Friday, October 31, 2008

Them, I & Them. NASIO ...........No Love

Nasio Fontaine
"They talking about Love, yet they got no love at all, talking bout peace, yet all i see is war. You talk about this, you talk about that. Poor people just a suffer (are suffering) while you live out FAT"
Ni maneno toka kwake Nasio Fontaine Mmoja wa wanamuziki wa Roots Reggae ambaye amesimama imara katika kutetea haki za wanyonge, kufumbua maovu ya viongozi na watawala na kufundisha njia m'badala za kujikomboa kwa tabaka likandamizwalo.
Namzungumzia Nasio na wimbo huu No Love Ijumaa hii kutokana na yale yaliyotokea wiki hii barani mwetu. Kwanza ni mkutano wa Bunge la Afrika na pili rabsha za Congo.
Tumeona viongozi wanavyosimama na kuzungumza kuhusu amani ambayo hawaonekani kuwa na nia ya kuisaka. Wanakwenda mikutanoni kuendesha vikao vya amani wakilipwa pesa nzuri na kuota vitambi wakati amani izungumziwayo haipo na wenye uhitaji wakiendelea kutaabika na machafuko hayo. Wengine bila hata aibu wanasema mapigano hayo wanayaleta kutaka kuleta Demokrasia nchini mwao na ndio maana Nasio kwenye wimbo huu akasema "you coming with your bribes and treachery to murder in the name of democracy. You living in your false pride and Luxury, while millions (are) dying in their poverty"
Wanapoomba kura wanakuwa na ahadi mbalimbali zenye kuwapa matumaini watu. Wanaahidi yale ambayo hawawezi kutekeleza wakijua wazi kuwa maslahi yao yanatangulia mbele na ndio maana hawajali vifo na ukimbizi utokanao na yale wafanyayo. Nalo hili Nasio aliliona aliposema "The wickedman ain't got no love for humanity, yet they got so much love for their vanity. Their need for way is rising high, while the sufferers are left to die (in starvation and hunger). Vote for me i'll set you free, are lies and hypocrices"
Nawasikiliza viongozi walivyoanza fitna na majungu ya kujifanya wanachukua kila hatua kusitisha machafuko yaendeleayo barani Afrika kwa kupanga safari nono za kwenda kujadili amani isiyopatikana.
Kama alivyosema Nasio nami ndivyo niaminivyo kuwa LOVE AND LOVE ALONE WILL CONQURE na sina shaka kuwa wenye kuanzisha haya kwa manufaa yao siku yao yaja.
Pole kwa wale wote ambao kwa tamaa za viongozi wao wamejikuta wakiwa wahanga wa machafuko ya namna moja ama nyingine.

Waweza kujua mengi juu ya Nasio Fontaine kwa kubofya http://www.nasioreggae.com/main.html

BLESSINGS
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**

2 comments:

luihamu said...

amani iwe nawe kaka.

huyu ni nabii wa kweli,wale wote wanenao ya kweli ni manabii wapenda usawa na amani.

Mzee wa Changamoto said...

Nuff Respect Ras.