Showing posts with label Sports. Show all posts
Showing posts with label Sports. Show all posts
Tuesday, November 5, 2013
Tuesday, August 21, 2012
Je Waafrika tujifunze nini Kutoka Olympic 2012
Tukio la mwisho la Olimpiki 2012 lililokuwa na washindi toka Afrika Mashariki ni mbio za Marathon, mitaani London . Ingawa mshindi hakutoka Bongo- wakimbiaji wetu watatu walishiriki kwa dhati bila mafanikio. Kabla ya kurudi nyumbani wanamichezo walialikwa na Ubalozi wetu Uingereza. Je, ilikuwaje? Nini kilizungumziwa? Na je , nini funzo au somo la mashindano haya kwetu sote?
Tafakari, chukua hatua na kuwa sehemu ya suluhisho ili kuleta mapunduzi katika tasnia ya Michezo Tanzania.
Asanteni,
Urban Pulse Creative wakishirikina na Freddy Macha
Sunday, November 14, 2010
Manny Pacquiao.......mkanda wa 8, katika uzito wa 8 tofauti
Manny Pacquiao akisherehekea mkanda wake katika uzito wa Super Walter baada ya kumshinda mpinzani wake "mgumu" Antonio Margarito.Photo Credit: Getty Images via Yahoo Sports!
Hili ndilo limfanyalo Manny Pacquiao aitwe KING OF POUND FOR POUND. Yaani kwa tafsiri isiyo rasmi ni MFALME WA UZITO MBALIMBALI. Usiku wa kuamkia leo ameweza "kumvuruga" mpinzani wake Anthonio Margarito katika pambano la kugombea mkanda wa World Boxing Council super welterweight katika pambano lililofanyika mbele ya mashabiki 41,734 waliojitokeza ndani ya uwanja wa Cowboy. Hili lilionekana kuwa kati ya mapambano magumu zaidi kwa Pac-Man ambaye wengi walisema hajawahi pambana na "kichwa ngumu" kama Margarito ambaye jana aliingia uwanjani akiwa na "faida ya urefu wa inci 5 na pia paundi 17 zaidi ya Manny.
Paquiao ameshakuwa bingwa wa dunia katika uzito wa paundi 112, 122, 126, 130, 135, 140, 147 na usiku wa kuamkia leo akatwaa taji la uzito wa Paundi 154
Na hizi hapa chini ni dodoso za pambano hilo toka Yahoo Sports
Kisha msikilize alipohojiwa na ESPN baada ya pambano
NA SASA TUNAJUA KWANINI FLOYD MAYWEATHER ANAMKIMBIA BONDIA-MWANASIASA HUYU WA UFILIPINO
Sunday, March 14, 2010
Pacquiao amshinda Clottey kwa pointi
Usiku wa kuamkia leo, bondia Manny "Pacman" Pacquiao amedhihirisha kuwa yeye ni KING OF POUND FOR POUND pale alipomshinda kwa pointi bondia Joshua Clottey wa Ghana. Ushindi huu ambao umekuja kwa njia ya pointi, umekuja baada ya Pacquiao kushinda mapambano yake manne ya mwisho kwa KnockOut na likumbukwalo zaidi ni lile dhidi ya Miguel Cotto. Pia Clottey alipoteza pambano lake dhidi ya Cotto licha kuwa alionesha upinzani mkali na hata kumwangusha.
Lakini sasa kinachoangaliwa zaidi ni "nini chafuata baada ya pambano hili?"
Mei Mosi, Floyd Mayweather (aliyekimbia pambano dhidi ya Pacman) atapanda ulingoni kupambana na Shane Mosley. Na kwa kuwa kila mmoja wa watatu hawa ( Pacquiao, Mayweather na Mosley) alishajitangazia ama kutangazwa kama mfalme wa pound for pound, ushindi wa Pacquiao unafanya pambano la Mei Mosi kuwa la ushindani zaidi likitegemewa kutoa mpinzani wake
Je!! Ni nani atakayejipatia nafasi ya kupambana na Pacman kumsaka MFALME HALISI?
TUSUBIRI HIYO MEI MOSI
Tazama highlights za pambano la Pacquiao vs Clottey toka ESPN.COM
Na mahojiano ya Pacman baada ya pambano hapa chini

Saturday, February 13, 2010
Ufunguzi wa Michuano ya Olimpiki, unajifunza nini?
Blogu hii "ilizaliwa" August 25 2008. Na post ya pili kubandikwa hapa ilikuwa kuhusu kumalizika kwa michuano ya Olimpiki ya majira ya joto. Na swali nililouliza hapa lilikuwa Olimpiki imeisha. Tumejifunza kitu? (isome hapa). Na humo (licha ya uchanga wa uandishi)niliandika na kuuliza maswali kujua kama kuna tunachojifunza. SINA HAKIKA KAMA KIPO.Na sasa leo nimekaa kutazama ufunguzi wa michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi huko Vancouver Canada. Na swali lanijia tena kuwa TUNAJIFUNZA KITU?
Wapo wanaouliza kama kuna "utimamu" wa swali langu hasa ukizingatia kuwa michuano hii ni ya majira ya baridi ambayo sisi hatuna. Lakini kuna ninalotaka kuongea hapa.
Nimewahi kuandika juu ya KUUNGANISHA ELIMU NA MICHEZO NA FAIDA ZAKE KAMA ITASIMAMIWA VEMA.
Ni muunganisho huu (wa elimu na michezo) ambao umekua zao la uzalishaji wa wanamichezo wanaong'ara katika nchi mbalimbali. Mfano mzuri ni wanamichezo wanaong'ara kwenye nchi zisizo na uwezo mkubwa wa kuwaandaa ambao wanatumia uwezo wa kimichezo kwenda kusoma kwa scholarship huku wakijinoa na kutumia nafasi hiyo kufikia kiwango cha kuwawezesha kushiriki michuano mikubwa inayowapa pesa, heshima kwao na heshima kwa nchi zao.
Tumeona nchi kama Jamaica na nyingine ndogondogo za Carribean zikitamba katika michezo lakini asilimia kubwa ya wanamichezo wake wamekuwa wanafunzi katika nchi zilizoendelea. Pia katika michuano hiyohiyo ya majira ya joto tulishuhudia mwadada toka Afrika Kusini akiiwakilisha nchi japo makazi na mazoezi alikuwa akiyafanyia katika chuo kikuu cha Texas.
Na sasa TANZANIA tuna "tunda" moja la mfumo huu ambalo ni HASHIM THABIT ambaye kwa kutumia Scholarship ya UCONN, aliweza kufikia kiwango cha kuingia katika ligi kubwa na maarufu zaidi ya kikapu duniani ya NBA.
Leo hii tunashuhudia nchi ya ETHIOPIA (ambayo iko kwenye ukame zaidi ya Tanzania) ikiwakilishwa katika michuano hii. Mshiriki wake Robel Teklemariam anashiriki katika mchezo wa Cross-Country Skiing. Mzaliwa wa Addis Ababa, Robel alikulia New York nchini Marekani na kupenda mchezo huo kisha akarejea Ethiopia ambako ilimchukua miaka 3 kuweza kutimiza mambo muhimu kuiwezesha nchi kuwa na vigezo vya kuwa na kamati ya Olimpiki ya majira ya baridi na kumuwezesha kuiwakilisha. Alishiriki michuano ya 2006 ambako hakufanya vema sana na sasa amerejea.
Pia kuna Kwame Nkrumah-Acheampong wa Ghana ambaye alikuwa mfanyakazi wa mapokezi katika kituo cha skiing nchini uingereza kisha akaanza kujifunza na sasa anakuwa m-Ghana wa kwanza kushiriki michuano hii.
Senegal nayo inawakilishwa naye Leyti Seck ambaye anashiriki katika skiing.Afrika ya kusini nayo itawakilishwa na wanamichezo watatu ambao ni Peter Scott (Alpine Skiing), Bruce Warner (Paralympics Alpine) pamoja na Oliver Kraas (Cross Country Skiing).
Sijui unajifunza nini katika haya, lakini naamini kwa kuwekeza katika michezo kwa watoto ama wanamichezo wadogo, tunawajengea mazingira mazuri ya kunyakuliwa na vituo mbalimbali vya kuendeleza michezo na kisha kukuza vipaji vyao na kukuza uwakilishi nchi yetu.
Kutegemea kuwa na wawakilishi wazuri ambao hawana matayarisho mazuri ni kujidanganya. Na kutegemea kuwa na timu itakayotuwakilisha vema kwenye michuano mikubwa kwa kuanzia michezo ukubwani pia ni ndoto.
Tanzania imeamua kitu kimoja ambacho ni AMA KUWA NA WANAMICHEZO WAZOEFU WASIO NA ELIMU (kwa kuwa utastahili kutosoma ili ucheze) AMA KUWA NA WASOMI LAKINI WASIOLELEWA KIMICHEZO (kwa kuwa hakuna michezo mashuleni)
Sina hakina na DANGANYA TOTO ambayo Rais Kikwete anaifanya kwa KUGHARAMIA MAMILIONI YA DOLA KUMLIPA KOCHA WA KIMATAIFA ILHALI ANASEMA HAWEZI KURUHUSU MICHEZO KUANZIA SHULE ZA MSINGI. Alipohojiwa na mchambuzi wa michezo Bwn Israel Saria hapa, Rais Kikwete alisema "it is up to the Minister of Sports to come up with a good structure for how talent can be identified from class level up to national level. We should not forget that we also have good talent on the street and in some way this talent has to be identified and developed by having sports officers in the area or in clubs and retired sports figures, for example."
Saturday, January 23, 2010
Mtagwa apoteza pambano.
Monday, January 18, 2010
"Niko kwenye hali nzuri kwa pambano" Rogers
Bondia Rogers "The Tiger" Mtagwa (pichani juu) amesema yuko kwenye hali nzuri kiafya na kiakili kwa ajili ya pambano lake la kuwania mkanda wa dunia litakalofanyika jumamosi ijayo dhidi ya Yuriokis Gamboa wa Cuba.Akizungumza nami toka nyumbani kwake Philadelphia katika jimbo la Pensylvania, Rogers ambaye kwa miaka miwili mfululizo amepigana katika mapambano yaliyosemwa na baadhi kuwa "mapambano ya mwaka" (dhidi ya Thomas Villa mwaka 2008 na dhidi ya Juan Lopez mwaka jana) amesema anaendelea vema na mazoezi yake anayofanya mara tatu kwa siku na kuna tofauti kubwa kimaendeleo ukilinganisha na alivyokuwa katika pambano lililopita.
"Najua mpinzani wangu wa sasa ni mzuri kuliko niliyepambana naye awali lakini nami niko kwenye shape nzuri kuliko nilivyokuwa katika pambano la Lopez" alisema Rogers alipozungumza nami.
Pambano hili laonekana kuwa muhimu na gumu zaidi kwa mabondia wote. Rogers ana mapambano mengi zaidi ya kulipwa (professional) japo Gamboa ameshiriki mengi ya ridhaa (amateur)
Nilipomuuliza Rogers juu ya maandalizi na namna anavyoangalia mikanda ya mapambano ya Yuriokis, amesema ameiangalia mikanda yake lakini anajitahidi kuwa katika hali nzuri kimchezo na kutotumia mikanda hiyo kama kigezo pekee cha kumsoma mpinzani wake kwani kama yeye alivyobadilika tangu pambano lake la mwisho mwaka jana, anajua kuna uwezekano Gamboa naye akawa na mabadiliko. Lililo kuu ni kuwa katika hali nzuri na pumzi ya kutosha na kupambana mpaka dk ya mwisho.
Mahojiano ya Mtagwa na Kaka Sunday Simba Shomari yatarushwa usiku wa leo katika matangazo ya SAUTI YA AMERICA idhaa ya Kiswahili. Usikose. Na mahojiano yake na blogu ya Changamoto yetu yatawajia punde nikipata mtunzaji wa sauti online kwani niliyekuwa namtumia (imeem.com) "alitukimbia" bila taarifa.
Tazama Press Conference ya pambano la Jumamosi hapa chini
KILA LA KHERI KAKA MTAGWA.
Thursday, December 3, 2009
2010 kuwa na rekodi ya "wazee" kwenye Heavyweights
Bernard Hopkins enzi zake akiwa na mikanda yake
Evander enzi za enzi. Je wataweza kurejesha makali haya?Mwaka 2010 unaweza na rekodi ya kuwa na "wazee" kama mabingwa wa Dunia endapo nyota waliotawala mchezo huo kwa miongo kadhaa Bernard "The Executioner" Hopkins na Evander "The Real Deal" Holyfield watashinda mapambano yao mawili wanayokabiliana nayo mbeleni.
Hopkins ambaye usiku wa kuamkia leo alishinda pambano lake la raundi 12 dhidi ya Enrique Ornelas, ameonesha nia ya kuwania taji alilonalo David Haye ilhali Evander atakayepambana Jan 16 huko Uganda dhidi ya Francois Botha huku akiwa anawaza kupanda ulingoni mwishoni mwa mwaka 2010 kuwania mkanda wa WBC alionao Vitali Klitschko.
Hopkins atakuwa na miaka 45 mwanzoni mwa mwakani ilhali Evander ana miaka 47 sasa hivi.
Bondia George Foreman ndiye anayeshikiliza rekodi ya bondia mwenye umri mkubwa zaidi alipochukua mkanda akiwa na miaka 45 alipomshinda Michael Moorer kwa KO mwaka 1994.
Evander aliyeanzia kwenye uzito wa Cruiserweight, anashikilia rekodi ya kuwa bingwa wa Dunia uzito wa juu mara nne na anasaka rekodi ya tano.
Hopkins yeye alikuwa bingwa asiyepingika katika uzito Middleweight kwa zaidi ya miaka 10 kabla hajaamua kuongeza uzito kwenda Light Heavyweight na sasa anasaka mkanda wa Heavyweight.
Yetu macho na kila la kheri kwao wote
Sunday, November 29, 2009
Mtagwa kurejea ulingoni Jan 23 kuwania mkanda wa WBA.
Image courtesy of http://www.phillyboxinghistory.com/Baada ya kupoteza pambano lake kiutatanishi Oktoba 10 dhidi ya Juan Lopez na kukataliwa pambano la marejeano licha ya kuonesha uwezekano mkubwa wa "kumuumbua" Lopez, bondia mTanzania aishiye Philadelphia Rogers "The Tiger" Mtagwa atapanda ulingoni Jan 23, 2010 kupambana na bondia anayefanya vema saana na nyota ing'aayo toka Cuba Yuriorkis Gamboa.
Pambano hilo litakalopiganiwa New York na kuonekana kupitia HBO, litakuwa ni la kuwania mkanda wa Gamboa wa uzito wa Unyoya (featherweight) unaotambuliwa na Chama cha Ndondi Ulimwenguni (WBA). Usiku huohuo na katika ukumbi huohuo, Juan Manuel Lopez ambaye alipata ushindi dhidi ya Mtagwa atapambana na Steven Luevano kuwania mkanda wa Shirikisho la Ndondi Ulimwenguni (WBO) unaoshikiliwa na Luevano.
Iwapo Mtagwa atavuka kigingi hiki kigumu (kulingana na ubora na upiganaji wa Bwana mdogo Gamboa) atakuwa amejiweka katika mazingira mazuri ya kurejea ulingoni na Lopez kama wataweza kuafkiana katika kuunganisha mikanda kwani yote ni ya uzito mmoja.
Hapa chini ni Video ya pambano la Mtagwa la mwezi uliopita
Kila la kheri katika maandalizi yako Kaka Mtagwa.
Sunday, November 15, 2009
Manny "Pacman" Pacquio... Mkanda wa 7 katika uzito wa 7 tofauti
AP Photo/Mark J. Terrill
Picha toka HBO.COMHili ndilo linalomfanya aitwe MFALME WA POUND-FOR-POUND. Ni kwa kuwa ameweza kubadili uzito anapigana na kufanya vema kote. AMETAWALA kila uzito aendao na usiku wa kuamkia leo, ameweza kuvuka kile kilichokuwa kikionekana kuwa kigingi kikubwa zaidi katika maisha yake ya ndondi pale alipomsimamisha bondia Miguel Cotto wa Puerto Rico kwa TKO katika sekunde ya 55 ya raundi ya 12.
Fuatilia tukio zima katika picha kwa kuBOFYA HAPA, ama kusoma kila kilichotokea katika raundi zote 12 kwa kubofya hapa ama HAPA
Baada ya kumaliza pambano, Manny alifanya mahojiano na ESPN ambayo unaweza kuyaangalia hapa chini
Sasa njia i-wazi kwa m-Fillipino huyo kupambana na Floyd "Money" Mayweather katika kubainisha ni nani aliye "mfalme" wa ndondi ulimwenguni.
Hata hivyo, Manny amekuwa akinukuliwa akisema kuwa Mayweather ameanza kuonesha dalili za kumkacha jambo ambalo anasifika kwa kufanya. Alishagoma kupambana na Cotto mara kadhaa, akagoma kupambana na Antonio Margarito na hata bondia ambaye anabadili uzito ili kutafuta wapinzani Paul Williams.
Kama pambano la Pacquio vs Mayweather litafanyika kama ambavyo wengi tungependa, litampa nafasi Freddie Roach ambaye ni mkufunzi wa Manny kulipiza kisasi kwa Mayweather baada ya kugomewa pambano la marudiano alipokuwa na De La Hoya.

Sunday, October 11, 2009
Rogers Mtagwa...
Aonesha uhodari, nusura amuumbue Lopez...agomewa pambano la marudiano
Lopez (shoto) akipambana na Mtagwa (kulia) Picha na Chris Farina/Top Rank
"Mtagwa hurt Lopez with a series of shots late in the 10th round and never stopped swinging.
He sent Lopez staggering into the ropes at the end of the 11th round. Lopez only avoided a knockdown because he grabbed the ropes to keep himself upright and Cotton didn't see it as the bell rang.
Then the real drama started when the bell rang to start the 12th round.
Lopez came out of his corner on unsteady legs and you just knew it would be a race against the clock.
Could Lopez last three minutes?
He did, but just barely.
Mtagwa was all over him. Lopez was desperate to survive. He had no defense and could barely hold on and throw the occasional punch to stay in the fight as the crowd was standing and going wild."
Huu ni uchambuzi wa mkongwe wa uandishi wa ndondi katika mtandao wa ESPN Dan Rafael alipokuwa akieleza mpambano kati ya Rogers Mtagwa vs Jual Manuel Lopez. Katika pambano hilo Manuel alitetea ubingwa wake kwa kuonesha ujasiri wa kumaliza pambano aliloonekana kuumizwa katika raundi 3 za mwisho. Rogers ambaye alikuwa akipewa nafasi ndogo ya kushinda amekuwa bondia wa kwanza kumfikisha Lopez raundi ya 11 na ilionekana wazi kuwa alimzidi nguvu katika raundi ya 10-12. Hata hivyo, licha ya kuonesha uwezo mkubwa wa kumpiga na kunyakua mkanda huo, Promota Bob Arum amekataa ombi la Mtagwa la pambano la marudiano na kusisitiza kuwa anasonga mbele na maandalizi ya pambano la Jan 23 dhidi mmoja kati ya Celestino Caballero (ambaye anaonekana kutaka pesa zaidi ya zile ambazo promota Arum anapanga kumlipa) ama mabingwa wengine katika uzito wa featherweight Steven Luevano au Elio Rojas. Uamuzi huu wa kibiashara zaidi umeonekana kuleta mnong'ono kidogo kwa mashabiki wanaotoa maoni wakisema hata kama Mtagwa hatapata re-match, Lopez si bondia bora kama asemwavyo kwani hajapambana na nyota halisi wa mchezo huo na usiku wa jana ulikuwa dhihirisho.
MTAZAMO WA CHANGAMOTO YETU::Si jambo la kushangaza saana kwa promota kufanya hivyo kwani anaonekana kufuatilia maslahi zaidi na amegundua kuwa Lopez anauza zaidi ya Mtagwa (kutokana na upinzani wa jadi uliopo baina ya washabiki wa ndondi wa Puerto Rico na Mexico) na licha ya sifa zinazozidi ubora wa Lopez, bado wanajua kuwa mashabiki wa Puerto Rico na Mexico wanaingiza pato kubwa hivyo kumuweka Lopez katika nafasi ya kunyang'anywa mkanda na Mtagwa ni kupoteza pesa nyingi anategemea kama atampambanisha Lopez na bondia mwingine wa Marekani ya kusini katika pambano la kugombea mkanda. Na hili ndilo linaloonekana kuharibu ulimwengu wa ndondi kwa sasa ambapo ubora wa mabondia sio unaotawala mapambano, bali matakwa ya mabondia na mapromota. Tunaona sasa Heavyweight ilivyolala kwa kuwa hakutakuwa na pambano la kuunganisha mikanda (UNIFICATION BOUT) ambalo miaka ya nyuma lilitumika kumsaka bingwa bora zaidi wa uzito huzika, kwani wenye kuishikiliza mikanda ya uzito wa juu (ndugu Vitali na Vladimir Klitscho) walishaapa kutopigana baina yao. Tuliona namna ambavyo Mayweather aliwakimbia Cotto, Margaritto na hata Paul Williams licha ya kuwa ndio waliokuwa katika ubora na orodha ya kupambana naye. Na sasa tumeona namna ambavyo Mtagwa ameonesha kuwa bondia pekee aliye tishio kwa Lopez lakini promota Bob Arum anazuia uwezekano wa bondia wake kupoteza mkanda.
KAZI NZURI MTAGWA NA TWATUMAI MENGI MAZURI YAKO MBELE YAKO PUNDE.
Lopez (shoto) akipambana na Mtagwa (kulia) Picha na Chris Farina/Top Rank"Mtagwa hurt Lopez with a series of shots late in the 10th round and never stopped swinging.

Wednesday, October 7, 2009
Mechi ya kwanza ya Hasheem Thabeet NBA......MAFANIKIO
ANGALIZO. Hiyo si "tatoo", ni maandishi juu ya picha toka www.memphisbluebears.com
Hasheem Thabeet, usiku wa kuamkia leo alifungua pazia la kushiriki mechi ya kwanza ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA pale alipoichezea timu yake ya Memphis Grizzlies dhidi ya Washington Wizards katika mechi ya kwanza kati ya mapambano ya kujipima nguvu kabla ya kuanza rasmi kwa msimu wa 64 wa ligi ya NBA utakaoanza rasmi Oktoba 27 2009 na kumalizika Aprili 14 2010. Katika mechi hiyo ambayo Wizards walishinda 101-92, Hasheem alionekana kufanya vema kwa kuweza kufunga pointi 6 na kuzuia mitupo 4 ndani ya dakika 15. Huu si mwanzo m'baya kwa Hasheem ambaye alikuwa chaguo la pili kwa thamani katika draft ya NBA na sasa ameanza ngwe nyingine ya UCHEZAJI WA KULIPWA katika mpira wa kikapu.Kila la kheri Hasheem
Rogers "The Tiger" Mtagwa: Ndani ya Pay-Per-View pekee Oktoba
Ni Jumamosi hii (Okt 10)
Hali ya uchumi iliulazimisha mwaka huu kuwa na mapambano machache saana ya kulipia (Pay Per View) na katika mwezi huu, kutakuwa na pambano moja tu ambalo katika pambano kuu, anasimama nyota wa ndondi toka Tanzania Rogers "The Tiger" Mtagwa.
Roger mwenye rekodi ya (26-12-2) na anayeshikilia nafasi ya 9 ya ubora wa ndondi kwa uzito wake katika orodha ya WBO atapambana na Juan Manuel Lopez(49-4-1) wa Caguas, Puerto Rico katika kuwania mkanda wa Lopez katika uzito wa WBO junior featherweight.
Pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa WaMu Theatre uliopo eneo maarufu la Madison Square Garden jijini New York.

Hii ni hatua kubwa na ya kujivunia kwa Mtagwa ambaye ameonesha ujasiri na maendeleo makubwa katika ulimwengu wa ndondi kwa kutwaa ubingwa wa NABF na USBA katika uzito wa Feather na pia kwa kuonekana kuboreka kila ajapo ulingoni kiasi cha kuwafanya wengi kuliona pambano lake la mwaka jana dhidi ya Thomas Villa kama PAMBANO LA MWAKA 2008. Katika pambano hilo lililopiganwa Tucson Arizona, Mtagwa alishinda kwa KO ya raundi ya 10. Tazama hapa chini
Tujiunge kwa pamoja kumshangilia (kwa watakaoweza) na kumuombea Mtanzania mwenzetu anayefanya vema sasa katika ulimwengu wa ndondi aweze kufanikiwa.
Kuwa kwenye pambano pekee la pay per view kwa mwezi huu ni kuonesha thamani yake kwani wapo mabondia wengi wenye majina ambao wameshindwa kuweka mapambano yao kwenye hadhi hiyo.
Kumbuka kuwa nyota kama Yuriorkis Gamboa toka Cuba atapigana katika pambano la utangulizi usiku huo dhidi ya Whyber Garcia katika kuwania umiliki wa mkanda wa WBA "regular" featherweight title unaoshikiliwa na Gamboa kwa sasa. Nyota wengine waliopata kushikilia mikanda ya dunia ambao watapigana kwenye mapambano yasiyo ya kulipia ni pamoja na Jermaine Taylor vs Arthur Abraham watakaochuana Oct 17.

Blog ya Changamoto Yetu inapenda kumtakia kila la kheri Rogers Mtagwa katika pambano hili muhimu maishani mwake.
ANGALIZO KWA SERIKALI: Rogers anapigana sasa na anafanya vema. Hatuoni wala kusikia juhudi za kumpa ushirikiano ili aweze kufanikisha nia yake njema. Hatutapenda tena kuona mnakwenda kumpokea "SHUJAA" mwingine na kumualika kwenye ofisi zenu mbalimbali na kumfanya aonekani ni mwakilishi wa Taifa letu ilhali hamumsaidii anapohaha kukwea kileleni.
Yasije yakawa yaleyale niliyoandika HAPA
Thursday, August 20, 2009
Ati nini???? Anapimwa kujua kama ni MSICHANA KAMILI??

Kweli kuna ya Musa na Firauni. Na unapodhani umeona yote, ujue kuna mengine ya kujifunza.Binti wa miaka 18 toka Afrika Kusini Caster Semenya (pichani juu) ambaye ameshinda KWA KISHINDO mbio zinazoendelea za mashindano ya dunia huko Ujerumani, anaelekea kulazimika KUFANYIWA UCHUNGUZI KUONA KAMA ANA SIFA ZA KUMFANYA ASHIRIKI MICHUANO HIYO UPANDE WA WANAWAKE.
Sina utaalamu na hili na nisingependa kujaribu kutafsiri (kwa kiingereza changu cha ugoko) labda nikueleze kuwa HABARI KAMILI IKO HAPA
Ila huyu mdada ni kiboko. Hebu muangalie hapa chini (unaweza kuanzia dk 2:15) ama "alivyowafunga tela" kuanzia dk ya 4. Nisichojua wanafanya tests ngapi, wanazifanyaje na pia sijui ni nani anayeweza kwenda kwenye michuano hiyo tena AKIIWAKILISHA NCHI akiwa na jinsia tofauti na ashindanao nao. Kama nilivyosema, lazima mmoja aonekane kituko. Wanaotaka apimwe ama yeye (kulingana na majibu yatakavyokuja)
AMA KWELI TUMEUMBWA KATIKA MIILI NA MAWAZO TOFAUTI
Mtazame hapa chini
Sunday, July 26, 2009
Nyota mwingine auawa. Ni Vernon "The Vipe" Forrest
Tulikuwa tukijiandaa kushuhudia mpambano wa mkongwe huyu wa ndondi wiki ijayo (Aug 1)ambapo alitegemewa kutoa upinzani mkali na pengine kuibuka mshindi dhidi ya Sergio Martinez, lakini hilo halitatokea kwani Forrest ameuawa jana katika jaribio la kumpora gari lake aina ya Jaguar.Licha ya kuwa katika timu ya taifa ya Marekani iliyoshiriki Olympic mwaka 1992 na pia kuwa bingwa wa WBC uzito wa Super Walterweight, Forrest anakumbukwa zaidi kwa mapambano yake mawili dhidi ya Shane "Sugar" Mosley ambapo alishinda yote na Sep 18 mwaka jana alitwa mkanda wa WBC uzito wa paundi 154 lakini alinyang'anywa mwezi may mwaka huu baada ya kushindwa kuutetea kutokana na maumivu ya mbavu. Mpaka mauti yanamkuta, Forrest alikuwa na rekodi ya kushinda mapambano 41, kupoteza 3 na kutoka sare 1 na alishinda mapambano 29 kwa knockout.
Forrest anaongeza orodha ya wanamichezo maarufu waliouawa katika siku za karibuni na kuacha utata wa mwisho wa maisha yao. Habari za nyota wengine waliofariki karibuni (na pengine kiutata)BOFYA HAPA
Taarifa zaidi toka ESPN ni hii hapa chini
REST IN PEACE "THE VIPE"
Sunday, July 12, 2009
Nyota mwingine (Arturo "Thunder" Gatti) afa na kuacha utata zaidi
Mtiririko wa wanamichezo na wasanii mbalimbali kuendelea kupoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha unazidi kuishangaza dunia. Mmoja kati ya mabondia bora kabisa kuwahi kutokea ulimwenguni Arturo Gatti amekutwa amefariki katika chumba cha hoteli huko Brazil ambapo mkewe amehusishwa na kifo chake.Gatti ambaye anaamika kuwa mmoja wa bondia bora zaidi katika kizazi na uzito wake, aliwasili hotelini hapo na mkewe na mtoto wao wa mwaka mmoja na yasemekana kuwa kulikuwa na kutoelewana baina ya wanandoa hawa masaa machache kabla ya kifo cha Gatti. Polisi wa jimbo la Pernambuco nchini Brazil wanamshikilia mke wa bondia huyo Bi Amanda Rodrigues wakimhusisha na kifo hicho hasa kwa kuwa yasemekana wapenzi hawa walikuwa na wivu wa kupindukia baina yao.
Kifo cha Arturo Gatti kimekuja wakati kuna maswali ambayo hayajajibiwa kuhusu kifo cha nyota wengine kama Michael Jackson ambaye dadaye Latoya amekaririwa leo akisema kuwa "wamemuua kakangu" (Bofya kuisoma) na pia siku kadhaa baada ya nyota mstaafu wa Mpira wa "miguu" wa Marekani Steve McNair ambaye yasemekana "aliuawa na mpenziwe akiwa amelala" (bofya kuisoma)
Nimekuwa nikimfuatilia Gatti tangu nikiwa nafanya kipindi cha michezo pale Times Fm.
Tazama highlights ya mapambano yaliyompa heshima kubwa Arturo "Thunder" Gatti hapa chini.
Thursday, June 25, 2009
HASHEEM THABEET anyakuliwa na Memphis Grizzlies kama Second Pick
Kundi la Draft
Thabeet akipongezwa baada ya kutangazwa kama mchezaji mpya wa Memphis Grizzlies
Akiwa kwenye pozi jana. Picha zote toka NBA.COMNyota wa kikapu toka nchini Tanzania Hasheem Thabeet amenyakuliwa na timu ya MEMPHIS GRIZZLIES ya Tenesee kama Second Pick. Hasheem ana mengi ya kukamilisha na ana uwezo wa kukamilisha na twampongeza katika kila jema alilotenda na kumuombea mema katika kila jema apangalo kutenda.
KILA LA KHERI HASHEEM. Angalia video ya Hasheem akihojiwa kuhusu safari yake mpaka alipo.Kisha mtazame pale alipopata pick yake.Video zote toka ESPN
KILA LA KHERI HASHEEM. Angalia video ya Hasheem akihojiwa kuhusu safari yake mpaka alipo.Kisha mtazame pale alipopata pick yake.Video zote toka ESPN
KILA LA KHERI Martin Kolikoli & HasheemThabeet
Martin Kolikoli. Picha kwa hisani ya Michuzi Blog
Hasheem ThabeetMoja kati ya matukio makubwa ya kimichezo yanayoendelea hapa Marekani wiki hii ni kupatikana kwa wachezaji wapya watakajiunga na mchezo wa kikapu wa kulipwa katika ligi ya Taifa NBA. Na kama ilivyo miaka yote, tukio hili (ambalo wachezaji husika hupanda na kushuka thamani kama soko la hisa)linafika ukingoni leo ambapo mmoja wa wachezaji wa vyuo mwenye thamani ya juu ni mTanzania Hasheem Thabeet. Lakini pia yupo mchezaji Martin Kolikoli ambaye ameingia kwenye Draft hiyo.
Kwa Pamoja tunapenda kuwatakia kila la kheri katika mchakato huo ili wapate timu zitakazowakuza kimchezo na wao kuwa NYOTA NJEMA kwa chipukizi wengi na jamii kwa ujumla
Kwa Pamoja tunapenda kuwatakia kila la kheri katika mchakato huo ili wapate timu zitakazowakuza kimchezo na wao kuwa NYOTA NJEMA kwa chipukizi wengi na jamii kwa ujumla
KILA LA KHERI KWENU MARTIN na HASHEEM
Saturday, March 28, 2009
"Balozi mdogo" anayefanya vema kuitangaza nchi

Namwita "balozi mdogo" mwenye kuitanganza nchi kwa kasi, basi naamini anafanya kazi njema kwa sasa. Namzungumzia Hasheem Thabeet, kijana ambaye macho ya wengi katika michuano hii ya vyuo inayoelekea ukingoni yamemwelekea yeye.
Muda si mrefu wameshinda Ubingwa wa NCAA KANDA YA MAGHARIBI na kwa wale wafuatiliaji watakubaliana nami kuwa sasa Hasheem amewalazimisha wapendao mchezo kumuangalia, kisha kujiuliza kuhusu Historia yake na kisha kuweza (kwa lazima ama hiari) kuitambua ama kutambua uwepo wa Tanzania.
Mfano mzuri ni hayo maelezo ya picha yaliyo katika moja ya mitandao mikubwa ya michezo ulimwenguni wa ESPN
Connecticut's Hasheem Thabeet, of Tanzania, yells in celebration after their 82-75 win over Missouri in a men's NCAA college basketball tournament regional final in Glendale, Ariz., Saturday, March 28, 2009. (AP Photo/Chris Carlson)Hasheem amepitia changamoto nyingi kuanzia kukashfiwa na baadhi ya waTanzania kwenye baadhi ya mitandao, kashikashi za kujibidiisha kuwa katika kiwango alichopo, kucheza achezavyo na kisha kutwaa Tuzo ya mchezajibora-mwenza wa mwaka wa Big East na mlinzi bora.
Ni CHANGAMOTO YETU sote si kumpa ushirikiano, lakini kusaidiana naye kujua ni vipi ameweza kufikia alipo maana najua ni wengi wenye kipaji na uwezo kama wake walio nchini lakini hawajui njia sahihi ya kufika alipofika yeye.
PONGEZI KWAKO HASHEEM. KUMBUKA KUWA KILA HATUA UPIGAYO NI MWANZO WA NYINGINE ITAKAYOKUFIKISHA KATIKA KIWANGO, KIPATO NA HESHIMA KUBWA ZAIDI. BIDII NA IMANI VITAKUFIKISHA UTAKAKO
PONGEZI KWA WATANZANIA WALIOJUMUIKA NA MAMAKE KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA WAKIMSHANGILIA KAMA AMBAVYO WALIONEKANA MARA KADHAA LUNINGANI.
Nasi wana changamoto blog tutajitahidi kwa kina kutekeleza sehemu ya jukumu hilo kufanikisha nia hiyo
Kwa picha zaidi za mchuano huo, Bofya hapa
Friday, March 20, 2009
Hasheem Thabeet. GREAAATTTTTTT!!!!

Picha zote mali ya Michael Pere & Carolyn Kaster wa AP kupitia ESPN.COMKama kuna nyota tunaopaswa kujivunia sasa ni Hasheem. Na ni nyota njema kwa nchi (na hapa najua kuna wanaopinga) lakini kulingana na historia yetu kimchezo sasa yapaswa kumpa heshima anayostahili.
Kwa sasa Hasheem anaonekana kama mchezaji nyota pengine) kuliko wote katika timu yake ya chuo cha Connecticut. Ni mchezaji bora katika kanda yake na ni nyota njema ionekanayo kung'aa katika maidha ya mpira wa kikapu hapa nchini.
Jana katika kuelekea tamati ya michuano hiyo ambayo wiki hii inachukua nafasi kubwa kabisa, tumeshuhudia kazi aliyoifanya na kwa kushirikiana na wenzake wameweza kuinyuka timu na Chatanooga kwa tofauti ya pointi 56.
Kwa picha zaidi bofya hapa
Subscribe to:
Posts (Atom)