Friday, December 12, 2008

Zilipendwa za RTD hizi hapa kwa Da Subi

Zimepatikana zile za enzi ile ya External Service of RTD, Kijaluba hoyeee, (na watangazaji mahiri Mikidadi Mahamoud, Uncle J Nyaisanga...) na matangazo ya Vicks Kingo na sijui Meza Action mara ukiumwa na misuli tumia Salimia Liniment... tangazo la Revola (Vipi Mama Mariam! mbona unalalamika hivi? Ah, nguo hizi, kila ninapokazana kuzifua, hazitakati sijui nitumie nini?)...., zile hadithi za Bi Deborah Mwenda za Ua Jekundu, Binti Chura, Mbalamwezi Nyota Begani nk..... kiasi zipo hapa na hapa (nenda mwisho wa ukurasa)
Wikiendi njema!
Subi

NB: Kurasa ya burudani kwenye tovuti ya Da Subi ni mahala unapoweza kupata Habari, Nyimbo na Burudani mbalimbali kutoka vituo vya BBC Swahili, DW-Swahili, VOA-Swahili, Radio Japan-Swahili, Radio Maria, Jambo Radio, Bongo Radio, Ngoma Moto Vibes, Capital Fm, Taarifa za Habari toka Radio One na Radio Free Africa (RFA), Nyimbo za Injili na hizo za RTD. Ni ONE STOP kwa habari na burudani toka nyumbani. Bofya hapa kuelekea huko moja kwa moja.
ENJOY!!

4 comments:

Subi Nukta said...

Mkuu Mzee wa Ch...
Asante kwa kusambaza habari na kwa kufurahia Zilip...
Ujirani mwema huu!

Mzee wa Changamoto said...

Ni stahili yako Dada. Hakuna la ziada tunaloweza kufanya zaidi ya kuthamini yale ambayo wenye nia njema na juhudi zetu wanafanya. Ufanyayo si kwa ajili ya Subi pekee, bali ni kazi za kuhabarisha na kuburudisha wengi walio mbali na nyumbani.
Tuko pamoja Dada

MARKUS MPANGALA said...

mmmmmm kazi tamu hiyo hakika nimesadiki

Subi Nukta said...

Mzee wa Ch...chz,
Nashukuru kwa kunipamba nami najihisi kuku katika jamii ya vifaranga.

Mkuu rafiki Markus, nafurahi zaidi ikiwa nawe umefurahia pia zilipendwa.

Daima pamoja waTz!