Thursday, August 20, 2009

Ati nini???? Anapimwa kujua kama ni MSICHANA KAMILI??

Kweli kuna ya Musa na Firauni. Na unapodhani umeona yote, ujue kuna mengine ya kujifunza.
Binti wa miaka 18 toka Afrika Kusini Caster Semenya (pichani juu) ambaye ameshinda KWA KISHINDO mbio zinazoendelea za mashindano ya dunia huko Ujerumani, anaelekea kulazimika KUFANYIWA UCHUNGUZI KUONA KAMA ANA SIFA ZA KUMFANYA ASHIRIKI MICHUANO HIYO UPANDE WA WANAWAKE.
Sina utaalamu na hili na nisingependa kujaribu kutafsiri (kwa kiingereza changu cha ugoko) labda nikueleze kuwa HABARI KAMILI IKO HAPA
Ila huyu mdada ni kiboko. Hebu muangalie hapa chini (unaweza kuanzia dk 2:15) ama "alivyowafunga tela" kuanzia dk ya 4. Nisichojua wanafanya tests ngapi, wanazifanyaje na pia sijui ni nani anayeweza kwenda kwenye michuano hiyo tena AKIIWAKILISHA NCHI akiwa na jinsia tofauti na ashindanao nao. Kama nilivyosema, lazima mmoja aonekane kituko. Wanaotaka apimwe ama yeye (kulingana na majibu yatakavyokuja)
AMA KWELI TUMEUMBWA KATIKA MIILI NA MAWAZO TOFAUTI
Mtazame hapa chini

6 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sijui watapima niini

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kuangalia kwa haraka haraka ni kweli ana umbile la kiume na pia anavyokimbia. Liakini inawezekana watu tumeumbwa tofauti. Au labda alikuwa mwanaume na umebadili na kuwa mwanamke ....Lol

Born 2 Suffer said...

Kweli anaumbile la kiume ukiona lakini wamshakie hivyo tena mpaka apimwe, wadhungu wameshaona katika hii michezo washindi wakubwa ni waafrika watu weusi inawauma wanatafuta kila aina ya sababu sasa, angekua mweupe ana kutoka kwao au hata ni mweusi lakini wa kwao wasingeshakia.

Anonymous said...

sasa hapao wanapima nini kweli hata mimi nashindwa kulewa mmh lakini hebu ngoja tuwape nafasi ya kumpima, hawakawii kusema alijibadilisha maana na hizo round about duh kama men ha ha ha haya bwana tunangoja matokeo

chib said...

Ni kweli umbile lake duh! Lakini.... Hivi walikuwa wapi kuhusiana na hilo wazo wakati kashiriki mbio zote za mchujo, sasa kushinda tu ndio kabadilika kidume! Huyo pia mwenye mawazo hayo naye akapimwe

Faith S Hilary said...

anawezakana kuwa "intersexual" au "ambiguous genitalia" ambapo muonekano unakuwa wa opposite sex but the genitals are different. Ndio ninavyofikiria mimi because she looks and she acts like a man...