwa wotewaliohusika na kushiriki kwa namna yoyote katika tukio hili wanasakwapopote walipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Tunawatakaviongozi wa kisiasa, kidini na wananchi wote kwa ujumla kila mmoja kwanafasi yake kuwajibika ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwakisiwa cha amani na utulivu.

Mheshimiwa Spika,
mwisho nawasihi Watanzania wawe watulivu wakativyombo vya dola vikiwasaka waliohusika na shambulio hilo, kila mwenyetaarifa za kuwezesha kukamatwa wahalifu hao atoe taarifa hizo kwa Jeshila Polisi. Aidha, ninawaomba Watanzania tuendelee kukataa vitendo vyauvunjifu wa amani katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
SOURCE: Wavuti.com

Thursday, March 14, 2013

MJADALA: Kushuka kwa elimu Tanzania

Sehemu ya kwanza mpaka ya tatu ya WanaDMV waliofanya mjadala kujadili tatizo la kushuka kwa kiwango cha Elimu na matokeo mabaya ya kidato cha Nne kwa mwaka 2012 Wameeleza na kujadili mengi katika kutafuta sababu zinazoweza kuwa zimetufikisha hapa tulipo na namna tunavyoweza kuepuka ama kuondokana na hali hii. Pia, kuna baadhi ya historia kuhusu elimu toka kwa walimu wastaafu walioshiriki mjadala huu. KARIBU

Sunday, February 24, 2013

BLOGGERS.... SISI NI TATIZO NA / AMA SULUHISHO KWA JAMII

Katika maandalizi ya mkutano wa Diaspora wa mwaka 2010 nchini Uingereza, blogger Issa Michuzi alinukuliwa akisema kuwa "Kwa mahesbu ya haraka haraka hivi sasa kuna blog zinazotumia lugha ya kiswahili zipatazo 200 ambapo pia blog takriban 10 zinaanzishwa kila siku, na kuifanya Tanzania kuw nchi zinazoendelea katika tasnia ya habari kwa njia ya mtandao."
Hayo yalikuwa mahesabu ya mwaka 2010.
Sasa hivi blogu ni nyingi saana.
Yaani hata sisi bloggers hatujuani.
Na wingi wa blogs hizi hauendani na wingi wa mafunzo (japo ya awali) kuhusiana na suala zima la uandishi na maadili yake.
BLOGGERS WENZANGU....
Tuna WAJIBU KWA JAMII yetu jamani.
TUWEKE KANDO UDAKU NA MBIO ZA KUSAKA HITS NA WADHAMINI.
Tuwe macho ya wasioona na kiunganishi kwa wasiounganika
TUSAMBAZE YALIYO MAHITAJI YA JAMII WANDUGU
Ninaomba dakika 35 tu za maisha yako.
TAZAMA HILI. Kisha waza......tunao wangapi.
INAUMA, INASIKITISHA NA INATIA SHAKA SANA
Shukrani saana kwa Dada Rachel wa BLOG YA SWAHILI NA WASWAHILI kwa dokezo la post hii.
Naamini utakumbuka na VIDEO HII hapa chini niliyodokezwa na DADA SUBI WA WAVUTI.COM

Monday, February 18, 2013

Matokeo MABAYA ya kidato cha nne.....NI AKISI YA JAMII INAYOMOMONYOKA.


Photo credit:WAVUTI.COM
Kwenye matokeo haya ya kidato cha nne, nahofia zaidi waliofaulu kuliko waliofeli.
Kwa kuwa nahofia uongo kuliko ukweli.
Na nahisi wapo wafaulishwao mitihani wakifelishwa maisha.
TATIZO langu si nani kafeli na nani kafaulu.
Tatizo ni NINI KUFELI NA NINI KUFAULU?
TAFAKARI NAMI....
1: Unafahamu kuwa nchi yetu ipo ilivyo kwa kuwa imekuwa ikiongozwa na WATAWALA WALIOFAULU tena saana (kwa mujibu wa vyeti vyao)?
2: Unafahamu kuwa ni viongozi haohao waliofaulu ndio wanaopanga mitaala na vipimo vya ufaulu na ufeli wetu?
3: Unafahamu kuwa MITAALA YETU HAIMFANYI AFAULUYE AWEZE KUITUMIKIA JAMII IPASAVYO?
Na kuwa....
Wapo wanaofeli kwa kuwa wana majukumu ya kijamii yanayowakabili hata wawapo shuleni?
Na kuwa....
Wapo wafauluo kwa kuwa wanapuuza chochote katika jamii ili watumie muda wote KUKARIRI majibu ya mitihani yasiyoisaidia jamii?
Ndio maana kuna wakati ninaohisi waliofeli wanaweza kuwa msaada kwa jamii kwa kuwa kiwafelishacho ni USHIRIKA WAO KWA JAMII.
Ukweli ni kuwa MITAALA YA ELIMU YETU HAIMFUNZI MWANAFUNZI KUWA SEHEMU YA MAENDELEO YA JAMII.
Ni kweli kuwa waliofaulu sasa hawajui namna ya kukabiliana na mazingira ya maisha ya nyumbani.
Na ndio maana kuna baadhi ya mambo yanayohusisha WALIOFAULU yanatia shaka.
UNATAKA MIFANO?
Inapatikana kwenye POST HII ambayo ndani mwake nilitoa mifano ya namna ambavyo Tanzania Yangu iko na mikakati thabiti ya KUUA KILICHO CHAKE.
Niliuliza.....
Hivi kama serikali (ambayo naamini ina magari mengi sana) ingeweka ulazima wa magari yote kununua matairi kwenye viwanda vya ndani kama General Tyre, VINGEKUFA? Ama watasema matairi yaliyokuwa yakitengenezwa Arusha hayakukidhi ubora wa barabara na hali ya Tanzania?
Hivi kama serikali ingeweka mkakati madhubuti na kuamua kutumia magari yanayotengenezwa na kiwanda cha jeshi cha NYUMBU katika idara na ofisi zake zooote nchini, tusingepunguza uagizaji wa magari? Ama watasema MAGARI YA NYUMBU HAYAKO KATIKA KIWANGO CHA TANZANIA ukilinganisha na magari yatokayo Marekani / Japan / China?
Hivi serikali ingeamua kutumia (japo asilimia kubwa ya) saruji ya nyumbani, nondo za nyumbani na mafundi wa nyumbani kujenga "vikwangua anga" vyote vya nyumbani, ajira ingekuwa katika kiwangi ilichopo?
TUNAO "WASOMI" WALIOFAULU (kama vyeti vyao ni sahihi) WANAOFANYA MAAMUZI HAYA YASIYOTHAMINI VILIVYO VYETU.
Ni vipi tutaendeleza VAZI LA TAIFA iwapo mBunge asiyevaa SUTI haonekani kuvaa kiheshima ndani ya Bunge la Tanzania? Hata suti tunasikia kuwa wazivaazo wanazitoa nje ya nchi (kama WIKILEAKS ilikuwa sahihi).
Tutawezaje kuendeleza uzalishaji wa magari ya nyumbu ikiwa yale waliyotengeneza miaka hiyo hayajapata mteja na wala kupata nafasi ya kuonyeshwa na kunadiwa (zaidi ya siku ya maigizo ya uhuru)?
Ni vipi kiwanda kama General Tyre kingeshindana na viwanda vya nje iwapo maelfu ama malaki ya magari ya serikali yanatumia matairi yaliyoagizwa nje?
NIKUMBUSHE NILICHOWAHI KUANDIKA HAPA KWENYE POST HII ILIVYOSEMA "TUNAPOFELISHA KIZAZI KWA KUFAULISHA MITIHANI.
Sehemu ya post hiyo niliandika
"Lakini mifumo iliyojengwa na waalimu wetu (ambao yawezekana wamejengewa na waalimu wao) ni kuwa unastahili kupata daraja fulani ili uonekane umefaulu. Na ndio maana msisitizo hauko kwenye kuelewa na kuweza kutumia elimu katika maisha na kutatua matatizo ya jamii, bali ni katika kufaulu mtihani kwa kupata maksi kadhaa.
Tusemeje kuhusu WASOMI wetu wa IDARA YA MAWASILIANO IKULU? Unadhani hawakufaulu? Unadhani kuna sehemu yahitaji watu "waliofaulu" vema kama sehemu nyeti kama hizo? Umeshajiuliza wafanyalo huko? Basi SOMA HAPA ama HAPA uone WAFAULU MITIHANI HAWA WANAVYOLIFELISHA TAIFA KWENYE MAMBO NYETI KAMA MAWASILIANO HUKO IKULU
Na pia nimekuwa nikiona maswali meengi kuwa "kwanini wahandisi wa Tanzania hawabuni vitu vya kuisaidia jamii wakiwa nyumbani" na nahisi hili ndilo jibu lake. Kuwa waandisi ambao wamekuwa na alama nzuri darasani na kutunukiwa vyeti mbalimbali kuonesha UFANISI DARASANI lakini wanapoingia kwenye "ulimwengu wa kazi" inakuwa ni shughuli nyingine kabisa kwani wafunzwacho kwa nadharia hakionekani kuwa halisi kwenye utendaji wao. Ni hapo waajiri wanapoanza kusaka kama waajiriwa wao wana vyeti visivyo halali ama walipata matokeo hayo isivyo halali. Lakini mwisho wa siku ni kuwa WALIFUNZWA KUFAULU MITIHANI NA SIO KUFANIKISHA KAZI WASOMEAZO.
Yaani kwa wabunge ndio yaleyaleee. Kuonekana anafaulu kwa kupigiwa makofi katika kila asemacho hata kama hakina utekelezaji. Yaani twaifelisha jamii yetu kwa kufaulisha kile tunachoamini kuwa mtihani japokuwa kitu hicho si suluhisho la matatizo tuliyonayo."
Ukweli wa mambo ni kuwa MATOKEO MABAYA yameonyesha namna ambavyo JAMII YETU IMEFELI.
Hili si TATIZO....NI MATATIZO.
Hapa ni matatizo mengi.
Hili ni la kijamii zaidi.
Ni malezi kwenye jamii.
Ni maandalizi ya wanajamii.
Ni "utumwa wa kiakili" kwa jamii yetu.
Ni mitaala na vitendea kazi.
Ni moyo wa kazi na wito.
Ni mishahara na maisha ya walimu.
Ni majukumu na mazingira ya wanafunzi

Tazama takwimu hizi zilizobandikwa kwenye UKURASA HUU WA Mhe. Zitto Kabwe
2012 Form 4 results

DIV 1: 1,641 (0.4%)
DIV 2: 6,453 (1.6%)
DIV 3: 15,426 (3.9%)
DIV 4: 103,327 (26.0%)
DIV 0: 240,903 (60.1%)

2011 Form 4 results

DIV 1: 3,671 (1.09%)
DIV 2: 8,112 (2.41%)
DIV 3: 21,794 (6.84%)
DIV 4: 146,639 (43.60%)
DIV 0: 156,085 (46.41%)

2010 Form 4 results

DIV 1: 5,363 (1.53%)
DIV 2: 9,944 (2.83%)
DIV 3: 25,107 (7.14%)
DIV 4: 136,777 (38.9%)
DIV 0: 174,407 (49.60%)

2009 Form 4 results

DIV 1: 4,419 (1.78%)
DIV 2: 10,493 (4.21%)
DIV 3: 27,310 (11.2%)
DIV 4: 130,651 (52.61%)
DIV 0: 65,708 (26.46%)

DHIHIRISHO LA AKISI YA JAMII INAYOMOMONYOKA NA ILIYO NA VIONGOZI WASIOJALI JAMII HUSIKA LITAKUJA  KUDHIHIRIKA PALE ATAKAPOKOSEKANA WA KUWAJIBIKA, KUWAJIBISHWA NA / AMA KUWAJIBISHANA KWA HILI.


Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA
Tuonane "Next Ijayo"

Saturday, September 15, 2012

Wednesday, September 5, 2012

Tanzania Yangu....Yenye WIZARA ZISIZO NA MANUFAA KWA JAMII

Miaka ya karibuni tumeshuhudia kumomonyoka kwa maadili ya uandishi wa habari Tanzania. Fani nzuri na muhimu na kiungo muhimu kwa jamii yetu imeingiliwa.
Na kibaya zaidi, kama ilivyo kwa WIZARA nyingi zenye majina yasiyoendana na UTENDAJI wao, hatuoni lolote likitendeka inapotokea habari ikapotosha jamii.
Tunayo WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO ambayo KWA MTAZAMO WANGU ni kati ya WIZARA MFU ZAIDI NCHINI.
Dk. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Hii ni Wizara ambayo mpaka sasa sijajua inashughulikia vipi suala la HABARI kwa maana ya kuhakikisha NI MUAFAKA NA INAWAFIKIA WANANCHI WOTE.
Ni Wizara ambayo imeshindwa kufanya kazi ya kukuza (hata kutunza utamaduni) wa mTanzania ambao UNAMOMONYOKA KILA SIKU na pia ni Wizara yenye bajeti ya michezo lakini tunaona tunavyozidi kuwa KICHWA CHA MWENDAWAZIMU.
Vijana ndio haooooooo. Wanateseka na kuhaha kusaka maisha na HAKUNA (ama niseme hatuHABARIshwi lolote na Wizara hii kuhusu) mkakati wa kumkomboa kijana
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni moja ya WIZARA MIZIGO ZAIDI Tanzania hasa kwenye suala la michezo kwani zipo nchi (kama Marekani) ambazo HAZINA WIZARA ZA MICHEZO lakini zinafanya vema kwenye sekta hiyo.
Tanzania mpaka sasa hatujaona MKAKATI WA WAZI wa wizara hiyo kuhakikisha kuwa inatengemaa kwenye HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO.
Nikirejea kwenye fani yangu ya habari....huko ndio KUMESAHAULIKA
Wiki kadhaa zilizopita nilibandika picha ya kurasa ya mbele ya gazeti ambalo lilikuwa na habari inayopotosha jamii lakini HAKUNA LILILOSEMWA NA WIZARA.
Ninalowaza hapa ni kuwa,
  • Ni kwanini magazeti "yanayomchafua" Rais (mmoja) yafungiwe na kuacha haya yanayodanganya na kuharibu KIZAZI KIZIMA KISOMACHO?
  • Ni upi wajibu wa WIZARA YA HABARI nchini? Haionekani kusimamia upatikanaji wa HABARI SAHIHI NA MUHIMU kwa wananchi. Haionekani kuhakikisha kuwa wananchi wanaarifiwa kila kilicho sahihi. Haionekani kuhakikisha kuwa wananchi wa pande zote za nchi wanapata habari bila kujali kiwango cha maisha waishicho.
Leo hii nimekutana na habari nyingine (miongoni mwa nyingi) inayopotosha kabisa ukweli wa jitihada za kijana mwenzetu (Diamond) na bado Wizara imekaa kimya.
Labda hawajui uhakika wa safari yake, lakini wanaweza kuuliza na kuangalia UMUHIMU WA HABARI HII KWA JAMII.
HATA KAMA NI KWELI......
  • Kuna athari gani kwa Diamond kuitwa na Freemasons wa Marekani?
  • Ni maelezo gani yanayofuata baada ya kichwa hiki cha habari?
  • Habari hii ina athari gani kwa mamilioni ya wanaomfuatilia?
  • Na pengine ina athari gani kwa jamii nzima inayomuona kama kioo?
  • Si kuna uhuru wa kuabudu? Haujaingiliwa hapa (kama uongo huu ungekuwa kweli)?
Ninaloweza kuona ni kuwa (kama ilivyokuwa kwenye habari nyingi potofu) hakuna atakayewajibika kwa kuipotosha jamii namna hii.
Labda nikumbushe alichowahi kusema Malcom X kuhusu umuhimu wa vyombo vya habari kwani hii ni zaidi ya kazi kwangu.

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA

Tuonane "Next Ijayo"

Monday, September 3, 2012

"Injinia" MIMI na ukarabati wa "nyumba TANZANIA"

PHOTO CREDITS: Cool fun pics
TANZANIA YANGU.
Naitazama Tanzania na matukio kedekede yanayoikumba.
Natazama namna ambavyo inazidi kumomonyoa imani na matumaini kwa wananchi.
Labda wananchi hawajui ukweli na wanaendeshwa na TETESI.
Lakini LABDA wenye kujua ukweli hawajali kuhusu TETESI zinazoiharibia sifa ya kweli nchi yangu.
Kila siku ni matukio, na kila matukio ni KUUNDIWA TUME na kila tume inahusisha wataalamu ambao kwa mujibu wa sheria wana haki ya kuwemo kwenye tume licha ya kuwa WAMO KWENYE MFUMO ULIOHUSIKA KIMAKOSA.
Ni vigumu sana kuunga tume huru nchini bila kuhusisha sehemu ya mfumo uliohusika katika kosa linaloundiwa tume.
Lakini hii haimaanishi kuwa WENYE MADARAKA WANATUMIA MADARAKA YAO VIBAYA.
Linamaanisha kuwa wenye madaraka wamepewa madaraka kuliko wanayostahili.
Ndio nchi yangu TANZANIA.
Ambayo pia naitazama kama NYUMBA ambayo sisi wananchi ni wakaazi na rasilimali zeti ni mali zilizomo ndani.
Ni nani mwenye jukumu la kuijenga Tanzania yetu iwe bora na makini?
Ni sisi wananchi. Wakaazi wa "Tanzaniani" na hata wale waliotoka "ndani" kwenda kusaka riziki nje lakini wanajua kuwa watarejea "nyumbani"
Jambo moja muhimu la kutambua ni kuwa, KABLA HATUJAIJENGA NYUMBA IITWAYO TANZANIA, NI LAZIMA TUIBOMOE. MSINGI WAKE UMEHARIBIKA HIVYO UKARABATI WOWOTE USIOHUSISHA MSINGI NI KUPOTEZA MUDA NA PESA NA MSINGI WOWOTE UTAKAOKARABATIWA BILA KUVUNJA KILICHO JUU NI MIUJIZA.
Ni LAZIMA tuubomoe msingi wa nchi, kisha tuijenge upya.
MIMI na WEWE tuna wajibu mmoja. Kujua ni vipi tutaweza kuibomoa nchi sasa bila kuathiri "watu na mali" zilizo ndani kwani tusipofanya hivyo, "mali na watu" hao wataangukiwa na kuta na kuwa hasara zaidi mbele.
TUCHUKUE HATUA....HATUA SAHIHI...HATUA MAKINI.
  • Tukibomoa kwa umakini, tutapunguza gharama na hata baadhi ya vifaa vya ujenzi vitaweza kutumika tena.
  • Tusisubiri MJENZI aliyeijenga kwa makosa atuambie kuwa alikosea. Lakini tusimpuuze na kutomshirikisha kwenye ukarabati huu.
  • Tusimtishe kuwa tutamfunga kwa makosa ya ujenzi wake lakini tuhakikishe kuwa anajua kosa lake na halirudii tena.
  • Tusitafute sifa kwa kumshutumu mjenzi wa sasa na kusahau kutafuta SIFA ZA ATAKAYEKARABATI.
MWISHO....
Tukumbuke kuwa NI RAHISI KUBOMOA.
Na hata asiyeweza kubeba hata tofali, asiyejua kusoma ramani, asiyefahamu kuchanganya saruji na mchanga na hata asiyejua KWANINI TUNATAKA KUBOMOA anaweza kuwa m'bomoaji mzuri....LAKINI SI MJENZI.
Ninalomaanisha ni kuwa...SI KILA MWENYE UJUZI WA KUBOMOA ATAWEZA KUJENGA.
Tuibomoe Tanzania ili tuweze kuijenga, lakini kabla hatujaibomoa, tuhakikishe tuna mtu sahihi, mwenye ujuzi sahihi, vifaa sahihi, mpango sahihi na maelezo ya muda sahihi atakaotumia kuijenga Tanzania yetu.
La sivyo, ukarabati utakuwa mateso zaidi ya nyumba mbovu tuliyokuwa nayo.

Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!!!!!!!


Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA


Tuonane "Next Ijayo"