Tuesday, December 16, 2008

Hongera Father Kidevu na wanahabari wote.

Waziri Membe akimvisha tuzo Father Kidevu Waandishi wa Habari walioshiriki katika Oparesheni Democrasia Comoro wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe baada ya kutunukiwa Nishani za Anjoun.MSTARI WA MBELE TOKA KUSHOTO: Assa Mwambene, Mwantanga Ame, Bernard Membe, Faraja Kihongole na Khalfan Said. katikati toka kushoto: Victor Gunze, Manyerere Jackton, Stanley Ganzel na Sudi Mnete. NYUMA TOKA KUSHOTO: John Mapinduzi, Joseph Damas na Mroki Mroki
Hii Leo mmoja kati ya watunza kumbukumbu na wahabarishaji mahiri nchini Mroki Mroki maarufu kama Father Kidevu ametunukiwa nishani ya Anjoun ambayo imeenzi juhudi zao za kuhabarisha umma wakati wa Vita ya kumuondoa muasi wa visiwa vya Comoro Mohamed Bakar.
Father Kidevu ni kati ya waandishi 12 waliotunukiwa tuzo hizo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete
Mroki ni kati ya Bloggers mahiri kwa habari na picha ambaye licha ya misukosuko na vikwazo vingi kazini, bado anaendelea kutuhabarisha kupitia blog yake unayoweza kuiperuzi kwa kubofya hapa
Kwa niaba ya wana-Changamoto, napenda kumpongeza Father Kidevu kwa kazi anayoifanya ambayo kupitia kwake blog hii hupata taswira nyingi za kusindikiza habari na matukio mbalimbali. Pia kwa wahusika wa tuzo hizo kwa kutambua mchango muhimu walioutoa wanahabari hawa na kwa wanahabari na vyombo vya habari vyote nchini kwa ushirikiano walioutoa kwao wote walioshiriki katika haya.
Blessings

1 comment:

Simon Kitururu said...

Hongera kwa Father Kidevu na wana habari wenzake kwa mchango wao katika habari!

Bila watu kama hawa habari kibao zinabakia kuwa siri kwetu wengi tuliombali na tukio.