Monday, November 24, 2008

Ni kweli majina yetu huathiri mustakabali wa maisha yetu?


Kama maana tusomazo ndizo halisi. Basi swafi.

  Kama kweli majina huathiri maisha yajayo, basi siku saba baada ya kuzaliwa nilishasaidiwa kuchagua mustakabali (future) yangu
Unapopewa kazi ya kumtafutia mwana jina huwa unaanza na nini? Haya umeshajua jinsia kinachofuata ni nini? Historia ya maisha ya wazazi? Tukio kuu la wakati huo? Jina la wazazi wa wazazi wake ama?
Sijapata nafasi ya kuuliza hili kwa wazazi wangu kujua walikuwa na majina mangapi ya kuchagua na kwanini walifikia uamuzi wa kuniita niitwavyo na si vingine? Labda nikijua hilo na kujua kwanini wanaitwa waitwavyo itaepusha ama itanipa nafasi ya kutumia ama kutotumia majina yao kwa wanangu na ama nikiwaeleza wanangu juu ya majina yangu wataweza kujua kama kuna umuhimu wa kutumia ama kutotumia majina yangu kwa watoto wao.
Tunajua kuwa jina lako laweza kuwa chanzo cha kukosa baadhi ya itu ama nafasi. Kwani si bado tunakumbuka jinsi jina la kati la Rais Mteule wa Marekani la Hussein lilivyokuwa likitumiwa kuwatisha watu wasimchague? Lakini pia swali ni kwamba, ni kweli kuwa tabia za ndani za watu zaweza kuathiriwa na jina la mtu? Yaani kumuita mtoto SHIDA ama MATATIZO ama TABU kunaweza kusababisha awe na maisha ya hivyo? Kwani ukimuita mtoto OSAMA inampa tabia za kigaidi? Ama kumuita mwana HITLER kunaweza kumfanya awe mkatili kwa jamii fulani? Sasa mbona kuna watu wanapata watoto na kukata baadhi ya majina wakiamini kuwa watoto wao hawatakuwa watu wema wakiitwa majina hayo? Lakini pia, ni kweli kuwa majina hufanya tabia za watu zifanane? Yaani tukitafuta kina Mubelwa kama kumi kuna uwezekano tukawa na mfanano wa tabia? Ni kweli? Na kama ni kweli hufanana kwa tafsiri ipi? Mfano tafsiriya Mubelwa kikwetu ni tofauti na ile ipatikanayo kwa wanazuoni wa majina? Tumeona wengine wamezaliwa na kuitwa Obama siku ya uchaguzi wa Marekani, sijui tutegemee nini wakikua na sijui kwa utaratibu wa kuwaita majina ya babu zai itakuwaje kwa wajukuu zao kuitwa Obama bila hata kujua kwanini babu zao wameitwa hivyo. Na sina hakika kama kuitwa tu bila hata kujua maana ya jina lao (kama ilivyo kwa wengi) kunaweza kumfanya mtoto aamini maisha yake yanaenda na maana ya jina lake. Vipi walioitwa CCM? VALENTINE je? Ambaye alizaliwa tarehe 14 Februari; nami nimwite mwanangu Valentine kwa kuwa mwenye jina ni rafiki sana hata kama kazaliwa Oktoba 8?
  Well! Nimekuwa na bahati sana maishani mwangu na jina langu lamaanisha hivyo katika tafsiri ya kikwetu, lakini sina hakika kama nimeona hivyo kwa kuwa natamani iwe kweli ama ni kweli iko hivyo kwa kuwa wazazi wangu waliniita jina langu.
Hapa sina hakika kama naliona tatizo, ila bado naamini kuwa kama lipo, basi kila alionaye ataona tatizo.
Blessings

4 comments:

Anonymous said...

Sijui. Kuna msemo wa kihaya unasema eibara libi liita nyinalo. Yaani jina baya humdhuru mwenye nalo.Labda kuna kweli

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ofcourse majina mabaya huaribia wenye nayo kwa kiasi fulani kutokana na perception ya jamii lakini wakati mweingine kutokana na mwenye jina analichukuliaji au maana nyinginezo.
wazazi wengine huwapachika majina watoto wao yatokanayo na biblia bila kujua maana halisi na wengine huishia kushikwa na mapepo, kuwa wazinzi kutokana na majina eti yanayotamkika kidhungu. sitatoa mfano wa majina mabayo yatokayo kwenye bible kutokana na uwezekano wa wenyemajina hayo kutembelea hapa wasijejisikia vibaya.

nilitafuta sana maana ya jina langu la ubatizo nikagundua kuwa halinifahi na ndio maana silitumii na sio langu tena.

Yasinta Ngonyani said...

inawezakana kwani ninakotoka mimi mtoto akilia sana hasa usiku eti analilia jina kwa hiyo wanamshikia kuku na kutaja majina yote ya mababu na mabibi waliokufa. Akinyamaza katika jina lile walilotaja basi ataitwa hivyo. Na pia hii mtoto kuitwa matatizo, huzuni, shida hutokea mara nyingi kama wazazi/familia wamepatwa na jambo la kusikitisha kabla ya mtoto kuzaliwa.

hizi ni fikra zangu

Unknown said...

Kutokana na mazoea kuna ukweli juu ya hilo.
Niliwahi kufanya utafiti wakati fulani juu ya dhana hiyo, nikaja kugundua kuwa majina yamepewa nguvu kutokan na watu kuamini katika hizo imani.
Kiutambuzi jambo lolote likipewa nafasi katika jamii na kuaminiwa linakuwa na nguvu, ndio sababu ya watu wengi habudu mizimu na kwendakutambika katika makaburi kwa kuamini kwamba mambo yao yataanyooka, na hii inahusisha hata wale watu walioshika dini.
Kwa kuwa wameaminishwa kwamba bila kutambikiamizimu hakuna kufanikiwa, basi dhana hiyo inakaa kwenye ubongo wa kina na hapo ndipo imani hiyo inapokuwa na nguvu kwelikweli.
Kwa mfano uliotolewa na dada Yasinta, yote hiyo ni imani za kutengeneza tu, hakuna ukweli wowote.
Kwangu mimi jina ni jina hakuna jina baya balitafsiri zetu ndio mbaya.
Nimeshangaa kumsikia mwana utambuzi mwenzangu Kamala kwamba ilibidi aachane na jina lake la ubatizo kwa sababu eti lilikuwa halimfai, kwa bahati mbaya hakusema kwamba lilikuwa halimfai kivipi? kama angesema lilikuwa na mkosi, ningejua nimsaidie vipi mwanutambuzi mwenzangu lakini hakutoa sababu.
Ipo mifano mingi inayodhibitisha nguvu hizi za kutengeneza>
Kwa mfano Nchini Marekani, wanaamini kwamba mtu hawezi kupata Urais kama jina lake halina herufi G, O au W, na ndio sababu ukichunguza marais waliotawala katika nchi ile majina yao hayakosi herufi hizo.
Na hapa nchini kwetu inaaminiwa kuwa Herufi M ndio inatawala, kwa hiyo ukichunguza marais wetu wote majina yao yana Herufi M.
MWALIMU JULIAS KAMBARAGE NYERERE
ALI HASSANI MWINYI
BENJAMINI WILLIAM MKAPA
JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Na hata kwa upande wa mawaziri wakuu ni hivyo hivyo.

Naomba kuwasilisha.

Mtambuzi, Shabani Kaluse