Tuesday, August 18, 2009

Tanzania yangu. Ivunayo isipopanda

Labda TANZANIA YANGU ni jina limaanishalo SERIKALI. Ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikijitokeza kupongeza na kuonekana pale penye mafanikio na "kuwa likizo" kwenye matatizo. Ni kweli. Binafsi nilishangaa kuona watu wanashangaa kumuona Naibu Waziri wa michezo kaenda kumpokea Hasheem Thabeet uwanja wa ndege. Wapo waliohoji umuhimu wa Thabeet na wapo waliohoji majukumu ya Naibu Waziri. Kwa ujumla kila mtu alikuwa na lake la kueleza japo kwangu si kila mtu alikuwa na maana katika kutetea hoja yake. Lazima tukubali kuwa Hasheem amekuwa mtanzania wa kwanza kupata nafasi ya kucheza katika ligi ya Taifa ya mpira wa kikapu hapa Marekani NBA na ni lazima apate "attention" toka nyumbani na hasa katika safari yake ya kwanza kurejea tangu ajiunge na Memphis Grizzlies. Na si ajabu kwa SERIKALI kujibaraguza pembeni yake na kuonesha (kama) inajali ilhali tunajua mchango wao katika kufanikisha safari za wengi wenye nia ya kuwa kama Hasheem. Si jambo la kushangaza hata kidogo kwa sisi tunaofuatilia habari za michezo kwa muda mrefu. Hamkumbuki namna ambavyo WAZIRI MKUU alisherehekea ushindi wa Rashid "snake Boy" Matumla wakati ule akiwa kwenye kilele cha uchezaji wake? Matumla akapewa na "pass" ya VIP uwanja wa ndege na sasa sina hakika kama kuna kiongozi anayekumbuka aliko. Sina tatizo na mapokezi na sina tatizo na namna ambavyo viongozi wa serikali wanajitoa kuwapongeza wachezaji na watu mbalimbali wenye kuonesha kufika kilele cha mafanikio yao. KINACHONICHEFUA ni namna ambavyo SERIKALI inakurupuka na kuandaa mapokezi na dhifa na sherehe na hotuba za kuwapongeza wenzetu wanaofanya vema ilhali inapuuza mazingira yanayowawezesha kufika walipo.
Hatukusikia SERIKALI ikijihusisha na maandalizi ya Rashid Matumla ila tukamuona Waziri Mkuu Sumaye akimnyanyua mkono kwa mbwembwe zoote na bendera kuubwa. Hatukusikia serikali ikimsaidia Thabeet (alipokuwa akisaka njia ya kumfikisha alipo) kufikia ndoto zake lakini leo hii, lakini sasa hivi mpaka Rais anamuandalia chakula kumpongeza.
Sijui kwa wasomaji wangu, lakini nimechoshwa na siasa katika maisha ya watu (hasa ambapo hazistahili). SERIKALI ilistahili kushikwa aibu kwa mafanikio BINAFSI yaonekanayo miongoni mwa watu wake na ilistahili kujua ni wapi pa kuanzia kuwekeza. Inaoshindwa kuwahudumia wananchi wake kwenye shida, isijitokeze kwenye raha.
WATU WAMELIA SAANA KUHUSU WIZI UNAOENDELEA AIRPORT LAKINI HAJATUMWA MWAKILISHI NA SASA ANAKUJA NYOTA TUNAMUONA. Kwanini tusikae chini na kupanga program nzuri itakayowawezesha wale wengi wenye ndoto kama za hawa tuwapongezao kuzifikia? Haihitaji akili za ziada kujua hili. Najiuliza meengi kuhusu TANZANIA YANGU. Ni kwanini haiwekezi katika kupata itakayo? Labda niwakumbushe swali alilouliza Freddie McGregor alipowauliza viongozi kuwa "why dont you set the program, so the youth can work and survive. So that they can better themselves and show some progress in their life, teach the youth the positive things and make them realize, no shooting, no looting, bring back the LOVING and where did we go wrong? Msikilize hapa chini
JUMATANO NJEMA
Picha: Kutoka kwa Michuzi & Darhotwire

8 comments:

Anonymous said...

HII SERIKALI YA TANZANIA SIELEWI KABISAA NADHANI WANAJIPENDEKEZA,ENZI HIZO JAMAA ANGEAMBIWA APIGE BOOK NAWANGEMKATISHA TAMAA,HILO SI KITU ,HASHIMU ATAKUWA NA URAIA WA MAJUU KAMA WENGI WETU JE HII SERIKALI IKO TAYARI KUTUPA DUAL CITIZENSHIP.HASHIMU NI MMAREKANI BONGO COMES 2ND HATA KAMA ASILIA YAKE NI BONGO NASEMA HIVI KWA SABABU SERIKALI YETU NDIO ONATUAMBIA HIVYO INAPOKATAA KUTUPATIA DUALCITIZEN KWA KISINGIZIO CHA WAHINDI THAT NON SENSE

Simon Kitururu said...

Hoja hii Umemaliza Mkuu sina chakuongezea na nakubaliana nawe 110%!

Yasinta Ngonyani said...

Tupo pamoja Mubelwa kwani ulichosema ni kweli kabisa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

labda hoja hii isambae kabisa kwenye magazeti na vyombo vya habari ili hata wale wasiona uwezo wa kufikia blog walione.

ni kweli hatunajuhudi za kutafuta vipaji na vijanawetu wanamasikinikanavyo.

Faith S Hilary said...

Imekuwa kama wale marafiki, wakati wa shida hawapo ila ukipata basi marafiki wakubwa. Anyway maybe that's the way it is...but I agree with you kaka.

Faustine said...

Hoja nzuri..Sasa hivi huyo Rashid Matumla anapigana mapambano ya "mchangani' kupata tulaki ili kuganga njaa. Taifa limeshamtupa na kumsahau.
Tunapenda kuvuna tusipopanda.Mapokezi ya Thabeet ni mfano mzuri wa hili.

Tmark said...

Pesa zote wanajilimbikizia wao na watoto wao,unafikiri watataka kujua issue za wananchi? Saisa zao zimejaa usanii
Ila mwisho wao utafika tu.

Tmark said...

Wezi wakubwa wanatuibia pesa zetu na pia wanatuibia na akili zetu.
Wasanii wakubwa hasiojua siasa