Wednesday, October 7, 2009

Rogers "The Tiger" Mtagwa: Ndani ya Pay-Per-View pekee Oktoba

Ni Jumamosi hii (Okt 10)

Press Conference .

Hali ya uchumi iliulazimisha mwaka huu kuwa na mapambano machache saana ya kulipia (Pay Per View) na katika mwezi huu, kutakuwa na pambano moja tu ambalo katika pambano kuu, anasimama nyota wa ndondi toka Tanzania Rogers "The Tiger" Mtagwa.
Roger mwenye rekodi ya (26-12-2) na anayeshikilia nafasi ya 9 ya ubora wa ndondi kwa uzito wake katika orodha ya WBO atapambana na Juan Manuel Lopez(49-4-1) wa Caguas, Puerto Rico katika kuwania mkanda wa Lopez katika uzito wa WBO junior featherweight.
Pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa WaMu Theatre uliopo eneo maarufu la Madison Square Garden jijini New York.
Hii ni hatua kubwa na ya kujivunia kwa Mtagwa ambaye ameonesha ujasiri na maendeleo makubwa katika ulimwengu wa ndondi kwa kutwaa ubingwa wa NABF na USBA katika uzito wa Feather na pia kwa kuonekana kuboreka kila ajapo ulingoni kiasi cha kuwafanya wengi kuliona pambano lake la mwaka jana dhidi ya Thomas Villa kama PAMBANO LA MWAKA 2008. Katika pambano hilo lililopiganwa Tucson Arizona, Mtagwa alishinda kwa KO ya raundi ya 10. Tazama hapa chiniTujiunge kwa pamoja kumshangilia (kwa watakaoweza) na kumuombea Mtanzania mwenzetu anayefanya vema sasa katika ulimwengu wa ndondi aweze kufanikiwa.
Kuwa kwenye pambano pekee la pay per view kwa mwezi huu ni kuonesha thamani yake kwani wapo mabondia wengi wenye majina ambao wameshindwa kuweka mapambano yao kwenye hadhi hiyo.
Kumbuka kuwa nyota kama Yuriorkis Gamboa toka Cuba atapigana katika pambano la utangulizi usiku huo dhidi ya Whyber Garcia katika kuwania umiliki wa mkanda wa WBA "regular" featherweight title unaoshikiliwa na Gamboa kwa sasa. Nyota wengine waliopata kushikilia mikanda ya dunia ambao watapigana kwenye mapambano yasiyo ya kulipia ni pamoja na Jermaine Taylor vs Arthur Abraham watakaochuana Oct 17.

Blog ya Changamoto Yetu inapenda kumtakia kila la kheri Rogers Mtagwa katika pambano hili muhimu maishani mwake.
ANGALIZO KWA SERIKALI: Rogers anapigana sasa na anafanya vema. Hatuoni wala kusikia juhudi za kumpa ushirikiano ili aweze kufanikisha nia yake njema. Hatutapenda tena kuona mnakwenda kumpokea "SHUJAA" mwingine na kumualika kwenye ofisi zenu mbalimbali na kumfanya aonekani ni mwakilishi wa Taifa letu ilhali hamumsaidii anapohaha kukwea kileleni.
Yasije yakawa yaleyale niliyoandika HAPA

4 comments:

chib said...

Naungana nawe katika kumtakia kila la heri.

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kila la kheri maana hizo ndondi bwana zinatoa meno hizo...LOL

viva afrika said...

kila lililo la kheri kwake, manake kwa rekodi hiyo anahitaji pai dua zetu.

Aliko said...

Big Up Mtagwa da raundi za mwanzo katika hio clip nilidhani hatoshinda hilo pambano