Showing posts with label Nawaza kwa sauti. Show all posts
Showing posts with label Nawaza kwa sauti. Show all posts

Saturday, March 10, 2012

Mawazo ya sauti (I).....OMBI

Mmoja wa marafiki zangu wa Facebook alileta OMBI kuwa nikusanye yale NIWAZAYO KWA SAUTI na kutoa mkusanyo wa kijitabu. Sikuamini kama nimeshawaza vya kutosha kiasi cha kukusanya "kijitabu". Kisha akasema "basi yakusanye na kuyaweka mahala pamoja ambapo tunaweza kuyarejea kwa pamoja".
Nimeona nifanye hivyo hapa, kwani wapo WASOMAJI WANGU WAPENDWA wasio wanachama ama marafiki zangu kulee facebook.
Na haya yafuatayo ni baadhi ya MAWAZO YANGU YA SAUTI ambayo nimekuwa nikiwaza kwenye status zangu za Facebook.
KARIBU


Ndoto na UFUNUO ni matokeo ya matendo yako. Ukiota na usifuatilie ama usione kikitokea utaita ndoto. Ukiamka na kufuatilia kisha ukafanikiwa utaita UFUNUO. Yawezekana kila UFUNUO ni NDOTO ILIYOFANYIWA KAZI hivyo ushauri wangu ni kuwa UKIOTA KILICHO CHEMA, AMKA, NENDA KATENDEE KAZI. Utaifanya kuwa UFUNUO. Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
Nawaza kwa sauti tuuuu!!!!

Furaha ni "akiba" ya sikitiko lijalo na vivyo hivyo ni kinyume chake. Azaliwapo mtoto furahi ukijua kuwa yeye ama wewe utakufa (hapo mtasikitika) mkiamini kuwa (kama mlitenda wema) mtakutana mbinguni (mkifurahi). Ajaye huondoka na pengine huja tena. Tenda wema ili mwisho wa "mzunguko" huu, uwe mwenye furaha.
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!

Ni kwanini twaiita BIMA YA MAISHA ilhali hatuwezi kukusanya mafao yake mpaka baada ya kufa? Ni kweli twastahili kuiita "Life insurance"? Ama ni "post-life insurane" au tuwe wazi kuiita "Death Insurance"? Aaaaah!!
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!

PARADOKSI YA JAMII YANGU....Leo hii "nyuma ya kisasa" ni ile yenye game room na gym badala ya study room. Mji wa kisasa ni ule wenye clubs na bars nyingi badala ya Maktaba..... Na bado twasema twataka kujenga jamii bora yenye kuthamini elimu.
Nawaza kwa sauti tuuuu!!!!!

UPDATE: Mpango wa kuwapiku waMarekani, Urusi, Japan na wengineo kwenye mambo ya "space" unaendelea vema. Tunapanga kwenda JUANI na tumegundua kuwa ni lazima tutue kule USIKU. Tuna-calculate take-off time ili tu-land USIKU. Kama kuna volunteer awasiliane nami...
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!

PARADOKSI YA TANZANIA YANGU: Leo hii tuna wanasiasa ambao wanasema kuipiga vita rushwa ni mpaka wawe kwenye uongozi na uongozi huo hawaupati bila kutoa rushwa. Ina maana wanastahili kutoa rudhwa ili waweze kupata nafasi ya kuipinga rushwa. Swali ni kuwa WATAPINGAJE RUSHWA IKIWA NI LAZIMA WAITUMIE KUFIKA NAFASI ZA KUIPINGA?
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!!

Tatizo la kumuelimisha mtu anayedhani "ANAKUZIDI AKILI AMA WEREVU" ni kuwa kadri unapomuelimisha jinsi ulivyo sahihi, yeye anazidi kujidhihirisha kuwa hauna akili hata za kutambua kuwa ana akili kukuzidi.
Hapo sasaaa.
Hatakuelewa mpaka umuelimishe na ukimuelimisha anazidi kuona "ujinga" wako.
Gggggggggrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!!!!!!
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUUU

NAWAZA KUWA kazi ya mwendesha mashtaka si kusaka sababu za mshitakiwa kutenda alivyotenda, bali kumfanya mshitakiwa kuwa mwanzo na mwisho wa tendo /kosa alilotenda. Kwani wakisaka chanzo cha mtu kutenda makosa si wataishia kutomfunga wanayetaka alale jela? Na kumfunga wanayemtuhumu ni "kipimo cha ubora wa kazi zao"
Mmmmmmhhhhhhhhhhhhh!!!!!!
NAWAZA KWA SAUTI TUUU!!!!!!!!!!!!!

Hivi wajua kuwa UEREVU WA WENGINE WAONEKANA AMA KUSIFIKA KUTOKANA NA UJINGA WAO? Yaani wanaonekana kuwa na akili kwa kuwa hawana akili za kuwaza akili. Wanaonekana watiifu kwa kuwa ni wanafiki na wenye kupendwa na wakubwa wa kazi zao kwa kuwa ni wasaliti.
Labda WANA AKILI KWA KUWA HAWANA AKILI.
Ggggggrrrrrrrrrrrr!!!!!!!
Nawaza kwa sauti tuuuuu!!!!

NIMEFUNZWA kuwa HUWEZI KUMSHINDA ADUI YAKO MPAKA UMPENDE.
OK!!!!! Nililoelewa ni kuwa unastahili kumpenda adui ushindanyaye naye, na ukishampenda ina maana hatakuwa adui kwako na akishakuwa MPENDWA KWAKO, hamtashindana kwa nia mbaya, bali MTASHIRIKIANA.
NAKUBALIANA NAYO....... Wewe je?
Nawaza kwa sauti tuuuu....!!!!!!

Mtu anayetaka kuzuia maendeleo ya mwenzake ni yule anayejitahidi kumfanya mwenzie abaki ktk kiwango cha chini. Tatizo ni kuwa ukitaka abaki, itabidi umshikilie pale. Yaani nawe ubaki ambapo unataka usiyempenda abaki. Hivyo, aliyefanikiwa kuzuia maendeleo ya mwenzake ni yule ambaye naye hataendelea akijaribu kumzuia mwenzake. Ina maana afanikiwaye kumzuia mwenzake anakuwa kajizuia na mwenyewe.
Nawaza kwa sauti tuuu!!

Nimefunzwa kuwa KUONGEA NI KAMA MTIHANI. Kabla ya kuanza una maksi zote lkn uanzapo tu waanza jipunguzia ama kuzilinda. Na UJINGA ni vivyo hivyo, haupo kwa yeyote kama wote watakuwa kimya. Ukianza kuongea waonesha kiasi kilichomo ndani mwako.
Kwa maana nyingine HAKUNA MJINGA kama hakuna asemaye.
CHUNGA USEMACHO KWANI WAJIPIMISHA UJINGA / UEREVU WAKO
Nawaza kwa sauti tuuuuuuuuuuuuuuuu

KUIGA ni kama "bahati". Kwamba kuna "bahati nzuri" na "bahati mbaya". Yaani hata anayesema HAIGI, anaiga kutokuiga. Na pengine kutokufanya upende kuiga ni kuiga waliokataa kuiga. Ina maana hakuna asiyeiga japo yawezekana wapenda uigaji wako zaidi ya wa mwenzako.
Kwa kuwa sote twaiga, basi thamini "igo" lako, hakikisha haliathiri wasiolipenda na endelea KUHESHIMU WAIGAO USIYOIGA
Nawaza kwa sauti tuuuuu!!!!

ISOME, IWAZE NA HATA MAONI TOA KIMOYOMOYO.
WanaHistoria wanasema ilichukua miaka milioni kadhaa kwa nyani kugeuka mtu.
Ok!
Sasa kama miaka iliendelea kuongezeka na nyani waliendelea kuwepo, kwanini hatuoni nyani wapya wakigeuka watu kila miaka yao milioni kadhaa itimiapo tangu wawepo?
Nawaza kwa sauti tuuuuuuuuuuuu!!!!!

"Maisha huku hayafai. Nifanyie dili nije huko."
Nauliza "kisichofaa ni kipi hasa?" najibiwa "hakuna dili kabisa. Kila kitu chapanda bei. Huku sio mahala pa kuishi wala kuendesha maisha"
Nauliza "kwanini vinapanda bei?" najibiwa " wazungu na wachina wanakimbilia huku. Viwanja na nyumba za kukodi zinapanda bei? Wanafungua biashara kila mahali"
Nawaza..Kama hawa wanakuja huko, na wewe unasema hakuna dili, wamefata nini?

OK!!
"Wataalamu" wanasema addiction iliyo kuu ni watu kuwa ONLINE kwa muda mrefu. Na wana ushahidi kwa kuwa wamekuwa wakikaa online kuangalia watu wanavyokaa online na sasa wamehakikisha kuwa hilo ni tatizo. Kwanini wao wasijione ma-addicts pia? Siku hizi wezi wanapata pesa kwa kuwasaka wezi, wala rushwa wanawavumbua wala rushwa na addicts wa PC wanasema wanakaa kuchunguza addicts wa PC.
Nawaza kwa sauti tuuuuuu!!!!!

u-CHANYA wa u-HASI wao.
Atunzaye siri apendwa japo afanya hivyo kwa kuwa HAMUAMINI yeyote.
Asiye tegemezi apendwa japo afanya hivyo kwa kuwa HAAMINI kama kuna wa kumfanyia apendayo.
Aliye jasiri apendwa japo afanya hivyo kwa kuwa HAAMINI kama kuna haja ya kutegemea kwingine.
Apendaye apendwa japo afanya hivyo kwa kuwa HAAMINI kama wengine... watambua THAMANI YA UPENDO
TUPENDE U-HASI KWANI NDIO ULETAO U-CHANYA WETU
Nawaza kwa sauti tuuuuu!!!!

MASWALI MENGINE BWANAAA..
Bosi wangu ananiuliza "ni mara ngapi mawazo yako yame-concentrate 100% ktk kazi?" namwambia SIKUMBUKI.
Ati anakasirika na kuuliza KWANINI?
Namwambia "nikiwaza 100% katika kazi, sina % ya ziada kuwaza kuwa nime-concentrate 100% katika kazi. Na nikishawaza hata kwa 0.001% kuhusu concentration yangu ya kazi, ina maana sina 100% kazini."
Akacheka na kuondoka.
NIKAMUULIZA KIMOYOMOYO...UNANITEGA?

NDIO... Kuna JUU.
Na JUU yaweza kutokuwa ile JUU uliyokuwa ukiiota na kuitamani. Na pengine JUU ya "hadhi" sio ile JUU ya "kipato" ama hata ya "utekelezaji"
NA katika JUU hiyo, bado kuna "kati" na "chini".
BASI USHAURI WANGU NI KUWA....
Kama huko JUU hauko JUU, basi shuka CHINI ili uwe JUU....
Hivi naeleweka????
NAWAZA KWA SAUTI TU!!!

NAWAZA faida za "kinyumenyume"
Yaani HUJUI kuwa ulilala mpaka utakapoamka. Usipoamka....meet you in zion
Hujui USAHIHI mpaka utakapoona MAKOSA.
Huoni MAENDELEO mpaka ujue asiyeendelea ama kisichoendelea kilivyo.
Hutoitambua DHAMBI mpaka ujue upande wa pili wa kile uitacho dhambi.
Kwani unaamini HAKUNA FAIDA ya upande uuitao m'baya ambao kwa "kuukimbia" kunakufanya uonekane "mwema" na "mtakatifu"?
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUU!!!

MAFANIKIO
Ni kitu cha ajabu na TATA kwelikweli.... Kwa sababu
-Kila mtu hukiomba japo si kila akiombaye anataka kukitumia kwa wema ama lililo jema
-UFANISI wa wengine ambao wanasema WAMEFANIKIWA ktk watendayo kwaikwaza ama kuiadhibu jamii.
-Ili UFANIKIWE kumkamata ALIYEFANIKIWA kufanya yasiyo mema, ni lazima MAFANIKIO yako yazidi MAFANIKIO yake japo wote mwafanikiwa katika mambo yanayopingana.
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUUUU!!!

We (human beings) lives in the world of "delayed-now".There is no such a thing called THIS MOMENT because from the moment you think of it to the time you say it, it's not "THIS moment" anymore. May be "that-this moment". Hahahahahahaaaaaaaaaaa
Just THINKING OUT LOUD!!!!!!

CHOO....Labda ni jina tu kulingana na matumizi, kwani kulingana na uhitaji chaweza kuwa chumba na chumba ama sebule kuwa choo.
NAWAZA KWA SAUTI TUUUU!!!!!!

Labda UONGO ni UKWELI usio sahihi kwa wakati usemwao
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUU!!!

Thursday, January 12, 2012

UELEWA WA KUELEWA UELEWA

Kutokana na kuombwa na msomaji wangu aliyeiona kwenye ukurasa wangu wa Facebook, nimeona ni vema kuihamishia hapa ili kwa wale kina nanilii wasio kule wapate kuchanganua hili.
Nimeiboresha kidoogo kwa kuongeza sehemu ya maoni yangu katika hili.
TRUST ME. INAELWEKEA. Ilaaa.....UTAELEWA HAPA UKIELEWA UELEWA WA UELEWA WAKO KWANZA...
Ok......
UnaELEWA nini kuhusu kuELEWA? Tatizo ni kuwa ni lazima kuELEWA kuwa unaELEWA, ingawa kuwa muELEWA wa kuwa unaELEWA waweza kuhitaji uELEWA.
Yaani ninajiuliza hapa ni kama unatambua kama unaELEWA mwanzo wa uELEWA ulio ndani mwako?
Na vipi unawaELEWA wale wasiokuELEWA ambao wanaamini wanakuELEWA unavyoELEWA ilhali nawe waELEWA kuwa uELEWA wao si sahihi?
Labda hakuna anayeELEWA uELEWA wa wengine maana lazima utumie uELEWA wako kupinga ama kukubaliana na uELEWA wa mwingine ambaye yawezekana uELEWA wako wakueleza kuwa HAELEWEKI.
Hiviii.... kipi chanzo na / ama kipimo cha kuELEWA?
Kumbuka kuwa hutaELEWA kuwa unaELEWA hili kama hutaELEWA ninachoELEWA ama kutoELEWA uELEWA.
Kuna kuELEWA kwamba unaELEWA.
Kuna kuELEWA kwamba huelewi.
Kuna kuELEWA kwamba hueleweki.
Kuna kuELEWA kwamba huelewi kuwa hueleweki ambako kunaeleweka kwa asiyeelewa kwanini huelewi.
Kuna kuELEWA kwamba unaelewa japo huelewi kwamba unaloelewa halieleweki.
Kuna kutoelewa kwamba unaelewa kisichoeleweka.
Na huku kote twatendwa na watu na watu hawa wote SIWAELEWI
Labda sijielewi na ndio maana utaniELEWA ama hutaniELEWA.

Na kinyume chake ni sahihi?

UmeniELEWA?

NAWAZA KWA SAUTI TUUU!!!!!!!!!!!!

Sunday, December 11, 2011

Elimu ya Uhuru, uhuru wa elimu na elimu huru

SIKUISAHAU "SIKU KUU" HIINilikuwa nasubiri wamalize hii HANGOVER ya "mapato na matumizi" ya SHEREHE HIZI kisha wakishakuwa "sober" tuje kujadili namna ambavyo tutaoanisha ELIMU na UHURU.
Kama nilivyosema katika status yangu hukooo "usokitabu" na nairejea hapa chini.....
MIAKA 50 YA UHURU..........
Tunalohitaji ni MWALIMU wa kuwafuata wale waliopanga haya mashamsham ya uhuru kuhusu MIAKA 50 YA ELIMU YA UHURU ili waujue UHURU WA ELIMU na baada ya hapo wapewe ELIMU HURU ya kuwa HURU KIELIMU kuweza kuleta maendeleo nchini.
NAWAZA KWA SAUTI TUUUU!!!!!!

TUKUTANE "NEXT IJAYO" TUTAKAPOJADILI HILI.

Tuesday, December 6, 2011

Labda UNYOOFU si suluhisho la kutufikisha kila tunakotaka kwenda......

.......... japo twatumia unyoofu kama kielelezo cha kuelekea mafanikioni.Labda waTanzania tu-wanyoofu saana ilhali Tanzania yetu imeshapinda. Ndio maana ni kama twaendesha ki-ajali ajali
Labda Rais Kikwete yu-mnyoofu ilhali serikali na Tanzania yake imepinda. Ina maana hatatufikisha
Labda twajitahidi kuwaza ki-nyoofu ilhali suluhisho la mawazo hayo tayari limepinda. Ndio maana matokeo ni kutofika tutakako
LABDA HATUWAZI KULINGANA NA MAZINGIRA NA LABDA ILI TUSONGE MBELE, TWAHITAJI DEREVA ANAYEONA BARABARA IMEPINDA NAYE AKAPINDA KULINGANA NA BARABARA HIYO ILI TUFIKE TUENDAPO.
NAWAZA KWA SAUTI TU!!!!!!!

Sunday, November 20, 2011

Ndoa vs Harusi

NDOA vs HARUSI.
Mahusiano yake ni madogo sana (kama yapo) na pia mafanikio ya moja kati ya hayo hayana AKISI ya moja kwa moja kwa jingine. Tofauti baina yake ni kubwa kuliko inavyochukuliwa na umuhimu wa elimu juu ya uelewa wake ni zaidi ya inayotolewa.
Nilielezwa kuwa HARUSI ZOTE ZAFANANA JAPO KILA NDOA NI YA KIPEKEE. Na kuwa waweza kuwa na ndoa bila harusi na harusi isiyo na ndoa ya kweli.
Labda ni wakati wa kuangalia vema na kuwekeza katika NDOA na si HARUSI kama ilivyo kwa wengi hivi sasa.
Unaamini kuwa mafanikio ya ndoa yanategema (kwa namna yoyote ile) maandalizi ya harusi?
Unaamini kuwa mafanikio ya HARUSI yanaweza kuwa na ishara yoyote juu ya mafanikio ya ndoa?
Unaamini kuwa HARUSI yaweza kuwa chanzo cha mvurugano wa NDOA?
Kwanini tuwe na NDOA na HARUSI kama uhusiano wake waweza kutomaanisha lolote kwa pamoja?
Kwani NDOA NA HARUSI NI UTASHI AMA "MFUMO"
Nawaza kwa sauti tuuuuu!!

Labda hatuendelei kwa kuwa "wa kutuendelesha" hayuko kwenye "kiendelesheo" chetu

MAREJEO YA FEB. 3, 2011
Photo Credits:Jimmy Falon Blog
Natambuwa kuwa TUNA TAFSIRI TOFAUTI ya neno ama kitu MAENDELEO. Lakini haijalishi unatafsiri vipi, tutakubaliana kuwa SI KILA MABADILIKO NI MAENDELEO JAPO KILA MAENDELEO NI MABADILIKO.
Na kwa sehemu yoyote iliyo na maendeleo, utagundua kuwa ni wachache wafanyao maamuzi yanayoleta maendeleo hayo na ambao wakati mwingine wakati wafanyapo haya, hupuuzwa (kwa kuwa wengi wetu husita kubadilika). Kwa maana nyingine ni kuwa kwa maendeleo yoyote kufanyika, ni lazima wale wachache (ambao mara nyingi wamepewa ama kujipa dhamana) wanatakiwa kuwa makini katika kufanya maamuzi yao kwa manufaa ya nchi na wananchi.
Hawa (wafanya maamuzi) wanapokuwa na mtazamo mwingine, wanapokuwa wanawaza vingine, wanapojiweka katika ngazi ama hatua nyingine na wale wanaostahili kuwa nao, hawawezi kufanya maamuzi yawafaao kwa kuwa HAWANA MAHITAJI YAFANANANYO NAO. Kwa hiyo maendeleo kwao ni tofauti na maendeleo kwa wawaongozao.
Na ni hapo tunapokuja kuona mifano kadhaa.
1: Maendeleo yetu ni pamoja na KUTHAMINIWA.
Lakini tunaona namna ambavyo thamani ya mTanzania inavyokuwa kulingana na uajiri alionao, ama mahusiano kati yake na wakubwa mahala fulani. Hivi majuzi tumesikia habari ya WATOTO KUMI WALIOUKULIWA KWENYE SHIMO LA TAKATAKA huko Mwananyamala. Hiki kitendo kilitakiwa kupingwa na kufanyiwa uchunguzi wa hali ya juu. Hawa watoto hawakutendewa haki (hata kama walizaliwa wakiwa wafu) kwani kama viumbe na kama waTanzania, bado walikuwa na haki ya kupata HESHIMA ZOTE ZA MWISHO na kuzikwa kulingana na mila, desturi na imani za asili waliyorithi. Lakini hakuna aliyesikika akionekana kuwekeza ktika KUWAJIBISHA WATAKAOBAINIKA KUTENDA KITENDO HIKI CHA FEDHEHA.
Hawa walikuwa na bado ni waTanzania. Hazikuwa TAKWIMU. Hivi majuzi walipouawa watu Arizona tuliona Rais wa Marekani akienda kufariji.. Labda Rais wetu alikuwa "busy", lakini ni lini wanaotenda makosa kama haya wamewajibishwa?
Labda "waendeleshaji" wetu hawako kwenye "kiendelesheo" cha UTU NA THAMANI YA MTANZANIA kwani wangekuwa huko, wangemtafuta mhusika na kumuadhibu. HAWA WATOTO HAWAKUJIZIKA.
2: ADHA YA MIUNDOMBINU
Hakuna ubishi kwamba viongozi (ama niseme WATAWALA) hawatumii aina ya miundombinu tunayotumia sisi. Niliwahi kuandika kuhusu BARABARA ZETU (irejee hapa) , na mara kadhaa nimezungumzia suala la AJALI (rejea hapa). Haya yote licha ya kuwa yanachangia kuondoa nguvukazi ya jamii na kuzorotesha maendeleo ya nchi, WAHUSIKA HAWAJALI kwa kuwa wao si watu walio katika mfumo wetu wa maisha. Wakati sisi "tunalia" na foleni katikati ya jiji, wao wanafikiria kuanzisha huduma za helikopta za kukodi (as if zitamfaa aliye Mbagala ama Gongo la mboto ambaye ndiye mwenye uhitaji mkubwa wa kuondokana na foleni). Hawasafiri kwa barabara tupitazo sisi kwenda vijijini na ndio maana HAWAONI UCHUNGU NA ADHA YA UBOVU WAKE.
Siamini kama WANAPATA MGAO tunaosikia kila siku kwa ndugu zetu, na ndio maana hawana "LADHA HALISI" ya tatizo la kukatika kwa umeme. Hawatumii "line" za maji tutumiazo sisi, na ndio maana mabomba yao yakitoa maji masaa 24, hawajui kuwa kuna yanayomaliza miezi (kama sio miaka) bila kupitisha unyevu ndani mwake.
NI KWA KUWA HAWAKO KWENYE MIUNDOMBINU YETU, HAWAJUI ADHA ZETU.
3: ADHA YA HUDUMA ZA JAMII
Labda wangekuwa wanatibiwa atibiwako bibi yangu, ama kupata chakula apatapo mpwa wangu. Lada wangekuwa wanatambua adha hizi. Labda watoto wao wangesoma tuliposoma sisi wangethamini mazingira ya shule zetu, na labda wangekuwa wakikaa mahabusu wakaazo "wasingiziwa" wengine wangejua haki ya mtuhumiwa (kuwasi mkosaji mpaka atakapokutwa na hatia na mahakama)
Lakini kwa kuwa wao hupata dhamana hata kama kosa lao ni kubwa, kwa kuwa wao ksi zao huenda mwendo kasi, kwa kuwa wao hutibiwa nje, hufunga barabara waendapo vijijini, husafiri kwa ndege, husomesha nje ya chi, HAWAJUI MAHITAJI YETU KWA KUWA HAWAKO KATIKA NGAZI MOJA NASI.
Na haya ni machache ambayo yananifanya niingie katika sehemu hii ya tatu nikiwaza kuwa Labda hatuendelei kwa kuwa "wa kutuendelesha" hayupo kwenye "kiendelesheo" chetu
NAWAZA KWA SAUTI TU!!!!!!

Sunday, October 2, 2011

Chemsha bongo...Unaona nini?

Hii ilistahili kuungana na POST moja ijayo, lakini wacha niiweke hapa nanyi MTAFUNE (mfikirie) nami badala ya mimi "KUTAFUNA" peke yangu wakati wa kuiandika.
Dadangu B.M (love you plenty) kaiwazisha akili yangu kwa sauti juu ya taswira hii hapa chini. Ati wewe unaona tatizo gani kwenye picha hii? Ama ni DHIHAKA gani iliyomo humu? Kumbuka, ni "banner" kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya UHURU WA tanzania BARA.
Ukitaka "kugandamizia" soma hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/12/tanzania-yanguisherehekeayo-uhuru.html ama http://changamotoyetu.blogspot.com/2011/07/tanzania-yanguna-dhihaka-ya-kuwaenzi.html
TUWAZE KWA SAUTI, TUWAZE KWA PAMOJA

Thursday, September 22, 2011

Upendo kwa nchi

UPENDO KWA NCHI ni jambo TATA SANA. MJINGA yule ANAIPENDA SANA NCHI YAKE kiasi kwamba hataki iingie kwenye machafuko, hivyo ANAVUMILIA UPUMBAVU wa mtawala wake. MTAWALA yule ANAIPENDA SANA NCHI YAKE kwa kuwa anafanya atakalo, ANAIBA ATAKAVYO na HAKUNA WA KUMUWAJIBISHA. Najua viongozi wetu wanaipenda Tanzania. Hata kama wanaipenda kwa kuwa HAWAWAJIBISHWI KWA MATENDO YAO.
Nawaza kwa sauti tuuu!!!