Tuesday, November 25, 2008

Wazazi katika uchaguzi wa majina.

Pengine niifanye hii kuwa "SPECIAL". Na kama ntaulizwa kwanini ntajibu ni kwa kuwa ni kutoka kwa watu special juu ya kitu special. Yaani waliochagua jina nao wana la kusema kuhusu uchaguzi wa jina. Wazazi wangu wanasema

"Ni kweli kuwa ni vigumu kumwambia mtoto maana ya jina pale unapompa lakini ni kweli pia kuwa mtoto akipata ufahamu anaweza ama kujisikia vema au vibaya kutokana na jina alilopewa na wazazi, hii huwalazimisha wazazi kutafakari maana kabla ya kutoa jina. Maana hata kama jina laonekana kuwa limepinda au la kimizengwe, huwa kuna sababu za jina hilo na wazazi wakiulizwa maana wanaweza kusema. Ni vema kuchagua kwa makini jina la mtoto, maana katika kutoa jina si vema kuangalia mambo ya karibu sana na yanayopita, bali ni vema kujua kuwa jina lenye laana hulaani na lenye baraka hubariki.
Tunakutakia yaliyo mema na kama jina lako lilivyo basi uendelee kubarikiwa na kuneemeka. Hizi ni sala za wazazi wako."

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Kama kuna kitu najivunia basi ni maisha. Na maisha yanatanuka kuanzia kwa vile niishivyo mpaka wale niishio nao. Lazima nikubali kuwa maisha yangu yako yalivyo kutokana na historia yangu na kwa ajili ya mstakabali wangu pia. Kubwa ni kujua kuwa tuko tlivyo kulingana na tulivyokuzwa. Na hata kama hatukui na wazazi, wale walezi waliohusiana na wazazi wanawakilisha sehemu ya uzazi. Na ndio maana kama unakulia kwa familia iliyoungana na yako, ni kwa kuwa waliokutangulia wamekubaliana nao. Kwangu nimepitia familia njema na najivunia mengi kuanzia Wazazi mpaka walezi kama Baba na Mama wadogo, Wajomba na Shangazi, Kaka na Dada na maShemejina marafiki waliokuwa kiasi cha kufikia "undugu wa hiari". Wote hao niko nao kulingana na malezi ya awali na najivunia kila jema nililonalo nikikumbuka kuwa chimbuko lake ni familia njema niliyokulia.
Nawashukuru wazazi na walezi wangu wote kwa haya na kwa namna mnavyoendelea kuniunga mkono katika mengi mema niendeleayo kuyatenda.
NAWAPENDA