Wednesday, October 7, 2009

Mechi ya kwanza ya Hasheem Thabeet NBA......MAFANIKIO

Hasheem ndani ya "uzi" wa Memphis Grizzlies.
ANGALIZO. Hiyo si "tatoo", ni maandishi juu ya picha toka www.memphisbluebears.com
Hasheem Thabeet, usiku wa kuamkia leo alifungua pazia la kushiriki mechi ya kwanza ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA pale alipoichezea timu yake ya Memphis Grizzlies dhidi ya Washington Wizards katika mechi ya kwanza kati ya mapambano ya kujipima nguvu kabla ya kuanza rasmi kwa msimu wa 64 wa ligi ya NBA utakaoanza rasmi Oktoba 27 2009 na kumalizika Aprili 14 2010. Katika mechi hiyo ambayo Wizards walishinda 101-92, Hasheem alionekana kufanya vema kwa kuweza kufunga pointi 6 na kuzuia mitupo 4 ndani ya dakika 15. Huu si mwanzo m'baya kwa Hasheem ambaye alikuwa chaguo la pili kwa thamani katika draft ya NBA na sasa ameanza ngwe nyingine ya UCHEZAJI WA KULIPWA katika mpira wa kikapu.


Kila la kheri Hasheem

3 comments:

Koero Mkundi said...

SAFI SANA KAKA KWA HABARI HII...

Yasinta Ngonyani said...

Nakutakia kila la kher Hasheem maana ni safari ndefu najua utafanikiwa tu na Mungu atakuwa nawe daima.

chib said...

Kila la heri Hasheem, tunafuatilia maendeleo yako. Peperusha bendera ya Afrika hukooo