Saturday, January 17, 2009

CHEMSHA BONGO. WHAT IS LIFE?????

Najua tafsiri ya kitu kama maisha itatokana na namna mtu alivyokua na anavyoendelea kuishi. Na pengine inaweza kupingana na mwingine kwa kuwa tu hawako katika tafsiri, tathmini na mtazamo mmoja wa maisha. Najaribu kufikiri maisha ya aliye Msasani, Dar na yule wa kijijini Kibondo, Kigoma, ama wa Nangurukuru, Lindi na wa Rubafu, Bukoba kama yanaweza kuwa na tafsiri moja. Lakini je pia kwa aliye Tanzania ambaye amezaliwa na kukulia katika amani na aliye Palestina ambaye kwa takribani nusu karne anaona mauaji yatakuwa na tafsiri moja?
Ni wapi tunapoweza kujenga tafsiri moja ya maisha ambayo haitaleta tofauti yeyote ya thamani na tabaka kulingana na mazingira, imani, itikadi na migawanyo mingine?
Innocent Galinoma aliwahi kusema "some they say life is a gift from GOD, some they say life is a dream, some they say life is a mystery" na akaendelea kuuliza "is life a dream, or a test, or a punishment to my people?
Nami nauliza WHAT IS LIFE?
Msikilize Inno alipouliza "what is life" labda ataweza kuwa msaada kufikirisha
CHEMSHA BONGO NJEMA

5 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wengine wanasema maisha ni kuwepo (existane) wengine ni utukizi (coincidence) wengine wanasema ni malengo, japokuna waishio bila lengo. wengine wanasema ni kishi tuu.

kumbuka haizuii ukweli kwamba tunaishi hata tusipojua maisha ninini!
binadamu wa leo anazidi kuwa kichaa, maisha yanamkimbiza badala ya yeye kuyakimbiza.

kila mtu anadefinition yake ya ya maisha. kwa mfano mtwiba atakwambia maishi ni kuikimbia Bk na Bongo na kwenda states

Mzee wa Changamoto said...

We Kamala weweeee!! Nani kakwambia kuwa nimekimbia Bongo, nimekuja kusaka maisha japo naanza kuisaka tafsiri yake kwanza na nikigundua inasema ni kurejea home basi "ntajimuvuzisha" Bongo kuyamalizia. Lakini kuna hatua ngapi za maisha (mbali na zile za kuzaliwa na kufa)? Kuna kusaka ubora wa maisha na huko ndiko kuletako yote haya. Kunaleta amani na kuleta vita maana wote waanzishayo na kuendeleza hayo wanataka kula tu. Lakini wapi penye maisha? Kijijini unakokula kitu kinavyostahili kuwa ama mjini ambako ng'ombe anadungwa ma-homorne mpaka ndama wa miezi miwili ni mkubwa kuliko anavyostahili kuwa akiwa na miaka miwili? Kwani raha ya maisha ni nini? Kuoa ukawa mume wa fulani ama "kuwepo kuwepo" kama Kamala?
Hivi maisha ni nini?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tatizo lako ulianza kusaka maisha kabla ya kutafuta definition yake ndo maana ukaenda States, sasa umepotea, uko porini night kali!!!! (jicheke kidogo kwanza)

sasa hizo hatua wewe huzisemi, labda mimi ntasema kuna ya kuzaliwa bush kwenu, kwenda BK town, MZ, DAr, US embasy na story za Uongo na kweli, na sasa US, hizo ni step za maisha, sijui!!!

unaongelea ndama mnaokula huko kwenu eh? I dont share such a meal. wewe kama bado unakula maiti za viumbe hai, mimi simo na sitokuwemo kabisa kwa walji hao.

maishi ni kujitambua, na ukaishi kwa furaha halisi na amani ya kweli na upendo vilivyomo ndani mwako, japo hujagundua kama vimo ndo maana unavitafuta nje yako!!!!!

maisha ni matamu na mazuri japo wengi mnasema ni magumu. kama unaishi maisha ya kulamba ice cream, nyama na ya kukumbushwa kuwa unadhambi kila Jpili, mimi simo, na ninasema simo.

maisha, maisha,

Mzee wa Changamoto said...

Hahahaaaaa. Kweli namna uonavyo tatizo ndilo Tatizo Kamala.
Nami simo

Simon Kitururu said...

Labda wenye uhakika na tafsiri moja ya maisha wamekufa na mpaka tufe tunaweza kuwa na uhakika kwa kuchungulia waishiyo kama wanachungulika:-(