Friday, December 19, 2008

Them, I & Them. LUCIANO: Bandits

Luciano akiingia jukwani

Luciano na The MessenJah Band wakitumbuiza ndani ya Ukumbi wa Zanzibar On The Waterfront uliopo Washington DC May2, 2008
Ni kweli, Changamoto Blog nayo ilikuwepo
Kama kweli twaangalia Ulimwengu wa sasa ulivyo, basi tutakubaliana na Luciano kuwa umejazwa watu wenye mioyo ya tofauti. Wenye kutesa wasio na uwezo na wenye uhitaji. Watu wenye kujali maisha yao binafsi hata kama itamaanisha kutoa uhai wa wengine na kuwanyonya zaidi wale wenye kuhitaji msaada.
Luciano ambaye ni mmoja wa wasanii ambao wameendeleza jukumu lake la kuunganisha maisha yetu ya sasa na kusudi la Muumba katika maisha yetu anatueleza namna aonavyo ulimwengu wa sasa ulivyojaa watu wenye kusulubisha wenye uhitaji, kupokonya kidogo walichonacho watoto na wahitaji na cha kusikitisha ni kuwa wale wafanyao kazi ndio wanaokabiliana na ugumu halisi wa maisha, ilhali "some of claims they're bosses, all they do is steal"
Tumsikilize mwenyewe Luciano hapa kwenye wimbo wake Bandits kutoka albamu yake ya Great Controversy aliyoirekodia nchini Uingereza na moja kati ya albamu zake za zamani ambazo bado zina washabiki wengi. SIKILIZA MWENYEWE UJUMBE NDANI YA MUZIKI KISHA UOANISHE NA MAISHA TUISHIYO SASA, VIONGOZI WETU WA SASA NA "SIASA" ZITAWALAZO ULIMWENGU SASA
Kujua mengi juu ya Luciano bofya http://www.lucianoreggae.com/

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**

3 comments:

Anonymous said...

hay sasa umekuwa rastafarian tena, mbona hupigi visu sasa,Wahaya bwana mna mambo kweli kweli.

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaha. Safi sana Anon. Naona umetimiza nia ya kuwa na sehemu ya maoni. Yaani kusema kile udhaniacho ni sahihi. Na huo ni uhuru wa na haki yako. Lakini pia sehemu kubwa ya Blog hii ni KUELIMISHA, KUBURUDISHA na KUKUTOA KATIKA UTUMWA WA KIAKILI. Yaonekana umenasa kwenye utumwa udhaniao kuwa kila mtu ni balozi wa kabila lake. Si mimi. Ni kweli kuwa mimi ni mhaya halisi na najivunia hilo (maana hata Bob alisema "you can't run away fro yourself") na Bukoba ndiko kwetu (ambako Luciano alisema "i'm rooted and grounded") na kwa namna yoyote ile sitaweza kupakana. Lakini pia siwezi kuchukuliwa kama kielelezo cha tabia ya kabila zima. Na wala siwezi kumchukulia yeyote kama wakilisho la kabila lake pia. Ni njia ya kutugawa iliyopandikizwa vichwani mwa wavivu wa kufikiri ili kutugawa (kama Nasio alivyosema kuwa "these are ways and means to divide the people"). Kama hujatambua hilo unasikitisha. Kikubwa ni kuwa kila mtu ana kabila lakini hakuna balozi wa kabila. Kwa hiyo kusema "wahaya bwana mna mambo" ni fikra za kikabila (na ubaguzi pia) ambazo naamini hazistahili kuendelezwa maana ziliznzishwa na zinaendelezwa na wenye nia ya kutugawa kwa propaganda za kutujali na kutupenda. Sijui wawaza nini, lakini pengine Kaluse angekusaidia katika UTAMBUZI NA KUJITAMBUA ili Bwaya naye akusaidie uJIELEWE yale ambayo Kitururu atayaona MAWAZONI mwako katika MAISHA azungumziayo Da Yasinta.
Anyway; Hii ndio raha ya blog, kujua nani anawaza nini na kwa mtazamo gani. Maana sote twaweza kuona tatizo, japo namna uonavyo tatizo, ndilo laweza kuwa tatizo.
Karibu tena

Simon Kitururu said...

@Mzee wa Changamoto: Kwa jinsi ulivyojibu hoja , labda asiyeelewa ni profesa wakutoelewa.

Nazimia sana kazi za Luciano.