Sunday, July 12, 2009

Nyota mwingine (Arturo "Thunder" Gatti) afa na kuacha utata zaidi

Mtiririko wa wanamichezo na wasanii mbalimbali kuendelea kupoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha unazidi kuishangaza dunia. Mmoja kati ya mabondia bora kabisa kuwahi kutokea ulimwenguni Arturo Gatti amekutwa amefariki katika chumba cha hoteli huko Brazil ambapo mkewe amehusishwa na kifo chake.
Gatti ambaye anaamika kuwa mmoja wa bondia bora zaidi katika kizazi na uzito wake, aliwasili hotelini hapo na mkewe na mtoto wao wa mwaka mmoja na yasemekana kuwa kulikuwa na kutoelewana baina ya wanandoa hawa masaa machache kabla ya kifo cha Gatti. Polisi wa jimbo la Pernambuco nchini Brazil wanamshikilia mke wa bondia huyo Bi Amanda Rodrigues wakimhusisha na kifo hicho hasa kwa kuwa yasemekana wapenzi hawa walikuwa na wivu wa kupindukia baina yao.
Kifo cha Arturo Gatti kimekuja wakati kuna maswali ambayo hayajajibiwa kuhusu kifo cha nyota wengine kama Michael Jackson ambaye dadaye Latoya amekaririwa leo akisema kuwa "wamemuua kakangu" (Bofya kuisoma) na pia siku kadhaa baada ya nyota mstaafu wa Mpira wa "miguu" wa Marekani Steve McNair ambaye yasemekana "aliuawa na mpenziwe akiwa amelala" (bofya kuisoma)
Nimekuwa nikimfuatilia Gatti tangu nikiwa nafanya kipindi cha michezo pale Times Fm.
Tazama highlights ya mapambano yaliyompa heshima kubwa Arturo "Thunder" Gatti hapa chini.

No comments: