Friday, January 23, 2009

Them, I & Them. BUSHMAN: Give some more

"Tell me when will some clothes be issued to the naked, tell me when the hungry will be fed, tell me when will some shelter given to the homeless, ... can't you see the're dying there?"
Ndivyo anavyouliza Bushman katika "bridge" ya wimbo wake Give Some More ambao anaonekana kuwaeleza wanasiasa ni nini wanategemewa kufanya kwa jamii iliyowachagua. Bushman aliyeanza kwa kuwa muwazi akisema "politicians are deceiving" anaendelea kwa kueleza kuwa wanasiasa tuwategemeao ndio haohao watupelekao kubaya anaposema "cause the ones who are suppose to make it easy, are the same who are making it harder" na kuwaonya juu ya pesa na ahadi zao hewa wazitumiazo kupata nafasi walizonazo wakati wa kampeni.

Sijawahi kuona VIAPO vya ma-rais wetu, lakini natumai na kuamini kuwa wanaapa kulitumikia taifa na wananchi kuwatekelezea yale wahitajiyo kwa mujibu wa katiba na Ilani. Na ninapoangalia hali za Zimbabwe, Guinea, Congo, hata Tanzania kwenyewe napata mashaka kama kauli wazitumiazo huwa wanamaanisha ama ni njia ya kupata nafasi walizonazo. Njaa, magonjwa, vita na matatizo lukuki ambayo yanaendana na ka-mfumo ka kujuana na kubebana ambako kanasababisha maisha ya wengi wasio na hatia kudumaa kwa miaka mingi wakati wenye nafasi, madaraka, uwezo na wajibu wa kutengeneza maisha bora kwa kila mwananchi wakineemesha mafao yao

Basi kwa kuwa wanaelekea kutekeleza mipango ya Mwaka huu mpya, nawaomba kutimiza zaidi kwa wenye uhitaji kwa ku-GIVE SOME MORE TO THE POOR EVERYDAY

Bofya player hapo chini kumsikia Bushman akiwaeleza juu ya kuwajali waliowaweka walipo ndani ya wimbo GIVE ME SOME MORE toka albamu yake ya HIGHER GROUND,

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

1 comment:

Koero Mkundi said...

Hii inatosha, ujumbe umefika kaka.

"politicians are deceiving, cause the ones who are suppose to make it easy, are the same who are making it harder"