Saturday, March 28, 2009

"Balozi mdogo" anayefanya vema kuitangaza nchi


Mabingwa wa NCAA kanda ya Magharibi UCONN
Namwita "balozi mdogo" mwenye kuitanganza nchi kwa kasi, basi naamini anafanya kazi njema kwa sasa. Namzungumzia Hasheem Thabeet, kijana ambaye macho ya wengi katika michuano hii ya vyuo inayoelekea ukingoni yamemwelekea yeye.
Muda si mrefu wameshinda Ubingwa wa NCAA KANDA YA MAGHARIBI na kwa wale wafuatiliaji watakubaliana nami kuwa sasa Hasheem amewalazimisha wapendao mchezo kumuangalia, kisha kujiuliza kuhusu Historia yake na kisha kuweza (kwa lazima ama hiari) kuitambua ama kutambua uwepo wa Tanzania.
Mfano mzuri ni hayo maelezo ya picha yaliyo katika moja ya mitandao mikubwa ya michezo ulimwenguni wa ESPN Connecticut's Hasheem Thabeet, of Tanzania, yells in celebration after their 82-75 win over Missouri in a men's NCAA college basketball tournament regional final in Glendale, Ariz., Saturday, March 28, 2009. (AP Photo/Chris Carlson)

Hasheem amepitia changamoto nyingi kuanzia kukashfiwa na baadhi ya waTanzania kwenye baadhi ya mitandao, kashikashi za kujibidiisha kuwa katika kiwango alichopo, kucheza achezavyo na kisha kutwaa Tuzo ya mchezajibora-mwenza wa mwaka wa Big East na mlinzi bora.
Ni CHANGAMOTO YETU sote si kumpa ushirikiano, lakini kusaidiana naye kujua ni vipi ameweza kufikia alipo maana najua ni wengi wenye kipaji na uwezo kama wake walio nchini lakini hawajui njia sahihi ya kufika alipofika yeye.
PONGEZI KWAKO HASHEEM. KUMBUKA KUWA KILA HATUA UPIGAYO NI MWANZO WA NYINGINE ITAKAYOKUFIKISHA KATIKA KIWANGO, KIPATO NA HESHIMA KUBWA ZAIDI. BIDII NA IMANI VITAKUFIKISHA UTAKAKO
PONGEZI KWA WATANZANIA WALIOJUMUIKA NA MAMAKE KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA WAKIMSHANGILIA KAMA AMBAVYO WALIONEKANA MARA KADHAA LUNINGANI.
Nasi wana changamoto blog tutajitahidi kwa kina kutekeleza sehemu ya jukumu hilo kufanikisha nia hiyo
Kwa picha zaidi za mchuano huo, Bofya hapa

1 comment:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Mimi nasubiri Wakenya watakapoanza kudai kwamba Hashim anatoka Kisumu....