Thursday, January 12, 2012

UELEWA WA KUELEWA UELEWA

Kutokana na kuombwa na msomaji wangu aliyeiona kwenye ukurasa wangu wa Facebook, nimeona ni vema kuihamishia hapa ili kwa wale kina nanilii wasio kule wapate kuchanganua hili.
Nimeiboresha kidoogo kwa kuongeza sehemu ya maoni yangu katika hili.
TRUST ME. INAELWEKEA. Ilaaa.....UTAELEWA HAPA UKIELEWA UELEWA WA UELEWA WAKO KWANZA...
Ok......
UnaELEWA nini kuhusu kuELEWA? Tatizo ni kuwa ni lazima kuELEWA kuwa unaELEWA, ingawa kuwa muELEWA wa kuwa unaELEWA waweza kuhitaji uELEWA.
Yaani ninajiuliza hapa ni kama unatambua kama unaELEWA mwanzo wa uELEWA ulio ndani mwako?
Na vipi unawaELEWA wale wasiokuELEWA ambao wanaamini wanakuELEWA unavyoELEWA ilhali nawe waELEWA kuwa uELEWA wao si sahihi?
Labda hakuna anayeELEWA uELEWA wa wengine maana lazima utumie uELEWA wako kupinga ama kukubaliana na uELEWA wa mwingine ambaye yawezekana uELEWA wako wakueleza kuwa HAELEWEKI.
Hiviii.... kipi chanzo na / ama kipimo cha kuELEWA?
Kumbuka kuwa hutaELEWA kuwa unaELEWA hili kama hutaELEWA ninachoELEWA ama kutoELEWA uELEWA.
Kuna kuELEWA kwamba unaELEWA.
Kuna kuELEWA kwamba huelewi.
Kuna kuELEWA kwamba hueleweki.
Kuna kuELEWA kwamba huelewi kuwa hueleweki ambako kunaeleweka kwa asiyeelewa kwanini huelewi.
Kuna kuELEWA kwamba unaelewa japo huelewi kwamba unaloelewa halieleweki.
Kuna kutoelewa kwamba unaelewa kisichoeleweka.
Na huku kote twatendwa na watu na watu hawa wote SIWAELEWI
Labda sijielewi na ndio maana utaniELEWA ama hutaniELEWA.

Na kinyume chake ni sahihi?

UmeniELEWA?

NAWAZA KWA SAUTI TUUU!!!!!!!!!!!!

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kuelwa uelewa wa mwingine kwa kweli ni kazi kubwa sana. Mara nyingi huwa ni kutoelewana na mwishowe ni ugomvi na kutoelewana ..duh! hapa naona ku-ELEWA zilikuwa nyingi mno sijui kama nina uelewa/elewa

Rachel Siwa said...

Hahahahhaha da'Yasinta Umelewa ya kueleweka na mwingine anaweza asikuelewe wewe ulivyoelwa,nami sijui kamanimeelewa yaliyo elewehswa na waelewa!!!!!!!kaka wa mimi kwa Mistari ya Uelewa unanilewesha!!

Rachel Siwa said...

Duuhh mpaka nimechapia sehemu nyingi tuu kwakuelewa au kutoelewa tehtehteh mtaelewa tuu,mbarikiwe wooooooteee